Hizi taa za Jokate Mwegelo mbona bei ghali hivyo jamani au zina link na satelites?

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,675
2,000
Mjuu unajua bei ya nguzo moja ya chuma ya hizo taa? Hii sio taa wanayoenda kufunga kwenye socket nyumbani. Na si kila kitu ulichoona Alibaba bei rahisi kina ubora wa kununuliwa au ndio bei elekezi. Waacheni watu wafanye kazi.
Tender imeshatangazwa ?
 

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
15,578
2,000
Umepiga gharama ya mkandarasi ? Procurement n.k au unadhani hiyo hela ni taa peke yake?
Kwanza eneo lazima ifanyike survey, uandaliwe mchoro, baada ya hapo tender itangazwe au wafanye selective tendering, baada ya kupata mkandarasi kazi inaanza...
Kumbuka kuna kuchimba shimo ili uweke base ya kubeba hizo poles (nguzo) nazo ni gharama pia, Usisahau hiyo base inakua na reinforcement kuipa uimara,

Ongeza hili katika akili yako ni kwamba watu wanaweza kuandaa michoro lakini specification za material siyo locally yaan inabidi uagize nje, piga gharama ya shipping, clearing & forwarding...
Project documents/tender documents/biding documents zimetoka, zinapatikana wapi ?
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,486
2,000
Kwa mji kama Dar wenye sun peak hours kubwa nashauri tutumie taa za Solar maeneo mbalimbali kwanza tuta save bills kubwa ambazo hulipwa Na manispaa pia tutatunza mazingira
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,523
2,000
Nazani zitakuwa zile taa zenye Sola ukichanganya na gharama za ufundi na vifaa vingine
Hapana asee,zile taa,haziwezi kuzidi laki 5,pamoja na ufundi,
Taa zenyewe watt 200,haizidi 250,000,
Tena wakiagiza china bei inakuwa chini zaidi
 

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Jun 12, 2021
639
1,000
Hakuna taa ya milioni 3,,dunia nzima
inasikitisha sana na mitaa mingi iko na giza tu , acha watu wateteteee ulaji na naona upigaji umekolea moto kwa sasa hii ni blue print wilaya zote watafanya hivi tena nawashauri waweke taa za milioni 7 kwa taa moja ili isonekane serikali inapenda vitu vya kimaskini
 

Freelancer

JF-Expert Member
Sep 22, 2008
2,957
2,000
Hivi Taa kaweka Jokate au wameweka TARURA baada ya kumbwa na Jokate? Suala la gharama linawahusu zaidi TARURA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom