Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,512
- 5,965
BLUE BAND - watanzania wengi hawalijui neno la siagi, msamiati wa siagi umekuwa blueband kwasababu ni bidhaa iliyoweza kupata umaarufu kwa muda mrefu sana, hii kitu ikipakwa kweye mkate ushushie na chai ni ladha amazing sana.
KIWI - vile vile nayo imekuwa msamiati rasmi wa rangi ya kungarisha viatu, ni kwa muda mrefu sana wamekamata soko na sisi wateja tumeridhika, kwenye maandalizi ya kufungua shule hii bidhaa haikwepeki
KASUKU KIBERITI - Unapozungumzia kuwasha moto watanzania wengi tumezoea kiberiti na kiberiti maarufu ni Kasuku, Matumizi yake ni mengi sana kuanzia kuwasha jiko, kuchoma taka, kuvuta sigara, kuwasha mishumaa, n.k.
GOOD MORNING (dawa ya kikohozi) - hii dawa ipo mpaka leo kwenye maduka lakini ipo tangu muda mrefu, dozi yake ni kimfuniko chake mara 3 kwa siku ila uwe makini uweke mbali na watoto maana ni tamu wanaweza kunywa yote kwa mpigo.
VASELINE (Mafuta ya mwili) - losheni na mgando mafuta ya ngozi, watoto, nywele, n.k. ubora wake umeweza kujijengea jina na kuwa chaguo la watu wengi kwa muda mrefu.
OMO (kabla yake kulikuwa na aerial) - ni sabuni iliyoweza kuteka soko kwa muda mrefu, ni gharama kuzidi sabuni nyingi zenye ujazo mkubwa kwa bei chee, soko lake ni kwa wateja wanaojali zaidi ubora kuzidi ujazo,
PIPI, Big G na pipi kali, - Msamiati mwengine tunaotumia kwajili ya bidhaa maarufu za Kenya ni big g, Kwenye pipi kuna kifua na machungwa, kuna PK maarufu kama pipi kali. kuna watu wana survive kwa kuuza hizi bidhaa pekee wameziweka kwenye ungo maeneo ya stendi, watoto wanazipenda, zinatumika kukata harufu, n.k.