Hizi ni sababu za wanaotaka Katiba Mpya Tanzania

machashi

Member
Aug 17, 2019
15
5
Hizi ni sababu za waotaka katiba mpya Tanzania

Utawala bora na utawala wa sheria ni upi? Ni maswali ambayo hujiuliza watu wengi nchini Tanzania na ni moja ya vilio vya baadhi ya Watanzania kwamba kunakiukwa katiba ya nchi.

Mifano ya uvunjifu wa katiba ni suala la wabunge 19 wa Chadema ambao wanalalamikiwa na chama chao kwamba wamejipeleka bungeni bila kufuata katiba ya nchi.

Jambo la kusikitisha ni kwamba wanaofanya ‘madudu’ hayo ni wasomi wenye shahada wengine tatu lakini hawaoni haya tunayoona sisi ambao hatukusomea sheria?

Nimefuatilia suala hili kwa muda mrefu lakini wenye mamlaka hawajatoa tamko rasmi kwamba ni sababu zipi zinafanya wanachama wale 19 wanaendelea kuhudumiwa na fedha za walipa kodi wakati ukweli ni kwamba wamefukuzwa uanachama. Wakanakaa mbungeni kinyume cha katiba ya nchi, hapo ndipo utawala wa sheria unapokiukwa.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimefuatilia kwa karibu msuguano unaondelea kati ya Spika wa Bunge na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) juu wa wabunge hao ambao kwa maoni yangu wamekosa sifa kwa kuvuliwa uanachama.

Mgogoro huu sio tu unasigina demokrasia lakini kwa upande mwingine unavunja katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Misingi ya demokrasia inatawaliwa na dhana ya ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi juu ya mambo ya msingi yanayowahusu katika taifa lao, kwa Tanzania kama ilivyo katika nchi nyingi duniani uwakilishi wa wananchi katika ngazi za maamuzi unafanywa kwa uwakilishi wa watu wachache waliyochaguliwa na wananchi hao yaani indirect democracy.

Kwa mujibu wa ibara 21, 39, 47 na 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa haki ya mtu kuwawakilisha wananchi katika ngazi za maamuzi kwa sharti la kupitia au kudhaminiwa na chama cha siasa. Hivyo, kwa Katiba ya sasa suala la udhamini wa chama cha siasa katika ngazi za maamuzi ni takwa la msingi la kikatiba.

Kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(e), Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge endapo mbunge huyo ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge, wanaoteuliwa ni kama hao wa Chadema wa viti maalum.

Hatua ya Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndungai kuendelea kutambua wabunge waliovuliwa uanachama na Chadema kwa tafsiri ya moja kwa moja ni sawa na kuvunja Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyoainishwa.

Kwa mujibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu; kinatambua umuhimu wa uwakilishi wa wananchi katika ngazi za maamuzi pasipo changamoto za kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977.

Ni wazi kwamba, changamoto za kikatiba zilizojitokeza katika hatua ya Chadema kuwavua uanachama wabunge wake na Spika wa Bunge kuendelea kuwatambua wabunge hao ni uvunjifu wa Ibara ya 71(1)(e).

Katika suala hili, Kituo kinaona haja ya kufanyika mabadiliko ya kikatiba kutambua mgombea binafsi ili kuepuka hatari ya kuvunja Katiba ikizingatiwa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria.

Ikumbukwe kwamba, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilitoa uamuzi wa kuhusu haki ya mgombea binafsi kutambuliwa katika ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.

Katika upande mwingine, katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 kumeshuhudiwa matumizi makubwa ya rasilimali za wananchi kwa kufanya chaguzi za marudio katika majimbo na kata mbalimbali kutokana na wabunge na madiwani kutoka chama kimoja kwenda chama kingine cha siasa. Ni muhimu kurekebisha katiba ya sasa pamoja na sheria ili kuruhusu haki ya wananchi kuwakilishwa pasipo kufanyika marudio ya uchaguzi ikiwa mbunge au diwani atahama chama chake.

Nitowe wito wito wa kurudisha mchakato wa katiba ili kusawazisha changamoto za kikatiba zilizopo sasa na kuepisha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 bara na visiwani.

Historia inabainisha kuwa mchakato wa kuandika Katiba mpya Tanzania ulianza kutokana na madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka Katiba Mpya itakayokidhi matakwa ya nchi ambamo wananchi ndio wenye kushika hatamu. Inaweza kuanzia ilipokwamia na jinsi gani ya kuendelea mbele ili kupata katiba mpya ya Tanzania.

Nimeandika makala haya ili kuamsha mchakato wa Katiba Mpya ili kuukamilisha hadi kupata Katiba Mpya yenye muafaka wa kitaifa na kijamii. Nia ni kuhakikisha Tanzania inapata katiba yenye ubora na itakayokidhi matakwa ya wananchi.

Makala haya nimeandikia nikikusudia pia kutoa elimu, kuhamasisha na kushawishi upatikanaji wa katiba jumuishi yenye viwango vinavyokidhi. Malengo yangu ni kuwapa hamasa wananchi kudai katiba mpya ambayo itakuwa imejumuisha mawazo yao. Pia wafanya maamuzi wanachokozwa na kuhimizwa kuendelea au kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Ni eleze kwa kifupi sana historia ya katiba yetu. Tanzania ni Jamhuri ya Muungano. Ni Muungano wa nchi mbili zilizoungana mnano tarehe 26 Aprili 1964, nchi hizi (Tanganyika na Zanzibar) awali zilikuwa huru na zenye mamlaka kamili. Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zipo katiba mbili, katiba ya pili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hivyo, kwa upande wa Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumewahi kuwa na Katiba zifuatazo, katiba ya Uhuru ya Mwaka 1961, Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962, Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1964 (Katiba ya Muungano), Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1965 na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwa kifupi, uandishi wa katiba zote tajwa hapo juu haukuwa shirikishi. Wananchi hawakupata nafasi ya kutoa maoni yao wakati wa mchakato wa kuandika katiba. Na pia, katiba zote ziliandikwa wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja. Baada ya nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 isingeweza kutumika bila kufanyiwa marekebisho makubwa. Kwa misingi hii, haja ya kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa haiepukiki.

Mchakato wa uandishi na maudhui ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake 14 vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutoshirikisha wananchi kikamilifu. Pamoja na mchakato kutokuwa shirikishi kwa wananchi, suala kwamba uandishi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ulifanyika nchi ikiwa kwenye mfumo wa chama kimoja nalo limekuwa likilalamikiwa na wadau mbalimbali.

Pia, mwaka 2010 Zanzibar ilipofanya marekebisho ya katiba yake ya mwaka 1984 ilipelekea madai ya kudai katiba mpya ya Muungano kuongezeka. Sambamba na hilo, hali ya kisiasa hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nayo ilidhihirisha haja ya kuandika katiba mpya ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi.

Kwa kuzingatia hayo Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba ya kuuaga mwaka 2010 na kukaribisha mwaka 2011 aliridhia kuanza kwa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya. Pamoja na shinikizo la raia kupitia makundi yao mbalimbali hususani asasi za kiraia na vyama vya siasa, uamuzi wa Rais ulichochewa na zoezi la kujitathmini wenyewe tukiwa wanachama wa Mpango wa Kujitathmini Utawala Bora Afrika (APRM) tangu 2010.

Baada ya uwamuzi wa Rais, serikali iliandaa muswada na kuuchapisha katika Gazeti la Serikali mnamo tarehe 15 Machi 2011 na kuwasilishwa Bungeni Aprili 2011 ambapo baadaye ulipitishwa kuwa sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 8 ya mwaka 2011.

Sheria hii iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhiwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011 ilimpa Rais mamlaka ya kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Rais aliteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Mwanasheria nguli, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba ili kupata katiba ya kudumu miaka 50 hadi 100 bila haja ya kufanyiwa marekebisho makubwa.

. Wajumbe walioteuliwa walikuwa 32 (ikijumuisha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wajumbe 16 kutoka Tanzania Bara na 16 kutoka Zanzibar. Muundo wa Tume ulihusisha wawakilishi wa vyama vya siasa, wasomi, AZAKI, madhehebu ya dini na makundi mengine katika jamii.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge Maalum la Katiba (BMK) lilikuwa na wajumbe kutoka makundi matatu. Kundi la kwanza lilikuwa ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kundi la pili lilikuwa ni wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Kundi la tatu lilihusisha uteuzi wa wajumbe 201 watakaoteuliwa na Mhe. Rais wa Muungano kutoka makundi mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania. Bahati mbaya sana bunge hilo halikufaulu kwa sababu za itikadi za kisiasa. Ipo haja ya kutengeneza bunge la katiba jipya litakalotuletea katiba mpya ambayo haitaruhusu watu kuvivunja.

Ni wakati sasa kuishauri serikali ikubaliane na wazo la katiba mpya. Endapo Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Katiba utaitishwa, utakubaliana juu ya ni njia ipi itumike ili kufanikisha sehemu iliyosalia katika mchakato wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye Watanzania wapate nafasi ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana.

Inajulikana kwamba watanzania wanaweza kusema HAPANA endapo itakuwa imebeba zaidi maslahi ya watawala kuliko watawaliwa. Katiba ni lazima ikatae ukandamizaji wa wananchi kama vile kubambikia watu kesi, kunyima haki zao za msingi hasa haki.

Katiba mpya ikatae kabisa viongozi kuwa miungu watu. Naamini kwa kuipata katiba mpya nchi yetu itasonga mbele kimaendeleo, kijamii na kisiasa. Itaepusha mengi mabaya ambayo tunayaona sasa kwa baadhi ya viongozi kujichukulia sheria bila kujali katiba. Naomba kuwasilisha.

Mwandishi: Elvan Stambuli

Editor; Global Publishers & Tv/ radio

Simu: 0784 339 616
 
mara nyigi nilikuwa najiuliza kwa nini viongozi na wafuasi wa Chadema mara zote ni Wakorofi na huioa lugha za kuitisha mamlaka?
Kumbe Jibu lake ndio hili, kweli waswahili husema mtoto wa nyoka ni nyoka.

Kumbe kiongozi wa Chama alikuwa ananunua na kupanga vitendo vya kigaidi....ndio maaana wafuasi wa chadema ni wakorofi hatari.

Ushauri wangu, viongozi wa Chadema na wafuasi wote badilikeni, acheni vitendo vya uvunjifu wa amani, na kwa sasa IGP katangaza operesheni kubwa ya kuwasaka wale wote wenye lengo la kuvunja sheria.

Ushauri kwa Jeshi la polisi;

kuna haja ya kufuatilia nyendo za viongozi na wafuasi wa Chaema kila kona ya nchi.
 
Wote na kundi lako zakuambiwa changanyeni na zakwenu, au ni mmoja wa kundi bambikizi, kisa uoga wa dai pendwa la wananchi. Katiba mpya itanyoosha wenye akili zilizopinda.
 
mara nyigi nilikuwa najiuliza kwa nini viongozi na wafuasi wa Chadema mara zote ni Wakorofi na huioa lugha za kuitisha mamlaka?
Kumbe Jibu lake ndio hili, kweli waswahili husema mtoto wa nyoka ni nyoka.
Kumbe kiongozi wa Chama alikuwa ananunua na kupanga vitendo vya kigaidi....ndio maaana wafuasi wa chadema ni wakorofi hatari.
Ushauri wangu, viongozi wa Chadema na wafuasi wote badilikeni, acheni vitendo vya uvunjifu wa amani, na kwa sasa IGP katangaza operesheni kubwa ya kuwasaka wale wote wenye lengo la kuvunja sheria.
Ushauri kwa Jeshi la polisi;
kuna haja ya kufuatilia nyendo za viongozi na wafuasi wa Chaema kila kona ya nchi.
Umesikika hongera
 
Watanzania tunajitambua tunasema
Ben saanane yupo wapi?
Azory Gwanda?
Nani alipanga na alipiga risasi lissu?
Mbowe kaonewa
Tozo ni kandamizi.
Watanzania tunaojitambua tunasema mwenyekiti aachiwe.
 
Hizi ni sababu za waotaka katiba mpya Tanzania

Utawala bora na utawala wa sheria ni upi? Ni maswali ambayo hujiuliza watu wengi nchini Tanzania na ni moja ya vilio vya baadhi ya Watanzania kwamba kunakiukwa katiba ya nchi.

Mifano ya uvunjifu wa katiba ni suala la wabunge 19 wa Chadema ambao wanalalamikiwa na chama chao kwamba wamejipeleka bungeni bila kufuata katiba ya nchi.

Jambo la kusikitisha ni kwamba wanaofanya ‘madudu’ hayo ni wasomi wenye shahada wengine tatu lakini hawaoni haya tunayoona sisi ambao hatukusomea sheria?

Nimefuatilia suala hili kwa muda mrefu lakini wenye mamlaka hawajatoa tamko rasmi kwamba ni sababu zipi zinafanya wanachama wale 19 wanaendelea kuhudumiwa na fedha za walipa kodi wakati ukweli ni kwamba wamefukuzwa uanachama. Wakanakaa mbungeni kinyume cha katiba ya nchi, hapo ndipo utawala wa sheria unapokiukwa.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimefuatilia kwa karibu msuguano unaondelea kati ya Spika wa Bunge na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) juu wa wabunge hao ambao kwa maoni yangu wamekosa sifa kwa kuvuliwa uanachama.

Mgogoro huu sio tu unasigina demokrasia lakini kwa upande mwingine unavunja katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Misingi ya demokrasia inatawaliwa na dhana ya ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi juu ya mambo ya msingi yanayowahusu katika taifa lao, kwa Tanzania kama ilivyo katika nchi nyingi duniani uwakilishi wa wananchi katika ngazi za maamuzi unafanywa kwa uwakilishi wa watu wachache waliyochaguliwa na wananchi hao yaani indirect democracy.

Kwa mujibu wa ibara 21, 39, 47 na 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa haki ya mtu kuwawakilisha wananchi katika ngazi za maamuzi kwa sharti la kupitia au kudhaminiwa na chama cha siasa. Hivyo, kwa Katiba ya sasa suala la udhamini wa chama cha siasa katika ngazi za maamuzi ni takwa la msingi la kikatiba.

Kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(e), Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge endapo mbunge huyo ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge, wanaoteuliwa ni kama hao wa Chadema wa viti maalum.

Hatua ya Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndungai kuendelea kutambua wabunge waliovuliwa uanachama na Chadema kwa tafsiri ya moja kwa moja ni sawa na kuvunja Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyoainishwa.

Kwa mujibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu; kinatambua umuhimu wa uwakilishi wa wananchi katika ngazi za maamuzi pasipo changamoto za kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977.

Ni wazi kwamba, changamoto za kikatiba zilizojitokeza katika hatua ya Chadema kuwavua uanachama wabunge wake na Spika wa Bunge kuendelea kuwatambua wabunge hao ni uvunjifu wa Ibara ya 71(1)(e).

Katika suala hili, Kituo kinaona haja ya kufanyika mabadiliko ya kikatiba kutambua mgombea binafsi ili kuepuka hatari ya kuvunja Katiba ikizingatiwa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria.

Ikumbukwe kwamba, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilitoa uamuzi wa kuhusu haki ya mgombea binafsi kutambuliwa katika ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.

Katika upande mwingine, katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 kumeshuhudiwa matumizi makubwa ya rasilimali za wananchi kwa kufanya chaguzi za marudio katika majimbo na kata mbalimbali kutokana na wabunge na madiwani kutoka chama kimoja kwenda chama kingine cha siasa. Ni muhimu kurekebisha katiba ya sasa pamoja na sheria ili kuruhusu haki ya wananchi kuwakilishwa pasipo kufanyika marudio ya uchaguzi ikiwa mbunge au diwani atahama chama chake.

Nitowe wito wito wa kurudisha mchakato wa katiba ili kusawazisha changamoto za kikatiba zilizopo sasa na kuepisha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 bara na visiwani.

Historia inabainisha kuwa mchakato wa kuandika Katiba mpya Tanzania ulianza kutokana na madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka Katiba Mpya itakayokidhi matakwa ya nchi ambamo wananchi ndio wenye kushika hatamu. Inaweza kuanzia ilipokwamia na jinsi gani ya kuendelea mbele ili kupata katiba mpya ya Tanzania.

Nimeandika makala haya ili kuamsha mchakato wa Katiba Mpya ili kuukamilisha hadi kupata Katiba Mpya yenye muafaka wa kitaifa na kijamii. Nia ni kuhakikisha Tanzania inapata katiba yenye ubora na itakayokidhi matakwa ya wananchi.

Makala haya nimeandikia nikikusudia pia kutoa elimu, kuhamasisha na kushawishi upatikanaji wa katiba jumuishi yenye viwango vinavyokidhi. Malengo yangu ni kuwapa hamasa wananchi kudai katiba mpya ambayo itakuwa imejumuisha mawazo yao. Pia wafanya maamuzi wanachokozwa na kuhimizwa kuendelea au kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Ni eleze kwa kifupi sana historia ya katiba yetu. Tanzania ni Jamhuri ya Muungano. Ni Muungano wa nchi mbili zilizoungana mnano tarehe 26 Aprili 1964, nchi hizi (Tanganyika na Zanzibar) awali zilikuwa huru na zenye mamlaka kamili. Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zipo katiba mbili, katiba ya pili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hivyo, kwa upande wa Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumewahi kuwa na Katiba zifuatazo, katiba ya Uhuru ya Mwaka 1961, Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962, Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1964 (Katiba ya Muungano), Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1965 na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwa kifupi, uandishi wa katiba zote tajwa hapo juu haukuwa shirikishi. Wananchi hawakupata nafasi ya kutoa maoni yao wakati wa mchakato wa kuandika katiba. Na pia, katiba zote ziliandikwa wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja. Baada ya nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 isingeweza kutumika bila kufanyiwa marekebisho makubwa. Kwa misingi hii, haja ya kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa haiepukiki.

Mchakato wa uandishi na maudhui ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake 14 vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutoshirikisha wananchi kikamilifu. Pamoja na mchakato kutokuwa shirikishi kwa wananchi, suala kwamba uandishi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ulifanyika nchi ikiwa kwenye mfumo wa chama kimoja nalo limekuwa likilalamikiwa na wadau mbalimbali.

Pia, mwaka 2010 Zanzibar ilipofanya marekebisho ya katiba yake ya mwaka 1984 ilipelekea madai ya kudai katiba mpya ya Muungano kuongezeka. Sambamba na hilo, hali ya kisiasa hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nayo ilidhihirisha haja ya kuandika katiba mpya ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi.

Kwa kuzingatia hayo Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba ya kuuaga mwaka 2010 na kukaribisha mwaka 2011 aliridhia kuanza kwa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya. Pamoja na shinikizo la raia kupitia makundi yao mbalimbali hususani asasi za kiraia na vyama vya siasa, uamuzi wa Rais ulichochewa na zoezi la kujitathmini wenyewe tukiwa wanachama wa Mpango wa Kujitathmini Utawala Bora Afrika (APRM) tangu 2010.

Baada ya uwamuzi wa Rais, serikali iliandaa muswada na kuuchapisha katika Gazeti la Serikali mnamo tarehe 15 Machi 2011 na kuwasilishwa Bungeni Aprili 2011 ambapo baadaye ulipitishwa kuwa sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 8 ya mwaka 2011.

Sheria hii iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhiwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011 ilimpa Rais mamlaka ya kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Rais aliteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Mwanasheria nguli, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba ili kupata katiba ya kudumu miaka 50 hadi 100 bila haja ya kufanyiwa marekebisho makubwa.

. Wajumbe walioteuliwa walikuwa 32 (ikijumuisha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wajumbe 16 kutoka Tanzania Bara na 16 kutoka Zanzibar. Muundo wa Tume ulihusisha wawakilishi wa vyama vya siasa, wasomi, AZAKI, madhehebu ya dini na makundi mengine katika jamii.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge Maalum la Katiba (BMK) lilikuwa na wajumbe kutoka makundi matatu. Kundi la kwanza lilikuwa ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kundi la pili lilikuwa ni wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Kundi la tatu lilihusisha uteuzi wa wajumbe 201 watakaoteuliwa na Mhe. Rais wa Muungano kutoka makundi mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania. Bahati mbaya sana bunge hilo halikufaulu kwa sababu za itikadi za kisiasa. Ipo haja ya kutengeneza bunge la katiba jipya litakalotuletea katiba mpya ambayo haitaruhusu watu kuvivunja.

Ni wakati sasa kuishauri serikali ikubaliane na wazo la katiba mpya. Endapo Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Katiba utaitishwa, utakubaliana juu ya ni njia ipi itumike ili kufanikisha sehemu iliyosalia katika mchakato wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye Watanzania wapate nafasi ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana.

Inajulikana kwamba watanzania wanaweza kusema HAPANA endapo itakuwa imebeba zaidi maslahi ya watawala kuliko watawaliwa. Katiba ni lazima ikatae ukandamizaji wa wananchi kama vile kubambikia watu kesi, kunyima haki zao za msingi hasa haki.

Katiba mpya ikatae kabisa viongozi kuwa miungu watu. Naamini kwa kuipata katiba mpya nchi yetu itasonga mbele kimaendeleo, kijamii na kisiasa. Itaepusha mengi mabaya ambayo tunayaona sasa kwa baadhi ya viongozi kujichukulia sheria bila kujali katiba. Naomba kuwasilisha.

Mwandishi: Elvan Stambuli

Editor; Global Publishers & Tv/ radio

Simu: 0784 339 616

Mkuu unahisi watanzania hawajaendelea kwa kiwango chako kwa sababu ya Katiba mpya. Katika uzoefu wako Kuna nchi hapa majirani kwetu watu wao kwa wastani wa maisha ya mlo mmoja kwa siku wanakula na kuishi vizuri na kwa raha zao kuliko watanzania? Kenya wamebadilisha katiba Yao. Nje ya kuwanufaisha wanasiasa, Mwananchi wa Kule slums asiye na ardhi huku Bwana makamu na mkuu Wake wanamiliki robo yake anafaidikaje.

Katiba mpya ije kwa wakati Wake. Lakini Sasa sio wakati Wake. Katiba Mpya inahitaji fedhaaaaaaa kama kweli tunataka iwe na wananchi.

Lakini la msingi, kama watanzania hatutakuwa serious na maisha yetu na Pia na sense ya uzalendo kwa Mali za nchi yetu. Na Hii ikajengeka toka Familia zetu. Hata uje na katibaaaaaa pyam badala ya mpya. Maendeleo, Sijui haki Nk. Utaskia tu.

Start na wewe Kazini kwako na maeneo yote. Unahisi una mahali pa kupafanya upya kwa manufaa ya watz wote. Wakiamzia wa karibu yako. Rahisi sna pale unapodhani kidole kimoja unawaelekezea wengine na kusahau the remaining four fingers.
 
Back
Top Bottom