music mimi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 456
- 791
Asalam alleykum!
Nimepata kibarua Zanzibar nategemea kuhamishia makazi huko. Binafsi sijawahi kabisa kufika Zenj napasikia tu. Picha niliyonayo kuhusu Zanzibar ni ninayoisoma kwenye media na kuona kwenye media.
Wakuu naomba wale mnaoishi huko haswa wenyeji mnisaidie yafuatayo.
1. Eneo zuri la kupanga nyumba ni lipi, binafsi napendelea maeneo tulivu ila isiwe mbali na mji.
2 Bei za nyumba huko ni kiasi gani kwa nyumba ya kawaida self contained ya vyumba vi2 au vi3. Na utaratibu wa kupata nyumba huko upoje (huku Dsm tumezoea kutumia madalali)
3 Ni mambo gani natakiwa kuyaepuka mimi kama mgeni nikifika huko ili nisipate shida kuishi na wenyeji wangu. Mimi ni mkristo pia ni mkurya. So ningependa kujua mambo haswa ya kiutamaduni yanayoweza kuwa mageni kwangu ili nisipate tabu kuishi na watu.
4 Mimi ni mnywaji (sio mlevi) je kuna sehemu rasmi za kupata mambo yetu yalee ukiacha hayo mahotel ya kitalii.. Kuna clubs au pubs.?
5 Napenda ujasiriamali kwa sasa nna kikampuni cha usafi hapa Dsm... Je huko ni fursa gani au eneo gani naweza kuwekeza kwa biashara isiyoitaji supervision yangu ya 100% kwa kamtaji ka million 4 mpk 6 hivi.
6 Nikitaka kupata mchumba wa kinzazibar kuna tatizo? Maana naambiwa huko ni mwiko kutoka na mbara, eti wazazi wa binti wakijua wanaweza kukutumia 'umeme'
7 Nikitaka kuonana na kufahamu wabara walio huko.nawapata zaidi vipi na maeneo yapi?
NB usinishauri nisiende nimeshafanya maamuzi ya kwenda.