Hizi ni njia 9 bora za kufanikiwa katika jambo lolote

Mbwana Mwaveso

New Member
Jun 23, 2016
4
23
Hizi ni Njia 9 Bora za Kufanikiwa Katika Jambo Lolote.
images-27-114954572.jpeg


Kila siku binadamu wote duniani tunajishughulisha hili tutimize malengo yetu. Katika maisha kuna watu ambao wanafanikiwa katika mambo yao na kuna watu ambao hawafanikiwi. Binadamu tunamalengo na mahitaji katika maisha yetu. Tunajishughulisha kila siku kuyatimiza malengo hayo. Malengo yanaweza yakawa ni maswala ya Elimu, Kazi, Ufundi, Cheo, Uongozi nk.

Tafiti zinaonyesha ni watu wachache sana wanaotimiza malengo yao duniani kote, inawezekana ukawa miongoni mwa watu ambao hawajafanikiwa kutimiza malengo yao. Umeangaika sana katika kutimiza malengo yako lakini unashidwa kutimiza. Una muda mrefu sana unasaka maendeleo lakini unakosa. Unakuta wenzako wanafanikiwa katika mambo yao wewe unashidwa.

Zifuatazo ni njia 9 bora zitakazokufanya ufanikiwe katika maisha yako.

1. Weka Malengo.
Malengo ni dira, ni kitu pekee kinachokuonyesha unahitaji kutimiza nini. Huwezi kufanikiwa wala kushidwa kama hujui unahitaji nini. Kuna msemo unasema “Huwezi potea kama hujui unapokwenda” Safari yoyote isiyo na muelekeo basi kokote utakapoishia ni sawa tu. Malengo ni kipimo cha kushinda au kushindwa katika maisha yako.

Jiwekee malengo ya mwezi, miezi mitatu, miezi sita, mwaka au zaidi ya mwaka. Unahitaji ujue unahitaji nini na kwa muda gani. Kwa mfano unaweza kupanga kutaka kuwa na elimu ya kiwango fulani, kua kiongozi katika ngazi fulani au kumiliki biashara. Na pia malengo hayo yaambatane na muda. Mimi binafsi nimepanga kuandika makala zaidi ya 400 katika blog hii ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, hivyo basi nimejipangia kila siku kuandika makala zaidi ya moja.

Lengo kuu ni kuandika makala 400 ndani ya mwaka huu(2018) ambayo itatimizwa kwa kuandika makala zaidi ya moja kila siku. Ifikapo mwisho wa mwaka nitaweza kujipima kwa idadi ya makala nilizoandika, kama ikiwa chini ya 400 basi nimeshidwa kutimiza lengo langu na kama itazidi zaidi ya 400 basi itakua nimefanikiwa kutimiza lengo langu. Malengo yanatupa motisha ya kuendelea kusonga mbele na kutuonesha tumefanikisha jambo kwa kiasi gani.

Wakati nilipokua sekondari nilikua na rafiki yangu ambaye yeye alikua anasoma sana na ni mtu ambaye alikua anajiwekea malengo ya kufaulu kwa kiwango cha juu sana kwenye masomo yake, mimi pia nilikua nasoma sana lakini nilikua sijiwekei malengo ya namna gani nifaulu. Alikua akinishangaza sana tukifanya mitihani na kurudishiwa utakuta labda darasani yeye ndo kaongoza kwa kupata labda alama A ya 85% unakuta analalamika kwamba amefeli, hakika ni jambo la kushangaza.

Unakuta mimi labda nimepata alama B ya 65% naona sawa na najihisabia nimefaulu kwasababu nimevuka kiwango cha necta cha ufaulu ambacho ni D “Pass” tofauti na ningepata F “Fail”. Nipomuuliza alinijibu kua si malengo yake bali alipanga kupata alama A ya 95% na kuendelea. Kwahiyo kupitia malengo yake ndio iliyomfanya agundue kua zile alama alizopata amefeli na mimi pia kuamini kwamba alama nilizopata nimefaulu ingawaje nilikua chini yake.

Hakikisha unajiwekea malengo. Malengo hayo yaambatane na muda maalumu, kwasababu kama yasipokua na muda unaweza ukajikuta unatumia miaka 20 kununua Baiskel na ukajiona kua umefanikiwa, Ni kweli utakua umefanikiwa kununua baiskeli ila muda uliotumia ni mwingi kuliko uzito wa lengo lenyewe.

Maana yake ni kwamba kama ulikua unafanya kazi basi ulikua hujitumi sana ulikua ukibweteka kwakuamini kua lengo lako ni dogo na unaweza kulitimiza. Weka lengo ambalo unajua litakuogopesha na kila ukilifikiria ata wewe mwenyewe uone kua hutoweza kulitimiza lengo hilo. Lakini pambana na uamini kua utalitimiza.

2. Tengeneza mpango mkakati wa kutimiza malengo yako.
Baada ya kujua unataka kutimiza nini na kwa muda gani unatakiwa upange ni jinsi gani unakwenda kutimiza lengo lako. Mpango mkakati ni njia na mbinu mbalimbali utakazozitumia kutimiza malengo yako.

Kama mimi nilivyojipangia kuandika makala zaidi ya 400 ndani ya mwaka huu, jambo hilo litatimizwa kwa kuamka asubuhi na mapema na kuanza kuandika makala zisizopungua mbili kila siku, kujifunza mambo mbalimbali, kupata taarifa mbalimbali na kusoma sana vitabu hili nipate kua na mambo mengi ambayo yatanisaidia kuandika makala zangu.

Kwahiyo siku yangu mimi haiwezi kupita bila kusoma sana, kujifunza wala kuandika, hizo ndo njia pekee zitakazoweza kunisaidie kutimiza ndoto yangu ya kuandika makala zaidi ya 400 ndani ya mwaka huu. Ata wewe unatakiwa kupanga ni namna gani utaenda kutimiza malengo uliyojiwekea. Mpango mkakati ni chombo cha kufikia malengo yako.

Sawa na unaposafiri kunakua na vitu vitatu mahali unapotoka, unapokwenda(Lengo) na chombo kitakachotumika kukufikisha unapokwenda(mpango mkakati). Mpango mkakati ni chombo muhimu cha kufikia malengo yako. Weka mikakati yako vizuri na siku zote uitekeleze hili utimize malengo yako.

3. Dhamiria kutimiza malengo yako(Commitment).
Hii ndio sehemu muhimu sana ambayo kila mtafuta mafanikio anatakiwa kuwa nayo. Dhamiria kutimiza malengo yako. Dhamira itakufanya upigane kufa kupona hili jambo lako litimie. Moja ya sababu kubwa inayofanya watu wengi washidwe kutimiza malengo yao ni kukosa dhamira ya dhati ya kutimiza malengo yao(Lack of commitment).

Ukipanga malengo na kujiwekea mikakati yako yote itakua ni kazi bure kama utashidwa kuji-commit katika kutimiza malengo na kutekeleza mpango mkakati wako. Dhamira ya dhati itakusaidia kua na nguvu pale utakapojisikia umechoka.

4. Kuwa tayari kujitoa.
Kujitoa kunahitaji moyo. Uwe tayari kujitoa kuyaacha mambo uliyoyazoea au unayopendelea kuyafanya na kuanza kufanya mambo yanayopelekea kutimiza malengo yako. Binadamu tunaishi kwa mazoea na kufanya vitu ambavyo tunapenda kufanya, sasa hapa unatakiwa uache mazoea na kufanya mambo yote ambayo unapenda kuyafanya na uanze yale ya muhimu tu katika kutimiza ndoto zako.

Nakumbuka kabla sijaanza kua mwanablog nilivutiwa sana na makala mbalimbali ambazo zilikua zikiandikwa na rafiki na mwalimu wangu Deo Kessy ambaye ni muandishi mashuhuri wa blog na vitabu. Nilimuomba Deo kua mentor wangu katika maswala ya uandishi, moja ya njia ambayo Deo alinipa ni kuamka asubuhi na mapema(kuanzia saa 10 alfajiri) na kuanza kuandika makala.

Kwakweli hili jambo lilikua gumu sana kwangu nilishazoea kuamka saa 12 paka saa 1 asubuhi kama basi nitaamka asubuhi sana basi ni kwaajili ya safari lakini si kusoma wala kuandika makala basi lilikua swala gumu sana kwangu aswa ukizingatia nilianza kujifunza kuandika kipindi cha masika, asubuhi unaamka baridi kali na kimvumvua au unakuta mvua kubwa inanyesha.

Na rafiki angu Deo alivyokua akinikomesha alikua anataka ikifika tu saa 1 asubuhi nimtumie makala aipitie kwahiyo nilikua sina jinsi lazima niamke na kuandika makala. Unaweza kuona jinsi gani nilikua mjinga kwanini nilikua siandiki usiku au mchana alafu ikifika kesho asubuhi nimtumie, hapana ilikua lazima niamke asubuhi maana asubuhi ni muda mzuri sana kwa kuandika au kusoma kabla jua alijatoka basi kwakua niliji-commit kutimiza lengo langu na kuandika makala kwenye blog ilinilazimu kutekeleza.

Hakika lilikua swala gumu sana kuacha tabia ya kuamka baada ya jua kuchomoza, lakini nilijitahidi kuacha hili nitimize lengo na ilinichukua takribani wiki tatu kuzoea kuamka alfajiri. Hata wewe unamambo ambayo umezoea kuyafanya kila siku lakini unapokuja katika swala la kutimiza malengo yako lazima uendane na ufanye mambo yatakayopelekea kutimiza malengo yako.

5. Kuwa na nidhamu.
Nidhamu ya kukamilisha malengo na ratiba uliyojiwekea. Kila jambo linahitaji nidhamu. Nidhamu ni zana muhimu sana ya kutumia wakati wa kusaka mafanikio ya aina yoyote. Nidhamu maana yake nini katika kutafuta mafanikio? Ni kufata mipango na mikakati yote uliyojiwekea katika kutimiza malengo yako.

Hakuna mtu atakaye kujakukuforce wala kukusimamia katika kutekeleza mipango yako bali ni wewe mwenyewe ambaye utasimamia mipango hiyo. Kwahiyo unatakiwa uwe na nidhamu ya hali ya juu. Nidhamu itakusaidia kujiona mkosaji pale itakapotokea umeshidwa kutekeleza mipango uliyojipangia, kwahiyo itakusaidia kutimiza atakama kuna vikwazo kiasi gani.

6. Husikate tamaa.
Katika safari ya mafanikio inakua na vikwazo vingi sana. Kama unaona unatimiza lengo ambalo halina vikwazo basi ujue hilo lengo si saizi yako. Lengo ambalo zuri na lenye tija linagubikwa na vikwazo vingi sana tena kuna wakati unajihisi ata kulia. Sababu kubwa inayowafanya watu wengi washidwe kufanikiwa ni kukata tamaa.

Wanaanza kufanya jambo wakiona vikwazo vingi wanaacha. Kwa mfano mimi nisingeweza kushindana na usingizi wa alfajiri na uvivu wa kuandika basi ata mafundisho mazuri kama haya ndugu msomaji wangu husingeyapata. Vikwazo ni vingi sana katika safari ya mafanikio jitahidi kupambana nayo, hakika utafanikiwa.

7. Husibweteke na machache uliyoanza kuyatimiza.
Hapa ndipo wengi wanaposhidwa. Katika safari ya mafanikio kunakua na vipindi. Kuna kipindi utafika utaanza kuona matunda ya jitihada zako. Hapa wengi ukosea sana, watu wengi wakishaanza kuona matunda ya jitihada zao basi kama alikua akifanya sana kazi utakuta anaanza kuzembea. Katika kipindi ambacho unatakiwa ukazane sana tena sana yaani uongeze juhudi mara mbili ni kipindi cha kuanza kuona matunda ya jitihada ulizoziweka juu ya jambo fulani.

Niliwai kusoma historia ya mwanasoka nyota duniani anayeitwa Christian Ronaldo, kikubwa kilichonishangaza katika historia hiyo ni pale nilipoona kua pamoja na mafanikio yake makubwa aliyoyapata lakini ni mtu ambaye anafaynya sana mazoezi kuliko mchezaji mwingine yoyote duniani ilifika kipindi daktari wake alimwambia apunguze kufanya mazoezi. Wachezaji wenzake walikua wakiingia uwanjani kwaajili ya mazoezi wanamkuta na wakitoka wanamuacha na ndio siri kubwa ya mafanikio yake.

8. Weka bidii sana.
Katika kila jambo unalolifanya lifanye kwa ufanisi wa hali ya juu. Jitahidi kuweka bidii kwa kila jambo. Dunia ya sasa ni dunia ya ushindani, kila unachokifanya unatakiwa ukifanye kwa ufanisi mkubwa sana. Kila kitu ni kushindana, ukifanya jambo kwa uvivu hautafanikiwa kamwe. Waswahili wanakwambia “Mkono mtupu haulabwi”. Jitahidi sana uwe na kitu cha kukufanya ukaonekana ni mtu mashuhuri na si kingine bali kufanya unachofanya kwa bidii.

9. Jitathimini.
Kujitathimini ni kitu ambacho unatakiwa ufanye katika vipindi vyote vya kutimiza malengo yako. Kila hatua unayopiga unatakiwa uangalie kwa umakini zaidi ulipotoka, ulipo na unapokwenda katika kutimiza malengo yako. Hili litakusaidia kujua umahiri na udhaifu wako. Na ata kama utashidwa itakusaidia kujua ni kipi zaidi kilipelekea ushidwe na kuweza kijirekebisha katika mpango mwingine. Kujitathimini ni jambo ambalo anatakiwa alifanye kila binadamu, inasaidia kujitambua na kujijua zaidi. Kujitathimini ni kitu ambacho tunatakiwa tufanye binadamu katika kila hatua tunazopitia.

Naamini kupitia njia hizi basi utakua mtu tofauti kabisa, nitaanza kukuona ukitimiza malengo yako na kukuona katika kilele cha mafanikio. Nakutakia mafanikio mema.

Husisahau kushare kadri uwezavyo, share kwa marafiki zako nao wapate maarifa.

A.M.Mwaveso
amwaveso@gmail.com
 
huna lolote policcm wewe...kazi ni kumpampa mkuu tu...hujui kuwa kuna cku atastaafu??????????
 
Mafanikio wanasema jitihada hazishindi kudra, watu wana haha uwanja mzima mfungaji kaingia dk93 maisha ni fumbo, kuna mtu alikuwa Na kila kitu hivi sawa anatembea anaongea peke yake watoto kawatoa private ya bei mbaya sasa wako kayumba, ukizungumza nae kakosa kujiamini hakutizami usoni, kapata kisukali miguu inavuja Maji isee usimcheke mtu " kabla hujafa hujaumbika,
 
Na katika yote uyafanyayo mkabidhi Bwana Mungu wako naye atakufanikisha!!!!
 
mbona ni njia zilezile tangu niko la 7, au ni kwaajili ya form 4 wanaomaliza mwezi wa 10?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom