Hizi tabia 'hutaweza fanikiwa milele'

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,828
Naonaga watu wanahangaika mno na ujasiriamali
mara semina ya wapi sijui
mara wajaribu biashara hii na ile

lakini watu hao wengi wana tabia ambazo zinawafanya wasifanikiwe
hata wafanyaje...

hizi ni baadhi ya tabia hizo...

1. kutokupokea simu unapohitajika....
watu wengi wana shida sana na matumizi ya simu
unapiga wee ..hadi una ghairi....

2.kuajiri ndugu kwenye biashara....hili nalo
ni kero kuubwa...ndugu wengi hawana uchungu na biashara
wanajifayia tu..mwisho wanakufukuzia wateja

3.Kuzoeana sana na wateja hadi wanakuwa marafiki
wanakuonea aibu kukukosoa kama huduma au service sio nzuri
wanakukimbia kimya kimya

4.kujiwekea bei unayotaka bila kuangalia soko...
hili nalo linakwamisha biashara nyiingi....

5. kuwatazama watu kwa macho na kudhani wengine sio wateja...
mteja yeyote yule akija kwenye biashara yako mpe thamani yake
usije mtazama mtu ukadhani tu ni 'mpita njia'...utakimbiza wateja...

na zingine ntaongezea baadae
 
Ya pili umekosea huwa ni usemi ttu ambao upo,lakini ukitumia ndugu ni bora zaidi,jarbu kuangalia biashara za wahindi,waarabu na baadhi ya makabila hapa bongo kama wakinga,wachaga na n.k
 
Ya pili umekosea huwa ni usemi ttu ambao upo,lakini ukitumia ndugu ni bora zaidi,jarbu kuangalia biashara za wahindi,waarabu na baadhi ya makabila hapa bongo kama wakinga,wachaga na n.k
Nafikiri mkuu kosa kubwa la ndugu kwenye biashara yako ni kumtumia bila malipo, au kwa malipo madogo.

Hata kama umeajiri ndugu mpe stahiki zake kama mwajiriwa yeyote yule.

Wenzetu wachaga huwa wana makubaliano maalum, kwamba hili duka likifikia hapa au pale halafu lichukue.

Wenzetu wahindi hawafanyi bure, wanalipana vizuri sana na uaminifu ni suala la kwanza.
 
Umenena The Boss. Hasa hapo kwenye nyodo kwenye bihashara. Kuna watu wakianzisha kimradi tu wanajiona wametajirika au ndo wamefanikiwa. Unaenda mfàno dukani mtu kakuangalia tu. Hata karibu hamna. Kibaya zaidi amezungukwa na wengine watoa huduma kama yake na wengine mitaji ishakua kweli. Asante kwa uzi.
 
Hizi nyodo zinaua mno biashara
mtu mmeshindwana bei...baadae unaamua kununua kwa bei yake
anaamua tu hapokei simu yako
anafikiri bado unabembeleza bei....
mwisho unaamua kununua kwingine
 
Back
Top Bottom