Hizi nguvu za kichawi za Wakongo ni hatari sana.. Yaliyotokea kambi ya wakimbizi Nyarugusu Kigoma yanatisha!

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Kuna mkubwa au kiongozi wa wachawi ndani ya kambi ya wakimbizi Nyarugusu Kigoma amefariki na kabla ya kufariki alitoa maagizo kwa ndugu na jamaa zake kuwa siku akifariki basi wachukue mwili wake na waukatekate viungo tofauti tofauti na kila kiungo kizikwe tofauti au kila kila kiungo na kaburi lake.

Sasa baada ya kufariki hivi juzi tu ndani ya kambi nyumbani kwake ndugu zake hawakufuata maagizo yake ya kukatakata viungo vyake ili vizikwe tofauti badala yake wakachukua mwili wa marehemu na kuupeleka hospitali ndani ya kambi.

Kilichotokea baada ya hapo kila mmoja amepigwa na butwa,toka nyumbani kwake mpaka hospitali ardhi imepasuka na kuweka mashimo na mpaka kuta za hospitali nazo imepasuka kuweka nyufa kila ukuta

Wafanyakazi na wakimbizi ndani ya kambi wamebaki kuduwaa wasijue la kufanya. Ila hakuna aliyeshiriki mpaka sasa.

Nina video zake kutoka kambini zinazoonyesha hizo nyufa za ardhi na ukuta wa hospitali ilivopasuka na audio pia ila audio ipo kwa lugha ya Kirundi sijui kama zinakubalik kuzi load hapa JF.
 

Attachments

  • Nyarugusu 2.mp4
    11.2 MB · Views: 49
  • nyarugusu 1.mp4
    6.5 MB · Views: 46
duniani kuna wanga *****, kwa hili tukio lazima watafata maelekezo
 
Kwahiyo ni kipi hasa kinachokufanya uamini kwamba kupasuka kwa ardhi kuna uhusiano na huyo marehemu? Ulimuona huyo marehemu akipasua hiyo ardhi? Si inafahamika wazi kwamba mivutano chini ya ardhi ndio husababisha ardhi kupasuka ili kurelease ile presha inayokuwa imelundikana chini ya ardhi? Sasa huyo marehemu ameingiaje?
 
Unawezaje kuthibitisha kuwa huo mpasuko wa ardhi ni kutokana na kutokutimizwa masharti ya huyo mganga baada ya kufariki?
Je kwa kuwa bado hajazikwa na yupo bado amehifadhiwa, iweje hayo yatokee...?
Ina maana akizikwa kwa kukatwa katwa na kila kiungo kuzikwa kivyake hiyo ardhi itarudi katika hali ya kawaida?
 
Dadadeki....
Ngoja nisome Comment za Wana Sayansi kwanza, hiyo kwao ni Earthquake tu!
 
hii inaonyesha kwamba hata uwe na nguvu kiasi gani uwe mchawi kiasi gani ila kuna mwenye nguvu zaidi yako ambae atachukua pumzi yake ...

UTUKUFU WOTE NI KWA MUNGU [HASHTAG]#AMINA[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom