Wakuu, nina imani kila mmoja wetu amekuwa akijiuliza kwanini serikali imelikalia kimya suala la Makonda kuwa na vyeti feki. Binafsi nadhani hizi ndo sababu za msingi zinazomfanya Makonda asigusike;
1. MANGE KIMAMBI
Wote tunajua kuwa Mange ni mbaya wa mkulu wetu kwani amekuwa akimuandama mara nyingi kwa kuibua kashfa mbalimbali ikiwemo ya Makamu wa Rais kutaka kuachia ngazi. Katika hali kama hiyo mkulu hawezi kutengua uteuzi wake kwa kuwa tu imeibuliwa kwa mara ya kwanza kabisa na mbaya wake.
2. MAADUI WA MAKONDA NDO MAADUI WA MKULU
Kumekuwa na tetesi kuwa asilimia kubwa ya walotajwa na Makonda ni wale ambao hakuwa na uhusiano nao ulio mzuri. Na ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa wengi wao hawako katika uhusiano mzuri na Rais. Mfano Manji, Mbowe na Gwajima. Hivyo suala lililoibuliwa kutokana kuguswa na wabaya wa Mkulu linakosa mashiko kwa mkulu mwenyewe.
3. MKULU KUTANGAZA WAZIWAZI KUMKUBALI MAKONDA.
Wote tunajua kabisa kuwa kabla ya ishu ya madawa, tayari mkulu alishatangaza waziwazi kumkubali Makonda. Katika hali kama hii ni ngumu kuja kumtumbua kirahisi.
4. VYAMA VYA UPINZANI
Asilimia kubwa ya wanaopaza sauti kuhusu Makonda ni wa vyama vya upinzani. Hii inazifanya mamlaka husika kutolitilia mkazo suala hili. Hii imepelekea hata baadhi ya wanaCCM wanaolipigia kelele kuonekana wasaliti!
NB; Haya ni mawazo yangu, unaruhusiwa kunikosoa, kuongezea, kuyakubali lakini pia kuyakataa.