Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Tugas

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
243
500
Ni marufuku kumfanyia mtoto wako homework, sasa hapo mwalimu atampimaje kama alielewa au hakuelewa.
Wajibu wako km mzazi ni kuhakikisha mwano anapata muda wa kufanya home work na amalize, hata ukimuona ameandika masifuri sifuri mwache akachezee fimbo au azomewe na wenzake ndio atapata akili.

Nafikiri kwa maelezo ya watu wote! Wewe mkuu ndiye unaye elewa maana ya home work! Me wa kwangu huwa namuona anaenda chaka kabisa naishia tu kumuangalia! Home work hapewi mwanafunzi ili asaidiwe na mzazi! Bali jukumu la mzazi ni kuhakikisha amafanya home work zote hata akiandika majibu yasiyo sahihi hutakiwi kumuelekeza!
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,022
2,000
Umenena! Mtoto kaniuliza "you doesn't understand " ni kiingereza ? Nikamwambia mwalimu agesema"you don't understand " nikashangaa !!!
 

Angellight

Member
Apr 30, 2021
11
75
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Aiseee you was in my head....ahsante kwa hii thread ...sijui nisemaje yaani...nasubiri tu kikao Cha wazazi niongee
 

Angellight

Member
Apr 30, 2021
11
75
Aisee hii ni shida mwanangu maswali ya darasa la pili uafikir form3 du watamuua mwanangu, kweli mtoto wa std 2 una muuliza swali la mention four symptoms of tuberculosis kweli, mpaka nikampigia rafiki yanyu doctor mana mimi nilikua najua 2 tu. Sasa sijui nasoma mimi au mwanangu
Acha tu

Eti HIV/AIDS
TB
CHOLERA

Darasa la pili


Akija na homework nagoogle hahahahaa
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,984
2,000
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Umenigusa vilivyo.
Nina Kipenzi wangu Grade 1 Binti, yaani napata taabu kweli.
Tena Bahati Mbaya Nyumbani napatikana Weekend tu!
Huu Ujinga Muusome English Medium School mnao saana Ujinga huu.
 

Angellight

Member
Apr 30, 2021
11
75
Katika experience ya jf hakuna uzi umenichekesha kama huu!! Nadhan because it's involve my career, I have 3 years experience in this industry lkn sijawah kukutana na malalamiko ya wazaz khs homework, basically huwa nahakikisha maswali yanatoka within their reach,,, Nita akikisha maswali yote yamefanywa though I don't mind kama amekosa maana hata wrong answer pia ni jibu kikubwa tu mtoto asumbue akili yake kutafuta solution ya jambo at the end of the day itamsaidia Mwanafunz mwenyew,,, kikubwa tu zisiwe too much to extent it become hectic,,, ila ukitaka kujua wazaz wako serious na elimu hebu usitoe homework hamna rangi utaacha kuona kumbe in other side wazaz wako bored namna hii!!!!
Tunapenda wawe na homework lkn iwe kitu walichofundishwa darasani ...Sasa unakuta mtoto hajafundishwa .Matokeo yake tunalipa ada na kufanya kazi yenu ya ualimu...inaboa mno..saa ngapi tutafute hela na saa ngapi tufanye homework...wapeni watoto homework baada ya kuwafundisha...sio kila mtu ana kipaji Cha kufundisha....Mimi ni mkali natamani nifundishe aelewe...nyinyi mna skills na mmesomea
 

zeck john

Member
Aug 16, 2017
9
45

Mtoto wangu Homework ya Kiswahili alikosa methali na nahau, mtoto akaulizwa nani kakusaidia akajibu baba... Mwalimu akamwambia babaako na wewe wote akili hamna....

Taarifa ikanifikia, nikaona isiwe tabu, kwakuwa ni class VII nimemhamisha mkoa yupo boarding na homework hainihusu tena.

 

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,439
2,000
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo. Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
.acha mkuu,sikuhizi tofauti za zamani,ukiwa na kijana mwanafunzi,lazma na ww uwe dent tu,huwez kwepa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom