Hizi ni Series ambazo zimenishinda kabisa

Series niliyoiangaliaga ni Into the bad land na prison break Na Naagin ya kihindi tu..Series siangaliagi kabisa Mimi..Mimi n mpenzi wa movie tu,Na movie zangu ni za Ma niggas,Comedy na Drama basi.
1:Fatherhood
2:Coffee and Kareem
3:Uncle Drew
4:Barbershop
5:Friday
6:Titanic
7:Tom and Jerry 2021
8:Girls trip
9:Night school
10:What men want etc.
 
Katika kila series utakuta kuna mambi flani ya kitoto ila nyengine zimezidi
 
Wahindi kuweni seriuos mmefikia hatua sasa mmeanza kutudharau.

Sawa tunajua ni maigizo na sio lazima yaendane na uhalisia, lakini ndo umchome mwenzio na ndizi mpaka damu zitoke hadi kufa?

Hizo risasi zinavyokwepwa sasa aaah!

View attachment 1795701
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Hii Kali aisee uongo uliotiwa chumvi
 
Mitizamo inatofautiana wapo wanaozipenda hata watu wazima. Zamani alikuwepo mwimbaji mmoja anaimba nyimbo za kitoto za kipuuzi. Mr. Nice. Walikuwepo mashabiki wake wengi na aliuza sana.but mimi ilikuwa siwezi sikikiz nyimbo zake hata unipe na pesa.
Sijui alikuwa anaimba vitu gani mpaka akapendwa kiasi kile!!
 
Niliangalia series ya Supergirl episode kama 3 tu nikaona ni utopolo tu.

kuna dude linaitwa raised by wolves hii ngoma kuna sehemu waliniacha njiani sikulielewa kabisa labda s2 ikaeleweka.

Warrior nun hii iliisha kipumbavu ata sikuelewa
 
Korea na Spain series zao zinakuwa zikiongozwa na makampuni mkubwa kama Netflix lkn wakiongoza wenyewe zinakuwa mbovu sana
 
Nmejaribu sana kuangalia baadhi ya series za mataifa mengine nmejikuta nashindwa kabisa hasa za:

1. Spain
2. Mexico
3. Philippines
4. Turkey
5. Korea
6. China

Hawa jamaa bado wana series za kitoto kitoto sana. Uhalisia unapotea kabisa. Ukichanganya na lugha ndo nakwazika kabisa kukaa niangalie motions na pia subs. Huwa nachoka.

Mexico na Spain huwa wana storie nzuri ila zinawashinda kuigiza. Kama Money Heist ilipasWa iiishie season 2 hasa hasa. Wakaivuta kipuuzi iwe ndefu na hali bado haikuwa that much serious. Idea ile wangepata watu wenye akili na serious wangetoa kitu kikali.

Nmejikuta nafurahia series kama
1. Breaking Bad
2. Better Call Saul
3. Ozark
4. Gangs of London
5. Rome
6. Carnivale

Etc. Pia nikiwa nmeangalia nyingi za wa Norway, Belgium, Canada. Hawa wanajitahidi. Ukiacha za USA na UK. Ambako pia huwa nikikuta zenye utoto utoto mwingi naachana nazo.

The 100 ilikuwa nzuri mwanzoni mpaka walipokuja iharibu seasons za hivi karibuni hasa season 7.


Binafsi sipendi niangalie Series uongo uwe wazi mpaka nianze kuona kuwa mtengenezaji aliniona mimi mtizamaji fala sana. Ni kunikosea heshima. Uongo unafaa kufanana na ukweli kabisa katika movies.

Ukitaka nisikae home kwako.rahisi sana.niwekee series/movie ya Nigeria,Ghana, Tanzania, South Africa,kihindi etc. Hizi huwa na upumbavu flani hivi wa kudhani watizamaji wote ni watoto wadogo.
Povu mujarabu kabisa 🤣🤣🤣
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom