GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Wakati akizungumzia mipango ya Radio yao ya Efm mmoja wa Mabosi wa juu kabisa wa Efm Radio Denis Ssebo amesikika akisifia mambo kadha wa kadha ambayo Efm imeweza kufanikisha hadi sasa kuwa moja ya Radio bora na tishio hapa mjini lakini kuna kauli ambazo zinautata kidogo ambazo ni za kimafumbo zaidi amezitoa.
Nitazinukuu hizo kauli hapa chini.....
" Efm tumeweza ku set trend katika vipindi vingi hapa nchini Tanzania hadi wengine sasa wanakesha kutuiga badala ya kujifunza kutoka kwetu ".
" Efm tulianzisha Mwanamke wa Shoka na wao tunasikia juzi juzi tu wamekuja na kitu kile kile ila wamebadili jina tu hii kwetu inatufanya tuzidi kujiona ni washindi ".
" Efm tulianzisha kutangaza nje ili kuweza kuwafikia kabisa mtindo ambao tunauita nje ndani mara ghafla tukawaona na wenzetu nao Wazee wa kuiga na kukurupuka nao sasa wakiendesha baadhi ya Vipindi vya nje kama sisi ".
" Kuna Watu kwa kutuogopa sasa imewabidi hadi wabadili hata Vipindi vyao ili tu waweze kutukamata lakini wakasahau kuwa sisi Team yetu imejaa ubunifu wa ajabu sana na sasa kwakuwa ndiyo tumepewa Vibali vya kutanuka Mikoa tisa ( 9 ) nadhani watajuta kutufahamu Efm "
Najua kuwa humu JF ni nyumba ya Watu makini, werevu na wenye utambuzi wa kutukuka sana hivyo bila shaka mtaweza kunisaidia Mimi ' Popoma ' au Ngumbaru ' kujua kuwa hizo Kauli nilizozinukuu hapo juu alikuwa anamsema au anazielekeza kwa nani au akina nani hasa?
Nitawashukuru na naomba kuwasilisha.