Hizi ni dharau zingine wanazofanya wanaume kwenye ndoa

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,311
7,494
Imebainika kuwa asilimia kubwa za wanaume ukifuatilia kwa ukaribu majina ya watoto wao wa kwanza au wa tatu waliozaa kwenye ndoa ,majina ya kike walio wapa watoto wao ni majina ya wanawake ambao waliwahi kuwa michepuko yao

Kuna kisa kimetokea nikaanza uchunguzi nimegundua ni kweli na wanaume mna dharau hatari

Katika kisa chenyewe kuna dada mmoja yupo kwenye ndoa ameingia na mgogoro na mume wake hadi anatamani alifute jina la mtoto wake wa kwanza amuite jina lingine na huku yule mtoto alisha lizoea na yupo darasa la pili kwa jina hilo

Huyu mdada aliambiwa na mashost wake kuwa kuna mwanamke alikuwa mchepuko wa mume wake kabla hajakuoa ,ila kwa sasa kuna ishara ya kutaka kurudiana

Siku moja hakuvumilia alimfuata huyo mwanamke na kumuuliza nini kinaendelea na mume wake ndipo huyo mwanamke alimwambia maneno mazito

"Wewe unafikiri isingekuwa nyodo zangu unafikiri angekuwa mume wako au angekuwa wa kwangu, huyo mwanaume ananipenda mpaka sasa tena sana,tena ili uamini Mimi naitwa Angel na mtoto wako wa kwanza anaitwa Angel,unafikiri aliita jina langu bure kwa mtoto wake,alinipenda na mpaka sasa ananipenda"

Wanawake tuwe makini kuhoji majina ya watoto wetu wanayopewa na wanaume

Hivi na wanawake huwapa majina watoto wao wa kiume kama kumbukumbu ya mchepuko ambao alikuwa anaupenda enzi hizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vinapitwaga na wakati nashangaa ndoa na Ngono bado vipo tu..
Hapa Najaribu kuwaza Kwamba kwann isitokee Wanaume tugome kuoa kabisa tuone itakuaje maana Hawa ndugu zetu Ndoa wanataka kugeuza Kauwanja kakutokomolea.. Ndoa Ni Kama chupi, ukiona itakustiri we vaa tu.. mambo yakuchunguza chunguza utajidharirisha tu
 
Nyie mnaona mpo sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha Kuna page fulani insta Kuna mwanamke alisimulia alibeba ujauzito siku ya kujifungua nusura akufwe..Mume akatoa jina lililotoka kwa mchepuko..😂😂...mimba nibebe Mimi jina atoe mchepuko..🙄🙄 qudadekiiii!!!
 
Evaaaa.. jina zuri kweli lilianza kunifatafata kitambo sijui mbeleni itakuwaje..😅
 
Mungu akijalia mwaka huu mwishoni mwenyewe ninatarajia na hiki kitu sijawahi kukifikiria lakini kupitia maada yako umenifikirisha lakini nilikua naangalia names from UK, Spain na Italy. Ila siwezi kumpa mtoto wangu jina la mchepuko wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vinapitwaga na wakati nashangaa ndoa na Ngono bado vipo tu..
Hapa Najaribu kuwaza Kwamba kwann isitokee Wanaume tugome kuoa kabisa tuone itakuaje maana Hawa ndugu zetu Ndoa wanataka kugeuza Kauwanja kakutokomolea.. Ndoa Ni Kama chupi, ukiona itakustiri we vaa tu.. mambo yakuchunguza chunguza utajidharirisha tu
😃😃😃
 
Back
Top Bottom