Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Wakati wengi wakiamini kuwa Baba Mwenye Nyumba amekimbia makazi yake kutokana na hatari ya vile vijidudu,binafsi nimekuwa na mtazamo wa ziada kuwa mbali na hiyo kuweza kuwa ni moja ya sababu,lakini kitendo cha kukaa huko muda wote huu kwangu naanza kukiona kama ni dalili nyingine ya Baba huyu kuichoka na kutoipenda tena kazi yake na hivyo huenda akaamua kukaa pembeni jambo linaloweza kuwashangaza na kuwashitua wengi.
Hali hii inayoendelea inaashiria amepoteza hata mood ya kazi na huku kusemwa pengine ndio kabisa kunachangia kumkatisha tamaa ya kuendelea kukalitia hico kiti hivyo ni bora tu abaki ajipumzikie.
Wadau,binafsi naamini hali hii si ya kawaida na huenda kuna jambo haliko sawa kumuhusu na ambalo linafanywa siri kwa sasa.
Anaweza kurudi anakotakiwa kuwepo ila anaweza kufanya hivyo kwa lengo la kupunguza maswali au mashaka yanayoonza kujitokeza ila baada ya muda ataondoka tena na kurudi kijijini kwake.
Narudia,hali hii si ya kawaida unless ni katika kuuguza ingawa sababu hii nayo bado haiwezi ku-justfy kukaa kwake nje ya ofisi yake kwa muda wote huu.
Nahisi ni kama anaaga na wakati huo huo anawaandaa watu kisaikolojia.
Hii ingekuwa ni tabia yake,basi ingejitokeza tangu siku za mwanzo anaingia ofisini na leo isingekuwa ajabu lakini sio kuanza tabia hii kipindi hiki na kusiwe na sababu iliyolazimisha.
Moyo wa mtu ni siri nzito.