Hizi sikukuu kama 7.7 na 8.8 etc. ni miradi ya watu ama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi sikukuu kama 7.7 na 8.8 etc. ni miradi ya watu ama?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PSYCHOLOGY, Jul 1, 2011.

 1. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari JF!
  Naomba kuambiwa hizi sikukuu May Day na 7 7 mara 8 8 zinahusu nini katika jamii ya waTz?
  Zinatunufaisha wengi au ni wachache?
  Halafu maana ya hii sikukuu ya saba saba ni sikukuu ya nini? Maana naona humu viwanja vya maonesho ni biashara tu na matangazo ya biashara...tena hawana huruma kuingia humu lazima ulipie!
  Yaani ni taabu tupu hakuna utapolalamika ukasikilizwa!
  Opppps!
  Nawakilisha.
   
 2. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Asante kwa hii mada. nimekuwa nikiguswa na utitiri wa siku ziitwazo 'kuu' ktk nchi yetu nakujiuliza maana yazo. 7 7 na 8 8 ni mojawapo. wanadai 8 8 ni ya wakulima na haina historia ndefu sana. 7 7 nakumbuka ilikuwa maadhimisho ya kuzaliwa kwa TANU 1954. iligeuzwa kuwa siku ya maonesho ya biashara ya kimataifa nadhani kiusanii tu ila dhumuni kuu likiwa ni kushikilia siku ya TANU. Haina faid yoyote kwa nchi hii hii sikukuu.

  tuna sikukuu nyingine ambazo binafsi sioni faida yake. tunaadhimisha pasaka kuanzia Ijumaa Kuu na Jumapili ambayo ndiyo pasaka yenyewe. Jumatatu ya Pasaka kwa nini iwe sikukuu? inahusu nini? Tunayo x-mas. kesho yake tunakuwa na boxing day, ya nini? baada ya kufunga mwezi mzima wa ramadhan tunafuatiwa na Idd el fitr. kesho yake tuna idd pili, ambayo nayo tunapumzika. wengine wanakuwa wameanza tena kufunga sita siku hii. lkn sisi bado tunaadhimisha idd el fitr, tunahitaji kweli?

  halafu to make matters worse, tulikuwa na sept 1 kama siku ya mashujaa. wenzetu waliotukuka na hata kutoa maisha yao kwa ajili ya nchi hii. tulikuwa tunapumzika kuwaenzi mashujaa wetu. lkn siku hii ilitolewa kwenye mapumziko na kurudishwa nadhani july/aug 25 ambako wala hakuna mtu aijue zaidi ya wahusika ambao huishia kuweka ngao na mishale pale mnazi mmoja basi. sioni mantiki ya kupumzika 7 7, may day, 8 8, easter monday, boxing day, iddi pili nk na kuisahau siku ya mashujaa wetu. Napendekeza sikukuu zifuatazo zifutwe kwa faid yetu wenyewe. Easter Monday, Boxing Day, Idd Pili, 7 7, 8 8. Napendekeza tuirudishe kama sikukuu siku ya mashujaa. nawasilisha
   
 3. m

  matambo JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwani mwaka mpya unatusaidia nini? as apsychology u need a psychologist to help you
   
 4. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenijaza faida.Umekwenda mbele zaidi.Nilitaka fahamu na hivyo viingilio ni msaada kwetu sisi wananchi tena wazalendo tunaoingia maeneo hayo.Maana hizi sikukuu huwa sioni msaada wowote ila ni faida kwa wachache.Hizo X mass na Eid hizo hakuna viingilio...Yaan hua najiuliza sisi waTz ni mitaji ya wenzetu waTz?Bora tuambiane japo tujifahamu...nmeshachoka na hili nji!Japo sina pakukimbilia.
   
 5. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kumbukeni utawala wa mzee Mwinyi sikukuu ikiangukia jumamosi basi jumapili na jumatatu lazima Watanzania tupunzike halafu tuingie kazini jumanne, sasa kweli unategemea maisha bora kwa kila mtanzania yapo kweli?
   
 6. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakin wakati wa mzee wa Ruksa! Watu wengi walienjoy tafauti na awamu ya 3 na ....
  Hizi sikukuu zina tunufaishaje waTz? Maana pale viwanja vya jk Nyerere kiingilio kikubwa ...wanaoonesha biashara zao wanalipia...yaan kila kitu ni pesa je zinatusaidia nini wananchi? Au ni miradi ya watu vigogo?
   
 7. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Yaani tunapumzika sana licha ya umasikini tulionao. Tunasherekea mpaka inatia kinyaa, tunalewa pombe mpaka inakuwa aibu. Kimsingi hatuko serious unapogusa mambo ya msingi. Puuuuuuuuuuuuh!
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Nibora ununue uswahilini kuliko sabasaba vitu bei mbaya
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Zinawasaidia wafanyakazi wa serikali.ndo muda wa kupata alawansi za bwerere....
   
 10. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Vitu vingine uswahilini havipatikani.Jamaa yangu wa karibu ati yeye huenda kuangalia Nyani. Kumbuka huwezi ingia humo lazima utalipia kiingilio.
   
Loading...