Hizi ndo hoja za wabunge wetu

Mukuru

Member
Apr 14, 2009
40
0
Komba ‘amzimia’ Waziri Nagu

Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba amemsifu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Mary Nagu, kuwa ana sura nzuri na anauzika.

Mbunge huyo amelieleza Bunge leo kwamba, yupo tayari kutunga wimbo wa kumsifu Waziri huyo.

Kabla ya kutoa sifa hizo, Kapteni Komba alisema bungeni mjini Dodoma kwamba, Dk Nagu leo kapendeza kuliko siku nyingine zote.

Mbunge huyo ametoa sifa hizo wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko iliyowasilishwa leo bungeni.

Komba amesema, pamoja na sifa za uzuri wa sura na kuuzika, kwa kuwa Waziri Nagu ni mwanamke ana uwezo wa kutekeleza ombi lake la kuwasafirisha wawekezaji kwa ndege hadi Songea ili wafike Ziwa Nyasa.

Amesema, si rahisi kwa mwekezaji kusafiri kwa gari umbali wa kilomita 1,200 hadi Ziwa Nyasa lakini wakienda kwa ndege hadi Songea, wataweza kuwekeza huko kwa sababu watasafiri kwa gari kilomita 80.

Komba amesema, uwanja wa ndege wa Songea ni mzuri kama wa Mwanza lakini hakuna ndege zinazokwenda huko.

Amewakaribisha Dk Nagu na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Cyril Chami, Songea, Ruvuma na Ziwa Nyasa.

Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya, amesema, Dk Nagu, Dk Chami na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, wanastahili kuiongoza Wizara hiyo.

Kwa mujibu wa Mzindakaya, Mapunjo ana uwezo mkubwa wa kusimamia mambo hivyo Wizara hiyo imepata kiongozi mzuri. Mbunge huyo ameyasema hayo leo wakati anachangia bajeti ya Wizara hiyo.

Mzindakaya amesema, amefanya utafiti wa uhakika na kubaini kwamba, Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) ndiyo nchi tajiri zaidi kwa rasilimali miongoni wa nchi za maziwa makuu.

“Sasa uamuzi ni matumizi, mnavyoamua wenyewe kutumia” amesema Mzindakaya na kusisitiza kwamba,Tanzania isiendelee kufanya kosa la kuuza bidhaa ghafi nje, iuze bidhaa zilizosindikwa.

Mbunge huyo amesema, Wizara za Viwanda,Biashara na Masoko, Maliasili na Utalii, Kilimo, Chakula na Ushirika, Fedha na Uchumi zinapaswa kuandaa mfumo wa kufanya kazi pamoja ili programu ya Kilimo Kwanza iwe na manufaa kwa Taifa.

Mzindakaya amesema, utekelezaji wa programu ya Kilimo Kwanza uende sanjari na kasi ya kuiimarisha sekta ya viwanda, na pia hamasa ya kukuza usindikaji iendane sambamba na kasi ya kuimarisha masoko ya bidhaa.

“Kama halifanyiki hivyo tutaendelea kuwa watumwa kwa mambo mengine ambayo tunayaweza” amesema Mbunge huyo.
 
Huyu akaimbe tu, Chama Chetu cha mapidunziii cha jenga nchiiiiiiiiiiiiii..
 
Kwa mtu kama John Komba tutegemee nini la zaidi?. Ubunge aliupata kwa ajili ya kuimba na bila kusahau ni mgoni huyo wagonjwa sana kwa akina dada.
 
Anna_Lupembe.jpg
 
Mnategemea nini cha maana toka kwa John Komba?. Picha tu inajieleza ni mtu wa namna gani. Sishangai kabisa kumsifia na kumzimia waziri Mary Nagu.
 
Wabunge wengi na wanabofoa tu! binafsi sioni sababu kwanini wanakaa muda mrefu Dodoma wakati mambo mengi yanajiruduia na wachangiaji ni hao hao wengi wanasindikiza na kuunga hoja.

Na huyo mama hajitazame mngoni kambeep hakijichekesha tu kang'oka, alaah!
 
Uwakilishi wa wananchi si sawa na uimbaji kwa kweli. Sasa nimeamini kwa asilimia 100........
 
Duh katika pitapita za leo kwenye magazeti, nimeikuta hiki (kwangu ni kituko) manake inaonyesha wazee wetu waheshimiwa kweli wamekosa dira au pointi za kuongelea ndani ya lile Bunge letu "TUKUFU"

Mbunge ataka mawigi yapigwe marufuku

Na Sharon Sauwa
29th July 2009

Mbunge mmoja leo ametoa kali ya mwaka bungeni baada ya kuinuka na kuitaka Serikali ipige marufuku wanawake kuvaa nywele za bandia al maarufu mawigi, kwa madai kuwa nywele hizo ni za maiti.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Mji Mkongwe, Mhe. Mohamed Ibrahim Sanya, wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni leo asubuhi.
Mhe. Sanya akasema kwakuwa katika miaka ya 1960, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Aman Abeid Karume alipiga marufuku matumizi ya nyewele bandia ambazo wakati huo zilijulikana kama nywele za maiti na kwa kuwa imejengeka ulimwenguni kote dhana ya wanawake kuvaa nywele hizo bandia; "Je, Serikali haioni kuwa umefika wakati ikapiga marufuku matumizi ya nywele hilo ili watu waweze kutukuza nywele zao za asili, isipokuwa wale wenye vipara?"
Katika swali lake la pili la nyongeza, Mhe. Sanya akauliza: "Kwa kuwa Serikali inatumia kiasi kikubwa cha fedha kutibu maradhi ya kansa, haioni umuhimu wa kupiga marufuku vipodozi vyote na badala yake wanawake wajipambe kwa kutumia hina na wanja kama wanawake enzi za Mtume Muhammad (S.A.W) walivyofanya?"
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda, akasema kazi ya Serikali ni kushauri pale penye madhara.
Akasema hadi sasa. Serikali haijapata ushahidi wa kisayansi kuhusu madhara yatokanayo na watu kuvaa nywele za bandia.
Akawasihi wanawake waangalie kama wana aleji wanapotumia nywele hizo na jinsi ya kuepuka madhara yanayoweza kutokea kabla ya kutumia nywele hizo, kwa vile nyingine hutengenezwa kwa kutumia nailoni.
Kuhusu vipodozi, Dk. Kigoda amesema vile vinavyoharibu baadhi ya viungo kama vile ngozi, vimeshapigwa marufuku na Serikali.
Akasema kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA, Serikali inaruhusu vipodozi visivyokuwa na madhara kutumiwa na binadamu.
Kwa mujibu wa Dk. Kigoda, Serikali imeandaa vijarida, vipeperushi na vipindi vya uelimishaji kupitia redio, televisheni na magazeti kuhusiana na vipodozi vilivyo na viambata vyenye sumu.




CHANZO: ALASIRI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom