Hizi ni hela za kweli au fake? Mbona nyingi hivii

Cascos

New Member
Oct 13, 2012
0
198
Habarini jamvini,

Leo katika pita pita zangu YouTube nimekutana na video ya wimbo wa msanii Moni Centrozone unaokwenda kwa jina la 'MIHELA'. Kilichonifanya nikaja na uzi huu ni zile pesa zinazoonekana kwenye ile video, ni nyingi saaana kiasi kwamba kama ni zake basi ni miongoni mwa wasanii wenye hela zaidi Tanzania na kama sio zake ni za nani? (Kujua ni za nani haiwezi saidia kitu) Swali ni: Je, zile pesa ni real au fake? Kama ni real money kwanin hawajaweka Tsh na badala yake wameweka euros na dollars?

Kwa ambao hamjaiona video ya 'MIHELA' mnaweza kuitazama hapa kisha tukajadili kwa pamoja kama ni hela fake au real money!!
Halafu mbona huyu nae "Moni Centrozone" hajakamatwa kama kina Maua Sama na Soudy wakati na ye amekanyaga "MIHELA"?
 
Hayo ni makaratasi tu, kama angekuwa na hela kihivyo wazazi wake bado wangekuwa wanaishi nyumba ya udongo tena ya kupanga?
 
Back
Top Bottom