Hodi hodi kutoka kwa Kiranga

Leo umekuja na style tofauti kabisa, sijaamin kama ni wewe!

Kila lakher mkuu
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,
Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.
Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.
Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.
Natanguliza ungo wa shukurani
Kwa leo ni hayo tu,
Wasalaam,
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
 
Ha haaaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom