JENDALUJEJE
Member
- Nov 18, 2012
- 43
- 22
Hodi naipiga humu,JENDALUJEJE nasema,
:violin:Imeniingia hamu,Jukwaani kuja sema,
Mawazo mengi matamu,ya kumeza si kutema,
Hodi mi nasema hodi,ndio kwanza naingia.
Jamvini nasogelea,KARIBU naisubiri,
Kwa pupa sitoingia,subira yavuta heri,
Enyi mlotangulia,nasema SABALKHERI,

Midomo mkifungua,tabasamu mkaweka,
:violin:Woga shaka nitavua,na imani nitaweka,
Ndugu mkinitambua,makazi nitayaweka,
HODI MI NASEMA HODI,NDIO KWAANZA..NAINGIA!