HKigwangala: Msururu Muhimbili ni sababu ya Huduma Bora

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,600
5,803
Naibu wa Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto ameandika hivi ktk Facebook page yake:

Msongamano wa watu Muhimbili unaakisi ubora wa huduma zinazotolewa.
Hakuna mtu angeenda pale kama huduma zingekuwa mbaya! #AskHK

Je hii ndio sababu hasa ya msongamano Muhimbili¿¿
 
kwa nini wasiweke huduma bora na hospital zingine ili kila mtu asikimbilie Muhimbili?huyu si waziri wa afya Tanzania nzima?Boresheni hospitali zote Tanzania
 
Salim tulifikiri ni mmoja wa wale kumbe ni chuki za kiimani ndio zinamsumbua. Ata hivyo tutatuma mtu amtazame tujiridhishe.
 
Huyu jamaa ni kiazi... Na ni jipu... Kama ndio kama matatizo yakiwa mengi na wagonjwa wakiwa wengi ndio inamaanish kuwa huduma ni bora basi tuna safari ndefu sana bado
 
Hufikiria nini kabla hajaongea na kutenda huyu???
Kuna mambo hutakiwi kuyasema katika namna ya namna hii hata kama Kuna ukweli, Sawa na mstaafu aliyesema msongamano wa magari ni dalili ya maendeleo!!
 
Huduma bora ni pamoja na kuutoa huo msongamano.
Akina mama wanajifungulia chini halafu unasema kuna Huduma bora....?
 
Huyu jamaa ni kiazi... Na ni jipu... Kama ndio kama matatizo yakiwa mengi na wagonjwa wakiwa wengi ndio inamaanish kuwa huduma ni bora basi tuna safari ndefu sana bado

Kuchukua Mashine ya CT Scan kutoka Dodoma na kuileta dar kisha watu wa Dodoma kuja Muhimbili.
 
HK, ameandika haya katika FB account yake akiwa na akili timamu kweli au zilikuwa twisted na kilevi kwanza?

Kina mama kulala wanne wanne, wawili wawili ktk kitanda kimoja na wengine kutambaa sakafuni na matumbo yao ni kwa sababu ya huduma bora kweli??

Ama kweli hawa viongozi wanadhani sisi wananchi ni viazi sana na kwamba akili zetu ni kama zimeathiriwa na ulaji wa viwavi!!

Usishangae hata waziri wa elimu naye akaja kusema kuwa uwingi wa watoto madarasani hata wengine kukosa madawati na kulazimika kukaa chini kwenye mavumbi au kusomea chini ya miti ni ishara ya MFUMO BORA na UBORA WA ELIMU itolewayo ktk shule zetu!!

Hawa ndiyo viongozi wa kizazi cha HAPA KAZI TU!!

Kwani; wagonjwa kulala wanne, watatu, wawili juu kitanda kimoja;

Au; watoto 140 kurundikana ktk darasa moja na wakiwa wamekaa chini ni kwa sababu ya HAPA NI KAZI TU kudadadeki!!!
 
Kigwa ni miongoni mwa mawaziri vilaza sana. Yeye haoni kuwa mlundikano Muhimbili ni dalili mbaya kuwa hospitali zingine zimetelekezwa? Huduma huko ni mbovu?
 
Kigwa ni miongoni mwa mawaziri vilaza sana. Yeye haoni kuwa mlundikano Muhimbili ni dalili mbaya kuwa hospitali zingine zimetelekezwa? Huduma huko ni mbovu?
Unayo hoja ya msingi kabisa. Laiti Amana, Mwananyamala na Temeke zingeboreshwa, wengi wangeishia huko.
Lakini hizo nazo zinahitaji vituo vya afya viwe imara - watumishi wakutosha, vifaa tiba na madawa ya kutosha.
Vituo vya afya pia vinahitaji zahanati ziboreshwe.
 
Kigwa ni miongoni mwa mawaziri vilaza sana. Yeye haoni kuwa mlundikano Muhimbili ni dalili mbaya kuwa hospitali zingine zimetelekezwa? Huduma huko ni mbovu?

Huduma bora ni pamoja na kukaa miezi mitatu ukisubiri kipimo cha CT-Scan ??
 
Huyu waziri ziro kabisa. Wakati anatangazania akiwa kwenye mdahalo wa mkikimkiki aliwahi kusema kuwa "hjawahi kuona hospitali yenye upungufu wa vitanda mpaka wagonjwa wanalala chini" hadi leo bado upungufu upo.
 
Naibu wa Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto ameandika hivi ktk Facebook page yake:

Msongamano wa watu Muhimbili unaakisi ubora wa huduma zinazotolewa.
Hakuna mtu angeenda pale kama huduma zingekuwa mbaya! #AskHK

Je hii ndio sababu hasa ya msongamano Muhimbili¿¿
Mungu tuhurumie,hivi huyu mwenye kauli hizi ndio alijiaminisha kujaribu kutaka kuwa Rais wa Tanzania,haya.
 
kwa nini wasiweke huduma bora na hospital zingine ili kila mtu asikimbilie Muhimbili?huyu si waziri wa afya Tanzania nzima?Boresheni hospitali zote Tanzania
Mnajadili mistari tu ma critics....!!!
Jadili yoote na yaliyokusudiwa na kigwangala katika andiko ilo kwenye fb
Alafu mnajiita wakosoaji.... Nyie ni wapotoshaji...

Wazo hili la kuboresha hospitali za tmk, amana na m/nyamala mbona hamsemi kama ndio mpango unaotekelezwa na wizara?????

Mimi sio nyumbu asilani
 
Back
Top Bottom