mtambuzi tamba
New Member
- Nov 1, 2010
- 1
- 0
Mimi ni mmoja wa wale ambao tumechoshwa na ufisadi, hivyo napata faraja kubwa sana ninapoona haya matokeo yanayotolewa hapa kuwa mafisadi wanaelekea kupigwa chini. Lakini sasa napatwa na wasiwasi kama hizi habari ni sahihi au ni ushabiki tu wa kisiasa? Kwani naona kama matokeo yanataka kuja kinyume, jamani mnapoandika hizo habari mhakikishe mmezifanyia uhakiki wa kutosha, ili muweze kutupa data zilizo sahihi hasa sisi tuliyopo nje ya nchi.