Hodi hodi kutoka kwa Kiranga

Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
71,277
105,475
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,

Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.

Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.

Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.

Natanguliza ungo wa shukurani

Kwa leo ni hayo tu,

Wasalaam,

Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
 
Kiranga wa ngeda!, Oyee!!

Vigelegele!
Karibu!

Hapa ni JF...na kwanguwote:D ni JF Ville!

Kula Breki!!!

:D:D:D:D

Sina breki za mbavu!
 
Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa

Karibu sana.
Asante kwa kiswahili kizuri kweli kiswahili ni lugha mahiri

Naomba unipe ufafanuzi kuhusu maswali yangu

1. Kwa nini majina ya sehemu ulizotaja mengi yameongozana mawili mawili
kwa mfano Songo Songo, Somanga Funga, Kilwa Kivinje, Mbwa maji na mengineyo.

2. Yanaandikwaje kwa usahihi?
Kwamfano Mbwamaji hujaacha nafasi katikati lakini Sala-Sala umeacha nafasi

Mwisho, Ukiweza naomba unitafsirie ujumbe wangu hapo chini kwa kiswahili fasaha

Wasalaam
 
ECONOMIST,
Mtazamo wako ni mzuri.
Keep it up.
 
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,

Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.

Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.

Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.

Natanguliza ungo wa shukurani

Kwa leo ni hayo tu,

Wasalaam,

Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa

Kiranga karibu tena karibu sana, si haba kutufikiria kwa kutaka tujaalia japo kwa pepeta. Ukipitapita jijini tupitie vilingistoni, karibu ya kwa mtoro, kahawa tutaku kirimu, kashata za hapo pia si haba.

Mbawala vipi huko? au mmesha wabanjuwa wote?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom