Uchaguzi Igunga na Pepo za Mabadiliko Tanzania

Hongereni sana viongozi na wanachama wote mliojishughulisha kwenye uchaguzi mkuu katika jimbo la igunga. CDM imepata kura nyingi (Iwe zimechakachuliwa au la) , Ccm imepata ushindi mwembamba japokuwa wamemiliki jimbo hilo kwa miaka 18. Msife moyo tuendelee kupigana
kwani utawala wa CCM unaelekea ukingoni.

ni kweli kaka. kutofautiana kwa kura 3000, si nyingi kwani jitihada zikiwekwa za kusambaza elimu ya URAIA kwa wananzengo, WE SHALL OVERCOME in 2015 election.

BRVO CDM, BRAVO JAMII 4RAMU, BRAVO MEMBERS WA JAMII FORAMU, naamini tumechangia kwa kiwango kikubwa kupokonya ushindi wa CCM toka aslimia alizopata yule KUPE, ukilinganisha na KUPE huyu mpya.
 

Hela mlizo zi invest Igunga ingekuwa kufungua matawi yangekuwa 1578, mmepata pigo kubwa sana hamna furaha na mmeanza kusambaratika

Kama hatukuwa na matawi igunga lakini tumeweza kuvuna kura 20,000+ hilo pigo linatoka wapi? asiye na furaha ni nyie magamba A na mshirika wenu ccm-B.
 
CHADEMA Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee........ Huu ni mwanzo mzuri wa kisiasa Igunga...... Kura hizo ni ushindi wa CDM mwaka 2015
 
Uchaguzi huu wa Igunga, nafikiri umeipa joto ya jiwe CCM. Wakati kampeni za vyama vingine, haca Chadema na CUF inafanywa na wananchi wenye uchungu na nchi yao; lakini CCM inafanya kampeni kwa kutumia Rais Msatafafu, Rais aliyeko madarakani na viongozi lukuki waliotawala hii nchi yangu enzi za Nyerere - ambao wananchi wa kawaida wanalazimika kuwaamini hata kama wanaumia = kwa mtaji huo, hata kama CCM ingeshinda kwa 75% BADO HIYO NI KUSHINDWA TU. Ni aibu. Haina tofauti na watu wanaongojea matokeo ya timu ya Simba wanaocheza na watoto wa darasa la 5 la shule fulani. Mwisho wa mchezo, wanashangilia ua kuwa simba imeshindwa kwa kuipachika darasa la 5 goli 2 bila.

CCM ingekuwa inajiamini, ingemwachia mbunge aliyekuwa anagombania na viongozi wa chama wa mkoa, kama asingeambulia patupu. Kwa mtaji huo, CCM muone aibu kuchangilia mtakachokiita ushindi. Rudini kazini, shughulikieni kero za walalahoi, pamoja na wana Igunga.

Nataka niwapongeze Chadema kwa ujasiri wao wa kuweka mambo wazi. Tunawaelewa, tunayaona, yanatuumiza.Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
 
Tusivunjike moyo makamanda wote wa cdm, ninapokaribia kukata tamaa huwa nakumbuka ukweli hushinda, tz imejaa watu katili na mafisadi wakora vibaya sana wasio na hata chembe ya uzalendo kwa taifa hili, lakini pamoja na hayo yote pamoja tutashinda.hongereni sana makamanda wangu wote mliopigana vita ile ya haki na uhuru wa pili kwa wanaigunga tangu kuanza kwa kampeni.poleni kwa yote, aluta kontinua......

True that
 
Kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu Tanzania wa Oktoba 2010, tumeshuhudia pepo kubwa sana zikivuma kwa kasi kutoka pande zote za nchi yetu. Ni pepo za mabadiliko. Wananchi wanataka madadiliko ya kweli. Watawala walioko kwenye ngazi kubwa za nchi hii ama wamezisikia au kuziona hizo pepo lakini bado hawajaonesha jitihada za kuzizuia. Ni mwanzo wa miti mikubwa yenye nguvu kubwa (Key Politicians) kuangushwa chini na pepo hizo. Ni wakati ambapo watawala hawataamini kilichofanyika.

Mabadiliko haya yamenikumbusha Hotuba makini na ya kihistoria ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mr Hrold Macmillan alipotembelea Afrika na tarehe 3 Februari 1960 na akahutubia maelfu ya watu huko Afrika ya Kusini, na kusema:

"The wind of change is blowing through this continent (Africa), and whether we like it or not, this growth of national consciousness is a political fact. We must all accept it as a fact, and our national policies must take account of it." - Harold Macmillan.

Kwa uchaguzi huu, tutarajie mabadiliko makubwa yanakuja.... Nguvu ya umma ni kila kitu. Wazambia wamefanya. Ni zamu yetu mwaka 2015 kwa kutumia mtaji tulioupata Igunga na kwingineko. Mnasemaje wadau???
 
Imekaaje hii? Inatupatia picha gani? Kutoka 35,000+ hadi 26,000+: na kutoka 0 hadi 23,000+; na kutoka 11,000+ hadi 2,000+.

Kwa wasioelewa nasema niniu, hizo na tarakimu za kura walizopata vyama vikuu vitatu katika uchaguzi mdogo Igunga, zililinganishwa na zile za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
 
What had happened in Igunga over the weekend is a clear reflection of the 2015 elections. CCM will triumph again in 2015. CCM will retain the majority seats in the congress and the presidency as well.
 
Imekaaje hii? Inatupatia picha gani? Kutoka 35,000+ hadi 26,000+: na kutoka 0 hadi 23,000+; na kutoka 11,000+ hadi 2,000+.

Kwa wasioelewa nasema niniu, hizo na tarakimu za kura walizopata vyama vikuu vitatu katika uchaguzi mdogo Igunga, zililinganishwa na zile za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Spanner, you've cheered my heart - which was bleeding! Bravo comrade.
Uchaguzi ungefuata system ya USA ya 'electoral college' CDM ingechukua helm.
 
Imekaaje hii? Inatupatia picha gani? Kutoka 35,000+ hadi 26,000+: na kutoka 0 hadi 23,000+; na kutoka 11,000+ hadi 2,000+.

Kwa wasioelewa nasema niniu, hizo na tarakimu za kura walizopata vyama vikuu vitatu katika uchaguzi mdogo Igunga, zililinganishwa na zile za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Hii ina maana CCM wameshuka kwa 26% huku CUF wakishuka kwa asilimia 18%.Wakati huohuo CDM wamepanda kwa asilimia 23,000%.Hili ni ongezeko kubwa la kihistoria kwa maana hiyo, mathematically CDM ni washindi CCM hawana chao 2015.
 
iko wazi kwamba CCM zote mbili yaan A na B zinashuka kwa kasi ya ajabu,kufikia 2015,watakua hawana chao.
 
I still do not believe that only 33% of registered voters turned out to vote.
 
Ila walioumia zaidi ni CUF kwanza ni nyumbani kwa Lipumba. Nadhani Lipumba afikirie kustaafu pia
 
Binafsi nawapongeza CDM kwa matokeo hayo sikutarajia naamini hiyo ni asilimia ya ongezeko wakati wengine wamepata asilimia za upungufu wakijipanga vizuri kabla ya 2015 kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa 2014 kuhakikisha kupenya mpaka ngazi ya vitongoji, pia kuhamasisha vijana kujiandikisha.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom