Hodi hodi jamvini

TWIZAMALLYA

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
397
81
Ninayo furaha kubwa sana kujiunga na wana jamiiforums. kitu kilicho muhumu ni kwa wana Igunga kutoendelea kufanya makosa yaliyowafanya waishi katika hali ya umasikini mkubwa sana.Niliwahi kuishi huko Igunga aka mwambiti tarafa ya Igurubi. Enzi hizo kulikuwa na basi moja tu kati ya Igurubi na nzega liitwalo MAKOYE MEMBE. Maisha ya pale yalikuwa hell on earth.Unatembea kilomita 15 kutafuta maji ambapo utapata maji ndoo moja tu kwa tabu siku nzima. watu wa igunga wana mtindo wa kuchimba visima fulani vya kienyeji wakati wa masika na kuvifunikia kwa juu kama wafunikavyo vyoo vya kijijini. wakati wa mvua maji yanakuwa yanatiririka kwa juu na baadhi yanaingia ndani ya kisima. wakati wa kiangazi wanafunua hivyo visima ambavyo hata hivyo huishiwa maji baada ya muda mfupi sana kwani sehemu kubwa ya wilaya ya igunga ardhi yake haitunzi maji(mbuga kwa kisukuma).Visima hivi vinajulikana kwa jina la MAKOMELO.Hali ya maisha ya igunga inazidi kuwa mbaya sana,hata hayo makomelo they are no more kwa sababu ya hali ya mvua kutokuwa nzuri.Fisadi hajafanya kitu chochote pale.Huwezi kuamini kwamba Igunga ni kawida mtu kwenda mtoni na kuanza kunywa maji ya mto ambayo wanyama kama ng'ombe na mbwa wanakunywa. Hii ni kutokana na tatizo kubwa la maji lililopo Igunga.

Ni wakati wenu wana Igunga kufanya mabadiliko ili muweza kuonja mema ya nchi. Ubungo tulifanya maamuzi sahihi ambayo hata mwaka haujaisha tunaona mabadiliko. watu wa kimara,mbezi na Golani mtakuwa mashahidi wangu
 
Karibu sana jamvini, nadhani wana Igunga watakuwa wamekusikia.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom