Hizi ni mbinu za tume ya uchaguzi ili vijana wengi tusipige kura... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ni mbinu za tume ya uchaguzi ili vijana wengi tusipige kura...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Oct 21, 2010.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Habaar zenu Wana JF
  Nimetafakali sana na kujua kwa nini Vijana wengi hawatapiga KURA kutokana na HUJUMA za Tume ya Uchaguzi. Yaliyotokea kwa Vijana wa Chuo Kikuu yanareflect vijana wengine wengi wa Tanzania.
  Ikumbukwe Kuwa Mimi Siyo GODORO nakaa sehemu moja tu kwa Miaka MITANO. Na wakati mwingine hata Godoro linabadilishwa position.
  Miaka ya Nyuma Kidogo wakati nasoma Chuo,mwaka 2005 nilijiandikisha kama Mpiga Kura pale Chuoni,Upanga West na baada ya kuhitimu chuo mwaka 2007 nikapoteza haki yangu(presumably) ya kupiga kura katika jimbo la Upanga west kwani nilienda kuishi Kinondoni kwa Manyanya na Mwaka 2009 nikahamia Kikazi Kanda ya Ziwa ndo nikawa Mbali kabisa na kituo changu cha kupigia Kura, Mwaka huu wakati wanafanya Marekebisho ya Daftari la wapiga Kura nilikuwa Kanda ya Ziwa nikabadilisha Taarifa lakini mwanzoni mwa mwezi August nikahamia kikazi mikoa ya kusini Mwa Tanzania.....Nikiwa nimepoteza kabisa uwezekano wa kupiga kura katika kituo changu cha Kanda ya ziwa kwani siwezi kusafiri kutoka Mtwara au Lindi kwenda Mwanza kupiga kura katika hali hii ngumu ya Kiuchumi. Niliwaandikia tume ya Uchaguzi kuomba kuruhusiwa kupiga Kura huku huku kusini kwani kwa sasa mimi ni raia wa huku na Maendeleo katika ngazi zote mtaani ninapoishi yananigusa hivyo ningepaswa kuchagua Diwani,Mbunge na Rais.....lakini sijapata majibu. Juzi nilienda katika kituo cha Mtaani kwangu ili angalau nipige Kura ya Urais nikaambiwa 'NO' Haitawezekana.
  Katika hali hii mambo mawili makuu yamedhihirika:
  1. Tume ya Uchaguzi inatambua kuwa Vijana wengi sana ni 'Mobile' na kwa kuwa wanatembea tembea wanashuhudia serikali isivyo wajibika katika sehemu mbali mbali na kuanza kupiga 'vuvuzela' za mabadiliko ya Uongozi na njia pekee ya kuwazuia kutimiza haki yao ya kuiondoa serikali madarakani na kuleta mabadiliko ni kuweka Utaratibu Mbovu saana wa kupiga kura ili wengi wasipige kura.
  2. Kwa hali ilivyo CCM lazima ishinde kwa sababu watu wasio hama hama mara kwa mara kutafuta Maisha ni wakulima wa Vijijini na hao hao ndio bado wanaona Maisha ya kimasikini ni HAKI yao ...(utakuta nyumba ya nyasi na udongo na matobo kibao paani hadi ukutani na wanalala na wanyama ndani..nje kuna poster ya Chagua CCM Chagua Kikwete).
  PENDEKEZO
  Ili kuleta Mabadliko ya Kisiasa ni lazima tume ya Uchaguzi iandae electronic Voting system inayoruhusu mtanzania kupiga kura popote alipo..Japo kuwa Chance ya Serikali Kuchakachua Matokeo ya kielectronic ni Kubwa lakini hiyo ni DHAMBI ya serikali na mimi nitakuwa nimetimiza HAKI yangu. Mifumo hii imefanikiwa nchi nyingine na haijaleta malalamiko

  Nasikitika Kwamba harakati za kutafuta Maisha zimenifanya nipoteze haki yangu ya kupiga Kura.
   
 2. K

  Kaka Joe Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  The fact is wana Jamiiforums home of great thinkers, as it has been said and quoted "You can fool all the people some of the time, and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time. I believe that all this dirty politics will one day come to an End no matter what,
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  With Dr. Slaa at the helm of the nation all things are possible
   
Loading...