Hizi Tuhuma kwa Waziri Kangi Lugola, zina ukweli?

ninanukuu '
Ndipo ulifuatwa tena na wafanyabiashara ukiwa Dodoma na wakakuleta Arusha kwa gharama zao na malazi juu yao, unakumbuka ulitoa plate namba za gari ya serikali na wakakulipia Hotel Naura spring.
Hapa uliwahakikishia kuwa kuwa unakwenda kumaliza kazi lakini UKAWAOMBA WAKUCHANGIE UJENZI WA SHULE YAKO.
Ni kweli umetimiza na umetumbua na sasa unapokea changizo la 20ml kwa wafanyabiashara hao.'

Wavaa miwani watashughulikia na kupeleka majalada kwa bosi wao
 
Huyo jamaa acha kabisa
uyo DTO bihahamulo ni mchapakazi safi sana yaan huyo alikuwa kanyooka sio bodaboda,sio mwanajeshi ,sio polisi mwenyewe sio mwalimu wote aliwashughurikia kwa mujibu wa sheria ndio maana ata jina lake walimwita Trump
 
Mleta mada ni polisi mla rushwa,mh lugola kabana sana kwa sasa na anafuatilia vilivyo.

Lugola ni waziri wa mambo ya ndani ambaye kiukweli kabisa anachapa kazi,amewabana sana polisi wote wapenda rushwa,ubabe na polisi wote wasiopenda kufuata sheria.

Mh lugola chapa kazi,mkuu bado ana imani na wewe,na kamwe usikatishwe tamaa na baadhi ya askari wachache wasio waadilifu.
 
Huyu ndiye Lugola
Anaandika Kiseju;
Mheshimiwa sana Kangi Lugola salaam;
Napenda niseme machache yanayokuhusu;
MINONG'ONO YA VITENDO VYA RUSHWA
Mheshimiwa kumekuwa na malalamiko na minong'ono inayokuzunguka hasa ya kujinufaisha wewe binafsi kupitia wadhifa wako kama ifuatavyo;

1. Unapokea rushwa kuwasafisha baadhi ya maafisa wenye tuhuma za rushwa ama walioharibu.
Hili ulilifanya Oldonyosambu Arusha...
Ulimsafisha mmoja wa watendaji wako huku ukijua wazi alitolewa kituo flani kwa kuwabambikizia wananchi kesi na kupora mashamba yao na alihamishwa baada ya upepo kuchafuka, wewe ulimsafisha na kumrejesha Ngaramtoni.

2. Uliwatumbua RPC Ilala, Temeke, na Arusha kwa maslahi yako binafsi na wala hukufanya utafiti kwa yale uliyoyasikia. Inasemekana ulipokea chochote kuwawajibisha.
TUME
Iliundwa tume ya ufuatiliaji hizo tuhuma ulizowatuhumu na matokeo yake ofisi yako haikuwa tayari kutoa ushirikiano, unakumbuka tume ilivyojaribu kuomba ushirikiano lakini haukuwa tayari na meishowe ulitoa ushirikiano hafifu sana.
Tume ilijiridhisha kuwa tuhuma ulizotoa na kuwatumbua hazikuwa na ukweli ndio maana RPC wa Temeke alirudishwa kwenye nafasi yake na kupewa Mkoa wa Njombe.

3. TUHUMA ZA KUWATUMBUA WANAOCHAPA KAZI KWA UAMINIFU NA WELEDI
Kama tujuavyo kila anayesimamia haki na kutokupokea rushwa huwa hapendwi na wavunja sheria.
Katika hili umeumiza wengi kwa kuahidiwa CHOCHOTE ILI UWASHUGHULIKIE.
--Naomba nikukumbushe;
-umefanya vikao kadhaa Mwanza na kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara wazito ili uwaondoe DTO ulipokuwa Tilapia na Kingdom hotel Mwanza ili uwaondoe kama ifuatavyo;
-Biharamulo
-Mikumi
-Mkalama
-Manyoni umeondoa watumishi wawili.
Hawa ni watu wasiokuwa na mchezo na kazi zao lkn bila huruma umewapiga chini kwa MASLAHI BINAFSI YA KUSAIDIWA PESA ZA UBUNGE Mfanyabiashara anachangia 10ml na umewaomba wakusaidie ujenzi wa shule yako na mchango unaendelea baada ya kutimiza kazi waliyokutuma.

TUHUMA NYINGINE
Hivi karibuni tena umemtumbua RTO Arusha kwa kile ulichosema kuwa hatekelezi maagizo yako?

Huyu Bukombe ni nani asiyejua utendaji wake?
Kila alipofanya kazi aliacha alama...fuatilia utendaji wake Mwanza, Singida, Mara na Arusha alishainyoosha na inasadikika hakukuwa na ubabe barabarani tena.
Ukweli wa mambo ni huu hapa;
-Uliletewa malalamiko na wafanyabiashara mwaka jana mapema kuwa umwondoe kwani amewabana barabarani kwa madereva wao wanapelekwa mahakamani kwa uvunjivu wa sheria.
Mnamo tar 22/7/2018 ulikutana na baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara na wakakukabidhi $25,000, na baada ya kupokea ukiwa na furaha uliwaahidi kuwa kesho yake ungemtumbua katika kikao cha wewe, wafanyabishara ya wasafirisha watalii na uongozi wa mkoa wa Arusha.
Si unakumbuka ulijaribu kumtumbua kwa madai ya kitoto?
Eti hakujibu swali lako kwa usahihi?
Unakumbuka RC Gambo alikwambia umwache ni mchapakazi na haoni kosa katika majibu yake?
Baada ya hilo kukwama ulipanga njama na uongozi wa waendesha bodaboda ili waje kumtuhumu pale Kilombero kwenye mkutano wako ili umtumbue?
Hapo napo alitoa maelezo mazuri ukakwama tena kumtumbua.
Ndipo ulifuatwa tena na wafanyabiashara ukiwa Dodoma na wakakuleta Arusha kwa gharama zao na malazi juu yao, unakumbuka ulitoa plate namba za gari ya serikali na wakakulipia Hotel Naura spring.
Hapa uliwahakikishia kuwa kuwa unakwenda kumaliza kazi lakini UKAWAOMBA WAKUCHANGIE UJENZI WA SHULE YAKO.
Ni kweli umetimiza na umetumbua na sasa unapokea changizo la 20ml kwa wafanyabiashara hao.

MALALAMIKO YA MA RPC
Kumekuwa na malalamiko ya chini chini kuwa unawalazimisha ma RPC wakulipie hotel na mambo mengine...je posho za safari unazopewa na wizara unazifanyia nini?
Rais Magufuli analijua hili?

KUTOKUHUDHURIA MATUKIO MABAYA;
-Hukuhudhuria Njombe mauaji ya watoto, Simiyu mauaji yale wala hujawahi kufika maeneo yaliyokuwa tete kama Kibiti nk lakini umekuwa bize kushughulikia maslahi binafsi.

Natamani ungejitokeza kujibu tuhuma hizi nami nitoe vielelezo na ushahidi hapa.
Jumapili njema.
 
Back
Top Bottom