Hizi ndizo sera ambazo Rais Maguufuli atazitumia 2020 kuingia ikulu

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,602
2,000
Habari wadau!

Zifuatazo ni baadhi ya sera atakazotumia Mh. Rais kuomba ridhaa ya watanzania kuingia ikulu kwa mara nyingine tena;

1. "Ndugu zangu Watanzania nimetumia kipindi changu cha miaka 5 kutengeneza Tanzania iliyoibiwa, iliyoharibika , nchi hii ilioza sana na sasa kazi iliyobaki ni kuleta furaha na maisha mazuri , naomba mnipe kura nikamalizie kazi mliyonituma"

2. "Sakata la makinikia sasa nishalishughulikia na wapo katika hatua za kukamilisha malipo yetu ya matrilioni, naomba nipeni ruhusa ya kumalizia zoezi hili ili wasije watu wasio na uchungu na taifa hili wakaharibu kazi nzuri tuliyoifanya CCM awamu ya 5"

3. "Nimeondoa viongozi wazembe, mafisadi na wala rushwa, sasa nidhamu serikalini imerudi, nimeondoa wafanyakazi hewa maelfu kwa maelfu, nimeondoa wafanyakazi wasio na sifa wenye vyeti feki na sasa kazi iliyobaki ni kuwapa furaha watumishi wa umma nao waache kupanda daladala, waendeshe magari yao, walale kwenye nyumba nzuri."

4. "Tumeshaanza utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge, ujenzi ulisuasua kwakuwa tulikuwa tunatafuta fedha za kukamilisha ujenzi haraka, na nimezipata na natarajia kuanza kujenga kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma haraka mapema mwa mwakani , ndugu zangu nipeni nafasi nimalizie kazi hii "

Hii imekaa kama comedy hivi ila ndivyo itakavyokuwa kama tu Mungu akatupa uzima.
 
Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,817
2,000
Wakati nasoma hapo juu nikakumbuka alivyokuwa anatia huruma...dah!!!
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
19,921
2,000
"Tazara flyover nalo limefikia pazuri, nipeni nafasi nimalizie kazi niliyoianza ya kutokomeza foleni jijini Dar es salaam"
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
Zote ziko sawa pia nyingine ni badala ya PUSH UPS sasa watamuwekea VIFAA VYA GYM JUKWAANI...
 
Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,602
2,000
Atazungumzia ajila alizoziua!!??
Atakachokifanya ni kutangaza ajira kama elfu 50 kwa pamoja hivyo watu watafanya application huku wakisubiri backup ya applications zao wakati wa uchaguzi umewadia.
Ukipita uchaguzi sijui nini kitakachofuata kwa zoezi zima.
 
roboka kafwekamo

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
823
500
Habari wadau!

Zifuatazo ni baadhi ya sera atakazotumia Mh. Rais kuomba ridhaa ya watanzania kuingia ikulu kwa mara nyingine tena;

1. "Ndugu zangu Watanzania nimetumia kipindi changu cha miaka 5 kutengeneza Tanzania iliyoibiwa, iliyoharibika , nchi hii ilioza sana na sasa kazi iliyobaki ni kuleta furaha na maisha mazuri , naomba mnipe kura nikamalizie kazi mliyonituma"

2. "Sakata la makinikia sasa nishalishughulikia na wapo katika hatua za kukamilisha malipo yetu ya matrilioni, naomba nipeni ruhusa ya kumalizia zoezi hili ili wasije watu wasio na uchungu na taifa hili wakaharibu kazi nzuri tuliyoifanya CCM awamu ya 5"

3. "Nimeondoa viongozi wazembe, mafisadi na wala rushwa, sasa nidhamu serikalini imerudi, nimeondoa wafanyakazi hewa maelfu kwa maelfu, nimeondoa wafanyakazi wasio na sifa wenye vyeti feki na sasa kazi iliyobaki ni kuwapa furaha watumishi wa umma nao waache kupanda daladala, waendeshe magari yao, walale kwenye nyumba nzuri."

4. "Tumeshaanza utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge, ujenzi ulisuasua kwakuwa tulikuwa tunatafuta fedha za kukamilisha ujenzi haraka, na nimezipata na natarajia kuanza kujenga kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma haraka mapema mwa mwakani , ndugu zangu nipeni nafasi nimalizie kazi hii "

Hii imekaa kama comedy hivi ila ndivyo itakavyokuwa kama tu Mungu akatupa uzima.
Kisha atasema waliofukuzwa kazi na wote niliowafukuza kwa makosa mbalimbali watpunguza sana kura zangu na watu wanso niunga mkono ni wa vijijini na ndio hukohuko watendaji wabovu waliko jificha makonda na gambo najua watanipunguxia kura lakini nimragiza mabomu ya machozi tume ya uchsguzi nimeipanga upya bunduki na lisasi virungu na tunaendelea kusajiri ffu ili kulazimisha ushindi chezea uone.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom