Hizi smartphone zimeleta kizungumkuti, ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo

Black BackUp

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Messages
387
Points
250

Black BackUp

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2019
387 250
Habari wana JF, Niende straight to the point.

Unakuta mgeni amekuja kukutembelea nyumbani kwako/kwenu wote mnakuwa bize na simu kwenye mtandao kati yenu panakuwa hakuna stori zaidi ya salamu na kuitikiana tu ehee.

Mwingine anajibu hata kisichoulizwa/ambiwa,dereva naye anachati mpaka anasimama katikati ya zebra ama foleni inaenda hana habari.

Kilichonikumbusha niandike uzi yaani kwenye daladala jana mdada amemdondosha mtoto chini ya siti baada ya kukonsetreti kwenye simu mpaka akasahau kwamba kashika mtoto.

Jamani inabidi tubadilike, simu hizi (smartphone) ndiyo chanzo sana cha matatizo.
 

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Messages
15,504
Points
2,000

Castr

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2014
15,504 2,000
Zamani ilikua unaenda eneo la kusubiri huduma mfano benki unakuta magazeti au kama si magazeti unakuta wateja wenzako mtapiga stori za hapa na pale mpaka mnahudumiwa na kuondoka.

Magazeti na wateja wenzako wamekua replaced na smartphones. Ni mbaya ila ndiyo ukweli. Hii imepelekea kuharibu namna ya kuwasiliana, kusocialize na hata kushughulika na maswala madogo madogo yanayoweza kutatuliwa na maongezi.

Huwezi ikimbia teknolojia. Kaza mwendo.
 

Forum statistics

Threads 1,380,810
Members 525,890
Posts 33,780,656
Top