Hizi ndo shule 100 Kongwe na zilizotikisa Tanzania, na asilimia 90 humu tumepitia katika shule hizi

Mleta mada nadhani kabwia kiasi.... unaleta news zisizo na Data... weka miaka ya hizo shule tuone ukongwe wake... mfano hizo za jeshi kama Makongo siwezi kukubali kama ni Shule Kongwe... labda kama zama hizo hazikujulikana sababu walisoma wanajeshi pekee na baadae kuchanganya na raia... kuna Shule sijaziona hapo na ni nzee... afu hajaweka haswa kama ni Secondary school only au na primary pengine na Nursery.... Shule za Agakhan hajaweka hata moja.. even International School of Tanganyika... Shule Kongwe za Zanzibar hajui hata moja. ... nadhani katunga mada huyu
International School of Tanganyika (sekondari) siyo kongwe, ilikuwa ya msingi na chekechea, Bunge na Upanga. Wazungu, wahindi na wengine wenye uwezo sekondari walikwenda Iyunga.
 
Kitu namba 79 hiyoooo watu sema oyoooooooo, michezoooo tunachezaa vzri, shule yangu ..... Nitskuenziiiii, wapi wasikaji zangu acha kabisa majita road
 
Mbona kongwe nyingi sizioni, kwa mfano Musoma Alliance, Mkwawa High School, Itaga, Rugambwa, Shaaban Robert na Forodhani. halafu kuna shule juzi tu kama Jitegemee ambayo ilikuwa kwa ajili ya askari wa JWTZ kambi ya Lugalo tu enzi za Nyerere ambaye alitaka wanajeshi wote wawe na elimu at least ya kidato cha nne. Kuna shule nyingi za namna hiyo zilizokuwa makambini, kama ile ya Milambo Baracks Tabora na ile ya Nachingwea Baracks: sijui kama hizi bado zipo.
Kabisa.
 
Miaka ile ya sabini, timu ya mpira ya Musoma Alliance ilichachafya sana timu zote za mkoa wa mara; nadhani mpiga chenga wao mkubwa na mfungaji mkubwa wa magoli mkoani na taifa cup baadaye nadhani alikuwa ni profesa pale UDSM; Professor Bwatwa (sina uhakika kama ni yeye kweli ila Bwatwa wa Msuoma Alliance wakati huo alikuwa kama Pele). Halafu Mkwawa miaka hiyo iliitikisa wizara ya elimu mpaka wakaamua kuipandisha kutoka shule ya sekondari hadi kuwa chuo. Sekondari za wakati huo walikuwa miamba sana.
 
Hata Kilakala haipo!
Kama kilakala haipo Mod wafute uzi huu ukapangwe upya. Huwezi kuitaja Mzumbe bila kilakala
Ilikuwa balaa ndio tulikuwa tunatoana stress kwa muziki enzi hizo vibao vya Lady Madona, Break dance za Michael Jackson, vinatamba
Tunavaa suruali dont touch, nywele umepiga push back usafiri kwenda disco Kilakala gari la shule Isuzu TXD hili ni lori
 
Back
Top Bottom