Elections 2010 Hofu Uchaguzi Igunga Tume na dalili za Uchakachuaji Karatasi

Giddy Mangi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
830
184
Imenipatia wakati Mgumu ghafla baada ya kupokea simu na kuulizwa kama ninaweza kukodisha lorry langu na kupeleka Karatasi za kupigia kura Igunga,huku masharti ya kazi hiyo ni pamoja na uzito ni Tone 2.5,usafiri lazima uwe Fuso na bei isizidi Million 1 laki 2.

Huwezi amini hii kazi amepewa mtu tena dalali asiye na gari wala kampuni iliyo sajiliwa kisheria.Biafra Kinondoni na anatafuta usafiri usiku huu.Tume hii ni aibu kwa Serikali inayotumia Helcopter 2 kwenye campaign lakini inakuja na budget ya kubeba nyaraka muhimu kama karatasi za kupigia kura.

Kwanini isingetumia shirika la Posta kama Tume halina magari ya kufanya kazi hiyo.
 
hilo gari halikatizi saranda likijitahidi mwisho sekenke, ah natania tu bandugu!
 
Inatakiwa safari kuanza kesho Alfajiri na kusambazi karatasi hizo jimboni Igunga.
 
Imenipatia wakati Mgumu ghafla baada ya kupokea simu na kuulizwa kama ninaweza kukodisha lorry langu na kupeleka Karatasi za kupigia kura Igunga,huku masharti ya kazi hiyo ni pamoja na uzito ni Tone 2.5,usafiri lazima uwe Fuso na bei isizidi Million 1 laki 2.Huwezi amini hii kazi amepewa mtu tena dalali asiye na gari wala kampuni iliyo sajiliwa kisheria.Biafra Kinondoni na anatafuta usafiri usiku huu.Tume hii ni aibu kwa Serikali inayotumia Helcopter 2 kwenye campaign lakini inakuja na budget ya kubeba nyaraka muhimu kama karatasi za kupigia kura.Kwanini isingetumia shirika la Posta kama Tume halina magari ya kufanya kazi hiyo.

Nina wasiwasi na ukweli wa habari uliyoiweka
 
mkuu, biashara kichaa hiyo.
1.2m uende igunga una kichaa?? labda singida.

anyway, mkuu, unajua ccm kila kitu ni deal tu!! yule jamaa wa loliondo safaris pale biafra kwenye ofisi ya ccm ya kata ndo amepata hiyo deal, yeye huwa hana gari yoyote, kwa hiyo anatafuta bei rahisi, then yeye anavuta kubwa na mgao wa aliyemkatia hilo pande.

thats how it works, hata kwenye mambo nyeti kama haya.
 
Inasikitisha sana haiwezekani wana Igunga wanasubiri kumpata mwakilishi wao Bungeni kumbe kabla ya Uchaguzi tayari walishaandaliwa Mbunge.
 
Back
Top Bottom