Hizi sasa sifa; Baada ya kolabo na Rick Rosey, Diamond kuja na kolabo na Omarion

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
Kwema wana,

Yule mwanamziki pekee wa kimataifa panapo ardhi ya Nyerere, Diamond Platnumz yupo jikoni akiaanda ngoma nyingine na mkali kunako ardhi ya Trump, USA Baby.

Mtakumbuka kama wiki mbili zilizopita Mond alikuwa akipika hit song na Rick Rosey mwenye midevu yake.

Wale ambao hatujafikisha miaka 30 tutakuwa tunamjua vyema mnyama Omarion (ndiye alikuwa role model wetu) aliyekuwa kundi la B2K chini ya Rapa tajiri duniani P.Didy lakini sio wa JF asiyejua kuandika.

Wakati Diamond akiipeleka Bongo fleva duniani kuna kajamaa kenyewe kanashinda kijiweni kuvuta shisha na kula mirungi huku kakisubiri mwisho wa wiki kakagombee mic na Mwamba Geu , S Kide mtoto wa mama Shamte fiestani.


Omarion.png

 
Hapa ndipo Diamond anaponiacha hoi, yaani anafanya kolabo na mtu wa nje cha maana wanachokifanya hao watu ni kutaja neon moja tu kama vile 'oooo' 'uuuu' 'waaaa' 'haaaa', 'you know what', 'Hey Yo', wabongo wanaona ujiko, this is beyond stupidity? Unamlipa mtu so much money kuuza sura tu?
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom