Nape tangu amekuwa mwenezi wa CCM hakuwahi kukutana na ziara ngumu kama hii anayoendelea nayo kanda ya ziwa. Ugumu wa ziara si kukosa watu kwenye mikutano tu, bali zomea zomea iliyoikumba ziara yake na katibu mkuu wa Ccm ndg Kinana. Ilianzia pale Bukoba Nape aliposema meli iliyohaidiwa na Kikwete si kipaumble, wananchi wakamzomea. Kule Mleba alipojaribu kumpamba Prof Tibaijuka wananchi wakamzomea, aliposhuka tu Nkwenda wilaya ya Kyerwa boda boda wakazomea Nape akashika shati lake na kusema "ZOMEENI TU LAKINI HATA KWA DAMU SHATI HILI NDO LINAINGIA IKULU" haikuishia hapo jana akazomewa mpaka akwaambia watu wamekunywa viroba vya Chadema.
Kwingineko Zitto naye ameonja joto ya jiwe kule Geita, Momba na Mbeya mjini, Zitto kwa upande wake anakutana na kasheshe hiyo pale anapojaribu kukikosoa chama chake cha zamani au viongozi wake. Mfano Mbeya mjini alikumbana na dhahama pale alipomkosoa Mbowe kutembelea shangingi la kiongozi wa kambi ya upinzani. Zitto alilazimika kujitetea kwamba wanaozomea ni wale wanaoamini wanasiasa kupindukia kiasi cha kuaminshwa kwamba yeye ni MSALITI.
Kwa ujumla hizi zilikuwa wiki mbaya kwa vijana hawa, lakini je siku mbaya kwao zimepita? Kwa kuwa mara nyingi Zitto huzomewa kila anapojaribu kuisema Chadema, atafanyaje siasa bila kusema alifukuzwa Chadema kwa nini? Kuhusu Nape siku zake zinaweza kuwa zinahesabika kwa vile mara nyingi mwenyekiti mpya wa Ccm huja na sekeritarieti yake, lakini je kwa muda aliyobaki nao ajipambanue namna gani? asiiguse Chadema wakati ndiye mpizani wake mkuu?