"Hofu"- Kitabu cha Wiily Gamba kitukumbushe madhila yaloipata Tanzania kwenye miaka ya 70, kinachotokea sasa hivi ni mrejesho?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Mtunzi wa kitabu cha "Hofu" Elvis Alistablus Musiba aliona mbali, aliona hofu ilotawala taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa kitabu hicho Musiba anaeleza kuhusu dhahama hizo, kuanzia mwaka 1978 ambapo mambo yalikwenda mrama.

Kwanza, Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika, kukazuka, na ukame pia ambao uliathiri uchumi wetu.

Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia havikutupatia hata senti tano wakati huohuo wenzetu walipewa mamilioni ya fedha za kigeni.

Hayati Mwalimu Nyerere alijitahidi kuomba fedha IMF na World Bank lakini walikuja na masharti mengi tu ya kukatisha tamaa.

Wenzetu hao Uganda, Kenya na nchi zingine za Afrika ambazo zilifaidi fedha hizi za kigeni zilipiga kasi kimaendeleo ingawa si katika sehemu kubwa ya jamii zao.

Kwenye kitabu hichi cha Hofu, mpelelezi Willy Gamba anakabiliana na vikosi vya kukodi cha ilikuwa utawala wa kidhalimu wa Afrika Kusini ambao ulikuwa unapanga kuwadhuru baadhi ya viongozi wa nchi za kusini mwa bara la Afrika yaani wapigania Uhuru.

Lengo kuu likiwa ni kuchelewesha uhuru wa nchi hizo na kukandamiza jitihafda zote za kuimarisha uchumi wa nchi hizo ambazo zilikuwa zikisaidia nchi zingine kusini mwa Afrika kupata uhuru.

Willy akiwa na timu nzima ya majasusi kutoka nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini na Kenya wanaweka mkakati wa kukabiliana na njama hizo za makaburu.

Kuna upendo mkubwa sana baina ya mataifa ya Afrika upendo ambao katika miaka ya hivi karibuni umeonekana kudorora.

Hofu ni kitabu cha kukumbukwa kwani kinatufundisha mengi juu ya udhalimu wa kikundi cha watu wachache waliopo nje ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Hivi sasa Tanzania inakabiliana na nguvu kubwa ya mashirika ya kimataifa na hata Umoja wa Ulaya kiasi kwamba fedha za msaada zimezuiwa.

Kuna mambo kama 15 hivi ambayo yameoanishwa ikiwa ni masharti ya kurejeshwa kwa misaada hiyo.

Nadhani sasa hivi tunao akina Willy Gamba wa kutosha kukabiliana na hili la sasa iwe ardhini , kwenye mitandao au hata hukohuko maeneo ya tukio iwe Brussels au Washington.

Kukabiliana huko kusitumie pupa wala papara bali kuwe kwa akili sana.
 
Hiyo akili ingekuwepo tusingeona mabox ya kura yakitolewa vituoni mbele ya jeshi la polisi na kwenda kujazwa kura za ccm. Tunafanyiana hujuma wenyewe kwa wenyewe, saa hii hatua zinachukuliwa na wenye uwezo ndio mnataka liwe suala la wananchi wote. Ni nani hakuona hujuma ya wazi kwenye uchaguzi wa Znz? Wakati wa ile hujuma si tuliona jeshi likitumika kwenda kuwapa ccm ushindi? Hizi chaguzi za marudio wote si tunaona jinsi box la kura linavyochezewa na ukatili wa kutisha? Kwa kuwa vyombo vya dola vimekubaliana kuitumikia ccm na sio nchi, acha wazungu wachukue hatua mpaka tujifunze kuheshimu sheria zetu. Ingekuwa hakuna hujuma tungekuwa pamoja, lakini kwa hujuma hizo za wazi tutawaunga mkono wazungu. Tumechoka na dhuluma. Huwezi kuleta maendeleo kwa kuheshimu mifumo ya sheria kaa pembeni waingie wanaoweza.
 
Sasa hivi watu wana Hofu ya kumuogopa Jiwe.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Acha "HOFU"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom