Hizi ni zama mpya, tukikosa ubunifu tutaua upinzani kwa mikono yetu wenyewe

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Naamu wanabodi!

Leo nimeona nilete jambo tubadilishane mawazo ili huko tuendako tusije kuanza kumtafuta mchawi ni nani.Kuna kila ushahidi kwamba zama mpya imeanza kwani utawala wa kisiasa Nchini umekuja tofauti na ule wa awamu ya pili,tatu, na awamu ya nne.kuna viongozi wananchi wamewakubali kwa dhati kwa namna wanavyo tenda kazi zao.Kwa muda mfupi walio kaa madarakani nimegundua kuwa wananchi walio wengi wanataka viongozi wanao fanyakazi na siyo wanatokea chama gani, mkoa gani, kabila gani n.k.

Ni kweli kwamba kwa mara ya kwanza upinzani wamepata wabunge na madiwani wengi kuliko wakati mwingine wowote tangu vyama vingi vilipo anza upya mwaka 1992.hili ni jambo jema.Halmashauri nyingi zipo chini ya wapinzani. Je, tumemaliza kusherehekea ushindi tulio upata? wajibu wa tulio wachagua ni kuhakikisha Halmashauri hizi zina akisi matarajio ya wananchi, wananchi wanataka maendeleo! Tukikaa kumbeza Magufuli wakati wananchi wamemkubali haitusaidii. wapinzani tunatakiwa kufanya mambo mengi zaidi yake katika Halmashauri zetu ili kila mtu aone tofauti ya kiutendaji kati yetu na ccm.

Mheshimiwa Nassari ni mfano wa kiongozi mbunifu. haishi Dar kama viongozi wengi wanavyo fanya. anakaa na wananchi na kushirikiana nao.amesha nunua gari la wagonjwa na vitanda kwaajili ya hospitali katika jimbo lake!Halmashauri yake inasimamiwa ipasavyo na hayo ndio mambo ambayo wananchi wanayataka.

Ni wakati muafaka upinzani waweke mikakati thabiti ya namna kuendana na zama mpya. Magufuli ni mjanja tena mwerevu kweli tusipo angalia anaweza ku win nyoyo za wapiga kura wengi mpaka tukakosa pakuanzia.
 
siku zote iko hv, SERIKALI ikiwa dhaifu UPINZANI huwa imara, na kinyume chake ni SERIKAL IMARA upinzani DHAIFU, tatzo wapnzani wa tz hawapo kwa ajiri ya kuisimamia serikali, bali wanachotaka ni kuingia ikulu tu na kuongoza nchi bila kujal kwa kutumia wa2 gani, hata kwa kutumia MAFISADI wao hawajal ki2. but kwa maguful watabadilika 2
 
Mbona mnapata shida sana, acheni upinzani "Ufe" ili nchi iondokane na vyama vya "udini na ukanda". Alimselema! Halija!!
 
Kati ya watu waliotoa funzo nzito TZ na akaeleweka na watanzania ndani ya upinzani na kuwavuta watanzania maskini ni Dr.W.P.Slaa.
Ni moja kati ya viongozi waojipambanua kwa maneno na matendo kwa kuwa na uthubutu wa kusema na kuchukua hatua mara moja,alikuwa alama uadilifu,utetezi kwa wanyonge,uongozi uliotukuka toka kipindi akiwa makamu mwenyekiti chadema taifa.
Kwa kupima upepo ccm ni wajanja sana walilazimika kutua mzigo na kubeba asante ya watanzania wakampitisha Dr.slaa wa upande wa pili ambaye kwa namna moja au nyingine wanashabihiana kuwa Rais ili kutekeleza azma na hitaji la watanzania.
Kilichobaki sasa ni sisi kumpa support kubwa ili tufanikishe malengo yetu kabla ya muda wake kwisha maana muda ni mali ukipewa fursa itumie.
Upinzani wa sasa sina hakika kama ni wapinzani wa ukweli kwa nature walioko ndani ya vyama vyao hasa kilichokuwa chama kikuu kabla ya kuungana na vyama vingine kutafuta ushirika ambao nahisi wote wametumbukia kwenye shimo moja.
TUNAHITAJI UPINZANI MPYA TANZANIA, HUU WA SASA UFE TU MAANA TUKIWATAZAMA USONI NA MATENDO YAO YA HUKO NYUMA NA SASA HAKUNA MATUMAINI.NAHISI HAKUNA WA KUMKOSOA DR.JPM KWA MAANA KUWA HAKUNA MWENYE MORAL AUTHORITY.
TUNAMHITAJI DR.SLAA MWINGINE TANZANIA NA SIYO WAPIGA DILI.
RAIS ULICHOKISAHAU KWENYE DHAMIRA YAKE NI SUALA LA KUSHUSHA BEI YA VIFAA VYA UJENZI LIFANYIE KAZI.
 
Huyo padri wzako yuko wapi? What happened and why did he leave? Unajua kama imani ilihusika? And who financed his departure ? And who is financing him right now?
 
Hamna mtu kati ya hawo .....maramia ungemleta hashim rungwe
Huyu SIJARIBIW wakati akiwa Mkemia wa NCU si ndo alikuwa akiuza mbegu za pamba? leo hii uadirifu wake umetoka wapi?
Huyu huyu sijaribiwi aliwahi kumdhulumu mwananchi mmoja kiwanja chake pale mwanza miaka ya 1999-2000? Leo ametoa wapi uadirifu? SIJARIBIWI ni mnafiki tu.
 
jamii forum vipi mbona mada tofauti hapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????
 
Back
Top Bottom