Hizi ni miongoni mwa sababu zinazofanya kila mtu hapa sasa anatamani kuwa Mwanasiasa na hasa Mbunge!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
581
1,000
Sitaki kuongea mengi kuhusu suala la watu wengi hapa Tanzania sasa kutamani kufanya kazi ya siasa na hasa kuwa Mbunge.

Na ukitazama vizuri utagundua kuwa hii ndo siri kubwa ya kujitokeza kwa WATIA NIA ( Wagombea Ubunge wengi katika kura za maoni za CCM mwaka jana kuvunja rekodi).

Watu wengi wamekata tamaa na ufanisi duni,usumbufu na mazingira duni ya uzalishaji katika sekta zingine!

Mtu akifikiria kusajili kampuni BRELA kazi iliyokuwa ikichukuwa siku 3 hadi 7 huko nyuma leo inachukua hadi mwaka 1 kupata usajili au kuhuisha taarifa, kwanini hasitamani kazi ya kufanya siasa!

Mtu akikumbuka usumbufu wa TRA na kodi, penalty za ajabu ajabu kwa nini mtu hasitamani kazi ya siasa!
Afisa wa TRA anabishana na mlipa kodi kuhusu " Provisional tax assessment" hata kabla ya Biashara kuanza!!!

Kila mtu lazima atamani kuwa Mbunge,kazi ya kupiga meza na makofi bungeni ndani ya mwezi milioni 12 zinaingia kwenye akaunti yako!

Benki za Biashara zikisikia Wabunge wapya wameingia wanakimbia kwa Spika kuomba kuandaa michapalo ( cocktail parties) kwa ajili ya kuwanasa wakope fedha hadi milioni 600 kwa Mbunge mmoja!

Sasa waite au wafuate hao Benki kwamba una fursa ya kuanzisha kiwanda kidogo cha mafuta ya kula cha milioni 150 na kila kitu unacho kuanzia dhamana, upatikanaji wa malighafi, masoko, ila unahitaji ku- improve working capital uone muziki wake!

Utapigwa maswali au utajaza fomu mpaka unaweza kukimbia na kuacha mkopo kama una roho nyepesi!

Hii Nchi bila watu kubadili mindset hatuwezi kutoboa !
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
39,025
2,000
Mifumo mibovu ya serikali ya CCM, mbunge 12M kwa mwezi bado posho na vinginevyo kwanini usikimbilie huko na wakati ni kwenda kugonga meza pekee hakuna la maana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom