Hofu miongoni mwa wana CCM ni udhaifu wa siasa za Hayati Magufuli: Rais Samia anajiamini

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Kumeibuka mada na mijadala mingi hapa JF na mitandao ya kijamii kutoka miongoni na wafuasi wa CCM inayokosoa, kulaani au kulalamikia mwenendo na misimamo ya utendaji wa Rais Samia. Zaidi kinachoendelea kwenye mijadala hii ni kumtaka Rais Samia “avae mabuti” na kupita njia za mtangulizi wake Hayati Rais Magufuli katika utendaji wake.

Lakini kitu kibaya katika mijadala hii ni pale wanapotoa maoni yao kwa kumchafua, kumdharau na kuonesha kwamba SSH hatoshi katika nafasi ya urais. Bila shaka wanatambua hawawezi kumlazimisha Rais kutekeleza misimamo wanayoitaka wao, ile ya JPM. Matokeo yake wanamchukulia Rais Samia kama msaliliti wa CCM na JPM na kwa maana hiyo wameamua kutumia njia ya “kujilipua” kupambana naye.

Mathalani kwenye mijadala yao wanatangaza na kuonesha miradi iliyokamilika kuwa imehusika na ufisadi katika utekelezaji wake na kwamba ufisadi huo husingetokea chini ya Magufuli. Unaweza kujiuliza kama kuna mradi wowote ulionzishwa na kukamilika ndani ya miezi miwili ya utawala wa SSH. Wengine wanakosoa dhamira ya SSH ya kuifungua nchi kwa madai kwamba inalenga kuirudisha nchi kutoka kwenye uchumi wa kujitegemea na kuwa nchi masikini na tegemezi kwa misaada ya wafadhili. Wanadiriki kutoa shutuma hizo kana kwamba chini ya uongozi wa Rais Magufuli nchi haikuwahi kuomba na kupokea misaada kutoka kwa wafadhiili.

Mapambano na chuki za wana “CCM mpya” (MATAGA) dhidi ya SSH zimekuwa zikiongezeka kadiri anavyoendelea kutangaza na kutekeza misimamo ya uongozi wake. Alipotangaza dhamira ya kutozingatia itikadi za kisiasa katika kuteua viongozi na watendaji serikalini wafuasi wa siasa za JPM wamechukia. Lakini kumtengua mkuu wa wilaya ya Hai, Sabaya, ambaye ni miongoni mwa wawakilishi muhimu wa siasa na misimamo ya JPM kumewakwaza sana MATAGA. Wanamshutumu Rais kuwa anasikiliza na kutekeleza mapenzi ya wanasiasa wa upinzani na kwamba kwa kitendo hicho anahatarisha uhai wa CCM.

Kwa mitizamo hii ya wafuasi wa JPM juu ya hatua zinazotekelezwa na Rais SSH ni dhahiri kwamba chama chao kilishapoteza nguvu ya ushawishi na sasa hakiwezi “kutoboa” kwenye siasa za ushindani kwa “kuwachekelea” wapinzani. Kwa maneno mengine, CCM kinahitaji viongozi “wakuda” na wenye uwezo wa kusimamia “siasa za JPM” kama akina Sabaya na Ndugai. Hawaamini kama CCM ingetoboa kwenye jimbo la Hai au Arusha Mjini kama si ukuda wa Sabaya.

Ninaposema siasa za JPM namaanisha siasa za ubabe zinazotumia mbinu za ulaghai, vitisho, utekaji na ahata mauaji ya raia au wanasiasa wakosoaji. Siasa za JPM hazilengi kujenga nguvu ya kukubalika CCM kwa raia na wapiga kura. Katika siasa za JPM kura za wananchi katika uchaguzi si kitu muhimu cha kukipa CCM ushindi na kwa maana hiyo mgombea wa CCM hana haja ya kuonesha unyenyekevu mbele ya wapiga kura. Kutokana na kushindwa kupata ushawishi kutoka kwa wapiga kura, siasa za JPM zilijikita katika “ku-deal” na washindani wao katika chaguzi.

Kushindwa kupata ushawishi na kupuuza umuhimu wa wapiga kura katika siasa za ushindani ni udhaifu wa siasa za JPM ambao ndo msingi wa hofu miongoni mwa wafuasi wake. Wafuasi wa Magufuli wanatambua dhaifu huu wa chama chao kwamba msingi wa ushindi wa chama chao hautokani na kura za wananchi bali ni kutokana na ku-deal na washindani wao ambao leo Rais SSH “anawachekelea”.

Hadi hapa, napenda kutoa angalizo kwa vyama vya upinzani kwamba wasistarehe kwenye kiti cha anasa na kuota jua la asubuhi wanapomuna Mama SSH akiwatumbua viongozi dizaini ya Sabaya. Bali wafuasi wa siasa za JPM wasihofie hatua zinazochukuliwa na “Bi Mkubwa” dhidi ya viongozi wanaowaamini kuwa ndio msingi wa “ushindi” wa CCM. Cha muhimu hapa ni kutambua kuwa Bi Mkubwa anajiamini na ana kila sifa ya kuwa mwanasiasa bora na imara kuliko mtangulizi wake Rais JPM. Kama wapinzani wanamkubali Bimkubwa, maana yake ana nguvu ya ushawishi na huo ndo uhakika na uhalali wa ushindi wake kwenye siasa za ushindani. Bali wafuasi wa siasa za JPM wanatakiwa kuwa “flexible” na “ku-oscillate” na midundo ya Bimkubwa, vionginevyo ataendelea kuwaengua na wasiweze kumkwamisha.
 
Utaishia kutukanwa na MATAGA. Sijajua kwanini hawampendia Mama Samia
 
Kila dakika inayopita bila katiba mpya mataga wanazidi kuwa hatari kwa ustawi wa taifa hili endapo utawala utarudi mikononi mwao, tutakuja kujuta.
 
CCM haina agenda tena za kuwaeleza watanzania ndiyo ililazimika kuongoza nchi kibabe
Enzi za mwenye nguvu mpishe sasa ni enzi nyingine za kuunganisha nguvu. Neno la wakenya la harambee lafaa sana sasa. Ubabe mama ameuweka pembeni
 
Jukwaa ni la moto sana kwa ccm maana hawana ushawishi tena kwa watu
Ushawishi wa ccm haupo hapa jukwani.

Ccm yenyewe inafurahi sana mnavyohangaika na vi ishu vidogo kama hivi!

Badala ya kujadili ishu nyeti nyie mmekomaa na Sabaya!

2025 utaijua ccm kama ipo hapa jf au iko huko field
 
Kila dakika inayopita bila katiba mpya mataga wanazidi kuwa hatari kwa ustawi wa taifa hili endapo utawala utarudi mikononi mwao, tutakuja kujuta.
Kwani sasa hivi uko kwa nani?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom