Hizi ndizo sheria nilizomuwekea mke wangu juu ya mimi na mpira

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Wasalaam wakuu


Kipenzi mke wangu najua ananijali sana na kunipenda , ndiyo maana akakubali kwa kila hali na namna ifaayo kunipokea

Na kabisa baraka tele ziwe juu ya huyu mwanadada juu ya maswahibu yangu aendeelee kutunza familia yangu na watato wangu

Nayeye haachagi kunisifia kuwa ni mwanaume mwaminifu msikivu na mtiifu ,,,

Lakini linapofika swala la Mpira wa miguu, ni kama mke mwenza wake,, nmekuwa mtu wa kutoka sana kwenda kwenye vibanda umiza kufata vibes lakini pale inapobidi mimi kuangalia mpira nyumbani




Na hizi ndiyo sheria na bashtwitwi anazokutana nazo kutoka kwa mimi mume juu ya swala zima la Mpira






1. Remote ya TV hakikisha muda wote iko mikononi mwangu


2. Wakati game inaendelea epuka kuniuliza maswali ya kipuuzi .

mfano

"Eti hubby hao Barcelona wanacheza na Ujerumani??


3. Wakati game inaendelea uwe unaniangalia usoni, na ukihisi Natabasamu basi nawewe Tabasamu, ikiwezekana nikiss😘 kama unavyofanyaga ila ukiona nimenuna😠 Aidha nawewe Nuna au Chomoka ingia chumbani kimya


4. Huyo dogo anayenyonya mda wote wa game hakikisha hajui kitu chochote kinachoitwa Kulia😭

5. Wakati game inaendelea pita Mgongoni kwangu, kama ni lazima upite mbele yangu pita kwa kutambaa Sakafuni,, sawa mama nakupenda enhee😍

6.Tumia mbinu zote kutambua moyo wangu upo Timu gani... Ukiona nipo timu usiyoipenda ....🚶‍♀️nyooka jikoni au Chumbani kimyakimya, Ukachezee simu yako hadi uchoke, na ndiyo muda mzuri wa kuchart hata na mashost zako ambao huwa sipendi uwasliane nao


7. Huko Ulaya nitakusamehe utachagua timu yoyote tofauti na yangu mimi ,, ila hapa kwetu kama moyo wako haupo MSIMBAZI ni aheri ushangilie timu yoyote ya kule kwenu Zanzibari hata Jang'ombe FC kuliko hawa wapinzani wetu.

8. Katika kipindi cha Kombe la Dunia na Michuano ya Kimataifa🏆 kama moyo wako hauko Brazil🇧🇷 au Ufaransa , basi kipenzi mke wangu sio mbaya kama utaenda home Tanga kumsalimu mama mkwe wako ukae kule hata mwezi muendelee kupika mapishi yenu yale ambayo huwa ndiyo ugonjwa wangu kutoka kwenu nyinyi vipenzi vyangu na jinsi mnavyoweza kuitumia NAZI 🥥 katika mapishi basi swadaktaah
Nadhani Utaniwakilisha vyema


✋✋
 
Kulikuwa na jamaa Yanga ikicheza anaifata popote.. .wakiwa Morogoro na yeye yupo..

Mchepuko wa mkewe ulifaidi sana..
Yanga ikienda Mbeya...jamaa anaenda Zanzibar na mkewe....

Ilikuwa Yanga ikicheza Tu hasa mikoani basi
Na Mke huku anajiachia na jamaa yake..
Mpaka nahama ule mtaa sikumbuki kama jamaa kuna watu walimwambia...
Hamu ya kuishi predictable na mechi za mpira ilinitoka kabisa
 
Kulikuwa na jamaa Yanga ikicheza anaifata popote.. .wakiwa Morogoro na yeye yupo..

Mchepuko wa mkewe ulifaidi sana..
Yanga ikienda Mbeya...jamaa anaenda Zanzibar na mkewe....

Ilikuwa Yanga ikicheza Tu hasa mikoani basi
Na Mke huku anajiachia na jamaa yake..
Mpaka nahama ule mtaa sikumbuki kama jamaa kuna watu walimwambia...
Hamu ya kuishi predictable na mechi za mpira ilinitoka kabisa
🤣🤣🤣ni hatari hiyo
Mimi Sjafikia level za kuondoka na Timu na sitakuja kufikia ushabiki wa namna hiyo labda aisee kipato kikikuwa nitakuwa naondoka mara moja moja kwenda kushuhudia fainali za makombe ya Ulaya lakini uyu mwadada nitaondoka nae 🤣🤣

Uzuri kashazoea si haba kumuona karudi nyumbani na Jersey zimeprintiwa kwa majina yangu as a gift
 
Back
Top Bottom