Hofu kubwa vikao vya CCM; huenda wanachama sita maarufu ndani ya chama hicho nchini wakatimuliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu kubwa vikao vya CCM; huenda wanachama sita maarufu ndani ya chama hicho nchini wakatimuliwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  HOFU kubwa imetawala miongoni mwa makada wa CCM kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba huenda wanachama sita maarufu ndani ya chama hicho kikomgwe nchini wakatimuliwa katika vikao vya juu ambavyo vitafanyika kaunzia mwishoni mwa wiki hii na kumalizika mapema wiki ijayo.

  Vikao hivyo ni vile vya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) kitakachotanguliwa na Kamati Kuu ya CCM (CC) ambavyo vitaongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

  Juzi kulikuwa na kikao cha maandalizi wa maofisa wa makao makuu wa CCM na jana Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Willson Mukama ilikutana kuandaa vikao hivyo ambavyo uamuzi wake unasubiriwa kwa shauku kubwa.

  Wakati maandalizi hayo yakiendelea habari kutoka ndani ya chama hicho zinadai kwamba hofu kubwa iliyotawala ni kuwepo kwa taarifa kwamba huenda makada sita ambao ni wanachama wakongwe wa CCM (majina tunayahifadhi kwa sasa) wakasimamishwa uongozi na wengine kutimuliwa uanachama kutokana na tuhuma kwamba wanakivuruga chama hicho.

  Habari za uhakika ambazo Mwananchi limezipata zinadai kwamba tayari watuhumiwa hao wa vurugu ndani ya CCM wameitwa mbele ya Kamati ya Maadili ambayo itafanya kikao chake leo au kesho chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete.

  Miongoni mwa tuhuma zinazowakabili makada hao ni kutoa kauli zinazokinzana hadharani, kupinga uamuzi halali wa vikao vya juu vya chama na kuendesha siasa za makundi ambazo zimekigawa chama hicho tawala.

  Mmoja wa wanaotajwa kuitwa mbele ya kamati ya maadili, alilithibitishia Mwananchi kupokea wito huo na kwamba atakwenda mjini Dodoma kusikia kile alichoitiwa.

  "Unachokisema ni kweli, nimeitwa kwenda mbele ya kamati ya maadili ijapokuwa sifahamu sababu ya wito huo, nitakwenda kusikiliza halafu nifahamu kile nilichoitiwa huko huko,"alisema kada huyo ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa moja ya mabaraza ya jumuiya za CCM.

  Jumuiya za CCM ni tatu ambazo ni Umoja wa Wanawake (UWT), Jumuiya ya Wazazi na Jumuiyaya Umoja wa Vijana (UVCCM).

  Maazimio ya NEC
  Kikao cha NEC kinakutana miezi minne tangu kilipokutana mara ya mwisho na kutoa maazimio ambayo yalisababisha mmoja wa makada wake, Rostam Aziz kujiuzulu ubunge katika jimbo la Igunga pamoja na ujumbe wa NEC.

  Rostam katika kujiuzulu huko aliitupia lawama sekretarieti ya chama hicho kwa kile alichokiita kuwa ni kuendesha siasa chafu dhidi yake na kuwataja kwa majina Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, John Chiligati na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuwa wahusika.

  Kujiuzulu kwa Rostam ambako kulifanya Bunge kutangaza nafasi wazi katika jimbo la Igunga mkoani Tabora, ni miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi kubwa katika mjadala wa CC na NEC.

  Katika mazingira hayo, kuna kika uwezekano wa kutathini jinsi falsafa ya kujivua gamba ilivyotekelezwa na kama ni Rostam peke yake ambaye alipaswa kuchukua uamuzi wa kujindoa kwenye nafasi za uongozi wa juu wa CCM.

  Habari zaidi zinadokeza kuwa Sekretarieti ya Mukama nayo imegawanyika katika suala la utekelezaji wa uamuzi wa NEC, hali inayoongeza sintofahamu ndani ya chama hicho.

  Kutokana na mambo yalivyo, busara ya Mwenyekiti, Rais KIkwete inatarajiwa sana kuchukua nafasi ili kuepusha uwezekano wa mgawanyiko kuwa mkubwa zaidi baada ya vikao hivyo.

  Hali ilivyo Dodoma
  Mmoja wa makda wa CCM aliliambia Mwananchi juzi mjini Dodoma kuwa kuna uwezekano wa hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya makada ambao wanatoka katika makundi ambayo yamekuwa yakipigana vita ndani ya chama.

  Alisema: "Kutokana na hali hiyo, kila kundi linafanya jitihada za kutafuta wafuasi wa kuliunga mkono ili watu wake wasifikwe na adhabu inayokusudiwa kutolewa".

  "Kuna taarifa kwamba Mwenyekiti (Rais Kikwete) amechoshwa na siasa hizi za kuviziana, sasa tunasikia kwamba ameamua kuchukua hatua na kuna uwezekano wa baadhi ya makada wenzetu wakafukuzwa kabisa uanachama".

  Katika kuthibitisha hali ilivyo tete, wabunge wanne wa CCM, wakiwamo mawaziri wawili kwa nyakati tofauti waliliambia gazeti hili kwamba hawatakubali mtu wao ang'olewe.

  "Mimi (anamtaja jina) akifukuzwa uanachama, basi hata mimi najiuzulu ubunge, huyu bwana ni mtu muhimu sana na ni brain ya chama, lakini hawa jamaa eti wanataka kumfukuza nadhani hilo halikubaliki,"alisema mmoja wa wabunge kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Mbunge mwingine alisema vita ndani ya CCM ni harakati za Urais wa mwaka 2015. "Ujue (anamtaja jina) anaogopwa sana kwamba anaweza kuwa Rais 2015, kila mmoja anamwona tishio hivyo anaandamwa kutoka kila kona, lakini ukiona hivyo ujue kwamba anafaa, kama mnaweza na ninyi tusaidieni basi".

  Tangu kuanza kwa kikao cha Bunge wiki iliyopita, baadhi ya makada wamekuwa wakiwashawishi baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa NEC kuwa na msimamo wa kuwaokoa wale wanaolengwa kufukuzwa ndani ya CCM.

  Miongoni mwa mbinu ambazo zimepangwa ni kupendekezwa kwa Mwenyekiti kwamba mtu asichukuliwe hatua bila kupewa nafasi ya kujieleza mbele ya kikao hicho na kwamba hatua hiyo inalenga kutoa mwanya wa mapendekezo ya kuwanusuru baadhi yao.

  "Hakuna mtu atakayechukuliwa hatua bila kusikilizwa, hilo tutalisimamia maana hiyo ndiyo natural justice kwa kila mtuhumiwa, na tukifanya hivyo tutafanikiwa tu,"alisema Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Kaskazini.

  Hali ndani ya CCM
  Kikao hicho pia kinafanyika wakati ambao kumekuwa na misigano miongoni mwa makada wa chama hicho tawala nchini hasa kuhusu jinsi Sekretarieti ya Katibu Mkuu Mukama inavyotekeleza maazimio ya kikao cha mwisho cha NEC kilichoridhia mabadiliko makubwa ndani ya chama hicho.

  Hatua ya Nape na Chiligati kutajwa na Rostam katika hotuba yake ya kujiuzulu aliyoitoa jimboni Igunga kwamba ni miongoni mwa viongozi waliopotosha nia njema ya kukivusha CCM katika matatizo yanayokikabili ni ishara kwamba kazi itakuwa kubwa wakati wa kikao cha NEC.

  Kujiuzulu kwa Rostam kulitafsiriwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya NEC hasa baada ya yeye (Rostam), Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kutajwa kwa majina kuwa ni miongoni mwa wanaotakiwa kujivua gamba kufuatia kutajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi.

  Tangu kutolewa kwa taarifa hiyo, hiki ni kikao cha kwanza cha juu cha CCM kukutana na taarifa hiyo ya Msekwa ambayo inachagizwa na kujiuzulu kwa Rostam huenda ikawasilishwa na kujadiliwa na NEC.

  Pia Msekwa siku chache zilizopita alikutana na wenyeviti wa CCM wa mikoa, huku Mukama akikutana na makatibu wa mikoa katika vikao visivyo vya kikatiba vilivyofanyika jijini Dar es Salaam kutafakari hali ilivyo ndani ya chama.

  Habari kutoka ndani ya vikao hivyo zilidai kwamba utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba ulipingwa vikali kwamba unakigawa chama hicho.

  Katika kile kinachothibitisha kuwepo kwa misigano miongoni mwa makada wa CCM, mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu wiki hii aliliambia Mwananchi mjini Dodoma kuwa "Wanachama wengi wa CCM hawafurahishwi na ziara za Nape na washirika wake mikoani," kwamba zinaweza kukigawa chama badala ya kukiimarisha.

  "Kwa mfano unapowataja watu watatu tu kwamba ndio wanaopaswa kujivua gamba una maanisha nini, Mimi nadhani si haki kabisa, hawa jamaa wanataka kutupeleka mahali ambako siko,"alisema mjumbe huyo wa CC.

  Siku chache zilizopita, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake, Benno Malisa uliingia katika mvutano na Nape, baada ya kutoleana kashfa hadharani.


  Mwananchi - 18 November 2011
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mbombo ngafu
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  haituasadii hii taarifa. Katiba kwanza.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Inavyoonekana watamshusha cheo Nape Nnauye au kuupa Ubunge na CC awe Mjumbe asiye na Madaraka

  Yuko kasi zaidi ya hivyo Vizee vya CC Malecela 85ysOld, Msekwa 87yrsOld, Kingunge 90yrsOld, Mwinyi 88yrsOld,Mkapa 76yrsOld, na wengi wengine
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  ahsante CCM kwa kuruhusu mauaji ya kimbari nchini
   
 6. M

  Malova JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  tunajua kwamba ndai ya ccm kuna watu wazuri wanaotetea maslahi ya watanzani. na hao lazima waende tofauti na ccm wengine kwasababu ya ubabe. mfano mzee SITTA, penye ukweli anaongea ukweli lakini ccm huonesha ukweli palipo paovu na uovu palipo na ukweli.so najua watu kama Sitta waweza kuwemo ktk sita wa kufukuzwa
   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  mbona vikao vyenyewe vinachelewa? Nalog off
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mimi hapa posho tu....raha ukialikwa na ccm ku-cover matukio yao. Ku-cover hapa inamaanisha dont cover a damn thing...halafu wewe unapewa libaasha la kaki lenye zile noti mpya.
   
 9. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Fijo Nkamu !
   
 10. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja washikane uchawi wao kwa wao!
   
 11. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  ..........CCM-A wameanza, CUF a.k.a CCM-B watafuata.
   
 12. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #12
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kila la kheri ila wasipigane tu
   
 13. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kufukuza wanachama na hasa wabunge si kazi rahisi kihivyo "Malema mwenyewe kasimashwa kwa miaka 3 ajifunze adabu ila bado mwanachama robo"
   
 14. j

  jigoku JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja ya kuwapongeza CCM aka Magamba kwa kufanikisha mauaji ya KIMBALI nchini kwetu Tanzania.Ila somo la Endurance tumefuzu pia,hivyo tutakwenda sawa na kwa watakaokufa basi,lakini huku tutakaowaacha basi wawe wamepunguza matatizo,shida na ikibidi kuyamaliza kabisa.
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,710
  Trophy Points: 280
  Hata wakitaka kuuana wote sawa tu kwani wana faida gani hao magamba? Mijitu kutwa nzima inaleta mipasho bungeni.
   
 16. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tunasubiri.
   
 17. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CCM sasa kumekucha, naomba mrudisha Imani kwa Watanzania, fukuza wote wanaoyumbisha Chama.
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  sika sunga
   
 19. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Hiyo hofu ingekuwa iko CDM ningeamini, lakini CCM hawana utamaduni wa kuwajibishana, hawana historia hiyo alikuwa nyerere tu wengine hakuna awezaye.Rostam KAJIUZURU AU KANG'ATUKA KAMA NYERERE HAJAFUKUZWA.Shughuli ya kuwajibishana kwa uwazi iko CDM bana utawapenda wale jamaa transparency 100%
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Fitusu fya kyinja
   
Loading...