Hizo pesa za kuninulia vifaa vya sport bunge zipelekwe Mashuleni kununua madawati

kahembe

Member
Mar 22, 2015
74
53
Nimeona kwenye taarifa ya habari ya ITV Leo tarehe 30.11.2021 sh. Mil. 20 zimetengwa kwa ajili ya kuninulia vifaa vya Michezo ya wabunge ili Hali shule nyingi asa za msingi watoto hawana madawati wanakaa chini. Huo ndo uzalendo wa viongozi wetu au wanafanya hivyo kisa watoto wao hawasomi katika hizi shule?
My intake Waziri wa Elimu na Waziri Tamisemi Tenga Muda wa kuzungukia Halmashauri na jaribu kuingia kwenye kata kuliko kuishia wilayani.Yaani huku Katani Hali ni mbaya.
 
Pia nimeona leo ITV waziri wa Elimu amesema kuna pesa za ujenzi wa shule hivyo wanategemea kujenga shule 1000 hasa kwa kata zisizo na shule za sekondari
 
Michezo ni afya, ni elimu, ni heshima, ni nadharia, na ni vitendo...

Kwa Waheshimiwa Wabunge kutengewa 20M binafsi naona ni ndogo kwasababu wanajianda na michezo ya Mabunge Afrika Mashariki, pamoja na kuboresha afya zao pia watajifunza kwani wao ndio wapitisha bajeti za michezo ktk Wizara.

Ikumbukwe kitendo cha kukutana Nchi majirani kidiplomasia ni heshima kubwa sana, hapo bado hatujawashinda ktk michezo.

Mwisho ni Nadharia kwa wasioshiriki na Vitendo kwa watakaoshiriki.
 
Back
Top Bottom