Hizi Sifa za TBC kwa Kijazi zimepitiliza

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,159
9,359
Jana kwa nasibu nilibahatika kuangalia taaarifa ya habari ya TBC! Bila Shaka taariffa hiyo ilimpa nafassi kubwa Sana Marehemu,kuanzia historia Hadi utumishi ambao wao waliuita uliotukuka!

Ila Cha kusikitisha ni kuwa badala ya kumjadili Kijazi ,walikuwa wanamjadili JPM!
Kimsingi waandaji wa habari zile ambazo zilitumia takribaini dk 20+ hawakuwa na weledi au waliweka weledi chini !

Mfano walitumia kigezo cha Barbara za Jiji la Dodoma kuelezea uchapakazi wa Marehemu!

Katika hotuba yake Rais alisema kuwa alipokuwa Naibu Waziri ujenzi miaka ya 1996+ Kijazi alikuwa Mhandisi wa Barabbara Dodoma,na kwa mujibu wa Rais alifanya vizuri Sana!Kilichopelekea apelekwe Wizarani!

Bila kutafakari TBC wakakimbilia Dodoma kwenda kutuonesha Barbara za lami na kuwahoji wananchi kuhusu mafanikio hayo...!😂😂

Barabara zilizooneshwa na wananchi kuhojiwa ni Barbara ya Dodoma Babati kupitia Kondoa,Barabara zakatikati ya jiji pale kwenye shopping centers na Nkuhungu !
Inashangaza kidogo hizi bàrabara nyingi zimejengwa miaka ya 2005 na si kipindi Kijazi alikuwa Mhandisi Dodoma ...ni muhimu kujifunza kusifu!

Sifa nyingine aliyopewa Marehemu ni Unyenyekevu!

Kwenye utumishi wa Umma kuwa mnyenyekevu no tungo Tata!
Kama mtu anafuata na kusimamia maadili ya Utumishi hahitaji kuwa mnyenyekevubali inakuja automatic'

Wala haihiitaji kusifiwa!

Pili,alikuwa mnyenyekevu kwa Nani 😂😂😂kuna baadhi ya Watawala ...ukiwa mnyenyekevu kwao Ina maaanisha kuwa wewe ni Benderaa fuata upepo!

Kuna nyadhifa za Urasimu Serikalini ukiwa àmbiwa mwenye nacho ni mnyenyekevu ...ni lazima ujiulize Mara mbilimbili!

Mwalimu Nyerere aliwateua kwenye uongozi watu wengi Sana ambao hawakuwa wanyenyekevu kwake ....miaka hii nani anaweza!

Tuwasifu watu kwa sifa zao bila kutia chumvi!
 
TBC ni state propaganda machine,hakuna kitu pale,
Wanatumia pesa yetu bure,hawana tofauti na kituo Cha russia today,RT kwa Urusi,Putin anakitumia kwa propaganda dhidi ya magharibi
 
Hivi wanaweza kuendesha mijadala serious na wataalamu kutoka nyanja mbalimbali? haishangazi hawajawahi kuitisha mjadala na mtaalamu kupata ufafanuzi kuhusu covid 21, utafikiri wameajiriwa kwa ajili ya kumpamba mkuu wa malaika....
 
TBC halali ni ile aliyo ianzisha Tido Mhando 2009/2010! Hakika ilitambulika kwa kauli mbiu yake ya Ukweli na Uhakika!! Ilikuwa ni ngumu sana ipite siku usiangalie! Na nina imani ule moto ungeendelea vile vile, basi leo tungekuwa na Shirika la Habari la Taifa, Huru na lenye nguvu sana.

Ila ndiyo hivyo tena! Tangu JK amfanyie figisu Tido, baada tu ya kuruhusu midahalo huru ya uchaguzi na hivyo ccm kupoteza viti vingi vya ubunge, akaja kumuweka yule mtumishi 'mnyenyekevu na msikivu' Clement Mshana, na huyu Dr/Prof Ayub Rioba, hiyo TBC imegeuka ghafla na kuwa TBCCM!

Kwa sasa ni kituo cha habari cha kusifia na kueneza propaganda za serikali ya ccm. Nothing more!
 
Halafu kwenye wasifu wake tumeambiwa na TBC kwamba marehemu alisomea SHAHADA YA UHANDISI WA UMMA hapo Mlimani UDSM. Yaani CIVIL ENGINEERING kwa Kiswahili ni Uhandisi wa Umma..? Mambo gani haya. Shame!!
 
TBC imekuwa hovyo sana. Bila shaka wafanyakazi wa huko, kuanzia mkurugenzi wao, ni watu hovyo. Wanaishi kwa unafiki na kujipendekeza kiasi cha kuonekana ni wajinga wa kudumu.
In Tanzania PATRIOTISM is synonymous to STUPIDITY! " UKIWA MPUMBAVU TANZANIA WEWE NDIO MZALENDO"
 
simjui. ila kwa kweli bwana Kijazi alikua anaoneka ni mtu mstaarabu sana.
 
Back
Top Bottom