Hizi ni sehemu ya sababu za CCM kuendelea kukataliwa na Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ni sehemu ya sababu za CCM kuendelea kukataliwa na Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkenazi, Apr 21, 2011.

 1. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sioni jambo jipya linaloweza kufanikishwa na CCM ikiwa mambo waliyopanga wenyewe yamewashida kama nilivyoweza kukumbuka machache hapa chini:

  1. Chama cha Mapinduzi kilishindwa kutekeleza programu yake ya miaka 15 (1987 2002). Pamoja na mambo mengine kulikuwa na kipengele kinasema "IFIKAPO 2002 kila wilaya itakuwa na matrekta 25" Mpaka leo hakuna kitu kama hicho badala yake miaka 24 baadae bado mnaongelea kununua Power tiller tena kwa UFISADI
  2. Chama cha mapinduzi kilianzisha mradi wake wa SUKITA pale bonde la Tabata kikashindwa, SUWATA kikashindwa ; leo CCM wanazunguka wanatuimbia wimbo wa EL, RA na AC yaani wanatafuta huruma za wananchi wa Tanzania kupitia mazao ya mfumo wao. Tumekwisha wagundua.
  3. Nchi nzuri Tanzania kwa sababu ya utawala wa CCM haina hata shirika la ndege lenye ndege za uhakika. Tunazidiwa na Rwanda. Hawa wawekezaji waliojaa nchini wangekuwa wanapanda ndege zetu shirika lingekuwa kubwa sana.
  4. UMEME – Eti mpaka leo hatuna umeme wa kutoshereza mjini. Mawazo ya CCM ni kukodisha tu hii ni milango ya UFISADI. Iko wapi mipango ya MCHCHUMA, KIWIRA na LIGANGA coal projects ? toka miaka hiyo mpo tu halafu mnasema mnataka ridhaa ya wanachi muendelee kuwatesa.
  5. VIWANDA, enzi hizo za Mwalimu Tanga, Morogoro, Dar Arusha n.k kulijaa viwanda vya kila namna na kutoa ajira leo viko wapi ? bado mnataka muendelee kutawala – Nasema imeishatosha pumzikeni muone wenye akili watakavyofanya kazi.
  6. CCM ni nini hasa ilichokianzisha kikafika mwisho kwa mafanikio ? Ilianzisha RUBADA – Rufiji Basin Development Authority miaka ya 1975 – Hilo bonde limeendelezwa ? ikaja KOTACO – Korea Tanzania Agricultural Company kwenye mabonde ya chitah je mlifanikiwa ?, haya kuna kilmo cha kufa na kupona miaka ya 1974, kilimo ni uti wa mgongo, Kilimo kwanza, MKUKUTA, Mkurabita n.k.
  7. Oh CCM – mmewadhoofisha wana wa Tanzania kwa kuwajengea mawazo hasi kwa kila eneo mf. Kauli ya viongozi wote wa CCM ni kusema tanzania ni masikini – hii ni mbaya sana. Nchi isiyotaka kutumia wataalamu wake Waandisi, wakandarasi n.k hii yote ni sababu ya UFISADI. – CCM inachojua ni kuchakachua tu hata taarifa za utafiti inachakachua ili ionekane imefanya vizuri.
  8. ELIMU – Shule za Yebo yebo – hakuna maabara halafu mnasisitiza masomo ya sayansi au kwa kuwa viongozi wengi na watoto wenu mnasomea siasa ?. Hakuna mkakati wa Kitaifa wa kuifanya sayansi ijenge uchumi wa nchi. Ikiwa mhandisi wa kitanzania ndiye supervisor kwenye makampuni ya wakoloni tutegemee nini ? - UFISADI kila sehemu.
  9. CCM, CCM, CCM pamoja na wabunge wako kitendo cha kuipenda ccm ya watu milioni tano kuliko watu milioni 40 wasiokuwa CCM na ambao ni wapiga kura wenu mnatenda kosa kubwa sana na ndio maana hamtapewa ridhaa tena ya kuongoza nchi hii. Wabunge wa CCM wanashangilia kil akitu hata kama ndani yake kina ajenda ya kuwachinja ndugu zao. Wabunge wa CCM walishangilia mswada wa uundaji wa tume ya Katiba mpya ulioondolewa bungeni, lakini pia wangeupitisaha serikali ingelazimisha uende bungeni. Huu ni wendawazimu ambao ni magamba kuliko hata haya y aya juzi kwani matokeo ya katiba dhaifu ni ufisadi uliokithiri.
  10. CCM kimekuwa ni chama cha kijeshi kama ifutavyo
  • Rais – ni mwnajeshi
  • Wakuu wa mikoa wengi wanajeshi wasitaafu
  • Wakuu wa wilaya – Wanajeshi
  • Makamba, Kapteni Mkuchika, Nape mtoto wa mwanajeshi, January Makamba – baba yake mwanajeshi, Kinana
  1. SHIME Watanzania tunayo kazi moja tu nayo ni kumwondoa nduli CCM kwani NIA tunayo, Sababu tunazo na uwezo tunao.
  Naomba kuwasilisha na nyie muongeze sababu za kwa nini CCM haiwezi kuendelea kutawala zaidi.
   
 2. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja na hamsini!
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Na baba yako aliyesomeshwa kwa jitihada za CCM akafanya hadi leo na wewe unajua ku CLICK mboja hujaiandika kama shortcoming hapo?
   
 4. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni lini uliona CCM wanasomesha watu? Lini umeona CCM wametangaza scholarships? Acha kudanganya watu kuhusu elimu. Utoaji wa elimu ni moja ya majukumu ya lazima yanayopaswa kutekelezwa na serikali yoyote ile, iwe ya kifalme, kidikteta, au ya ki-CCM. Na kwa kuzingatia hili ndo maana unaona kila mahali duniani serikali zote zinasomesha watu wake pasipokuwauliza itikadi zao wala dini zao. Ulimbukeni wenu huu ndo maana umepelekea kuchukulia suala la elimu kama moja ya mambo ya kutilia msisitizo kwenye ilani ya CCM. Masuala ya maji, chakula, elimu. afya, na ulinzi siyo priorities but they are the must. Utaona serikali yenu ya CCM inasema eti mkituchagua tutawaletea huduma ya maji, afya na elimu, huu ni ujuha kwani CCM imekuwa madarakani kwa kipindi kirefu na haijayatekeleza mambo yote ya lazima huku ikiendelea kukusanya kodi za wananchi hao bila kuwapelekea huduma muhimu. Unafikiri mfumo wa kutoza kodi ulianzishwa kwa misingi ipi? Lengo la kodi ni kuiwezesha serikali kutoa huduma za pamoja ambazo mtu mmoja mmoja hawezi kuwa nazo kwa jitihada zake binafsi. Na kwa kuzingatia kuwa serikali huwa inatoza kodi kwa watu wote iwe washabiki wa CHADEMA, CUF, NCCR- Mageuzi nk, vivyo hivyo inapaswa kutoa huduma za msingi kwa watu wote. Acha mtizamo wa kijima kwani wanaodanganywa kwa sera kama yako ni wale ambao hawakufika darasani sawasawa.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Du!!!
  Hii kali.
   
 6. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  naomba niunge mkono hoja kabla sijaongeza sababu za kuikataa ccm.
   
 7. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  mkubwa swala la elimu na huduma nygine ni haki kwa kila raia wa Tanzania na wala si hisani hatakidogo sasa kupewa haki yetu ya elimu hatulazimiki kumshukuru mtu yeyote,katafute vilaza wenzenu wenye Magamba
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Zinaweza zikawa sababu zinazowafanya wakataliwe na wananchi lakini at the same time ndiyo sababu zinazowafanya waendelee kuwa watawala.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  CCM wanakwenda kinyume na huu msemo maarufu kwa kimombo "when the boat is sinking you should cast the unnecessaries upon the water,but why wait until then?"
   
 10. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nakubaliana na hoja 100%. Shime tuungane pamoja kwani ukombizi wa mtanzania uko mikononi mwetu sote.
   
 11. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ili tupate chama safi kabisa kuongoza Tanzania Chadema iondoe picha hii kwanza TEC na Kanisa Katoliki kwa Ujumla wasijifanye washauri wa karibu wa Chadema na Kadinal Pengo asipende kudandia hoja za Chadema na Kutoa matamko! Pili Wachaga waiachie Chadema sasa kiondokane na sura ya ukabila yani kiondokane na Uchaga na kila mwana chama wake awe na haki sawa na heshima yake isitokane na Uchaga wake,tatu kama kuna deni analo dai Mzee Edwini Mtei kwa Kuanzisha Chadema alipwe ili chama kitoke kwenye Ukampuni Binafsi au Chama cha Ukoo na sasa kiwe Chama chenye sura ya Kitaifa! Na Mwisho Freeman Mbowe awape nafasi wanachama wengine washike nafasi ya kiti cha Mwenyekiti wa Taifa!
   
 12. k

  kakini Senior Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  inaonesha ni namna gani ulivokuwa mbumbumbu maana elimu, maji umeme na barabara ni vitu vya msingi yaani hata mtoto wa darasa la 4 anakushinda wewe zuzu kweli na nakuonea huruma wewe na familia yako
   
 13. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Toa jibu sahihi acha longolongo! Baba yako hajasomeshwa na CCM?
   
 14. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  you can fool some tanzanians sometimes but you can't fool them tanzanians all the times!!
   
 15. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  you can fool some tanzanians sometime but you cant fool them tanzanians all the time!!
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Duh yaani mpaka leo hii kuna watu wana mawazo ya siasa za 1995 (CCM imekusomesha, CCM imewasomesha) hii mbona iliisha julikana kuwa ni propaganda isiyoweza kushawishi hata mgonjwa wa akili?. CCM isomeshe watu ina hela za kutoka wapi?, watanzania wote wanaosoma either kwa mikopo au kipindi kile bure, ilikuwa ni pesa zao hizo, baba zao na mama zao wanalipa kodi za mazao yao kila siku. Na viwanja vya michezo CCM walivyojimilisha wajue kuwa whether wanaviuza au kuendelea kuviita uwanja wa micheza CCM.... navyo vitarudi kwa wananchi pindi wakichukua serikali yao.
   
 17. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii hoja jamaa umeing'ang'ania bure haina mashiko kwenye siasa. Baba yangu mimi hakusomeshwa na CCM, alisoma enzi za ukoloni ambapo CCM haikuwa inafikirika kama itakuja kutokea Tanganyika. Kama una akili japo ya kukuwezesha kujielewa mwenyewe nafikiri unaweza kunielewa hata mimi ninayetumia maneno rahisi kabisa. Kwa kuwa CCM haikuwepo enzi za ukoloni lakini watu walisomeshwa na hao wakoloni, huoni kuwa kazi ya kusomesha siyo sera ya CCM bali ni wajibu wa serikali yoyote inayokusanya kodi za wananchi? Kama jibu lako ni ndiyo, basi elewa kuwa watu husma kupitia kodi zao na siyo CCM. Serikali yoyote itakayoingia madarakani ni lazima isomeshe, siyo suala la mjadala wala propaganda za ki-magamba magamba hapa.
   
 18. S

  Simon B james Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafuta gazeti la mwanahalisi wiki hii tar 20 april to 25 utaona Kikwete anavyo nuka ufisadi. Mambo yote yameanikwa hadharani na mafisadi yote list ya kwanza ili iliyo tolewa mwaka 2007 tar 15 september ipo na majina mapya yapo akiwemo Msekwa na magufuli.
   
 19. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hata cdm ikishinda bado itakusanya kodi watu wasome tofauti iko wapi Kati ya CCM chadema na ukoloni. Tatizo la chadema ni uchaga na sera ya majimbo. Kwa mtaji wenu huo hamtakanyaga Magogoni, mtakuwa mnapaona kupitia linings .
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  We kweli POPOMPO, CCM wametoa wapihiyo hela ya kusomesha watu? KODI ZETU ndio zimetufiukisha hapa POPOMPO.
   
Loading...