Hizi ndizo saili zilizoongoza kuwa na waombaji kazi(wasailiwa) wengi kwa nafasi chache tangu nchi hii ipate uhuru

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Sio ubishi tena, Janga la ajira ni changamoto kubwa sana kwa kizazi Cha Sasa . Tujikumbushe kidogo

Tarehe 12/12/2014 ilikuwa ni siku ya usaili ya nafasi za kazi 50 tu zilizotangazwa na TRA takribani mwezi kabla ya tarehe ya usaili., baada ya kufanya short listing wakapatikana watu zaidi ya 10,000+ wenye sifa za kazi na wote wakaitwa kwenye usaili.

Tarehe 13/06/2014 mwaka huohuo uhamiaji walitoa tangazo la nafasi za kazi za watu 70 tu na Baada ya kufanya short listing wakapata pia watu zaidi ya 10,000+ wenye sifa za kufanyiwa usaili na ukafanyika pale uwanja wa taifa, ulituhumiwa kughubikwa na urasimu mwingi sana.

Hizi saili watu wa ndani niliopata kuzungumza nao kwenye hizi taasisi walisema walijatihidi sana kuwaondoa watuma maombi ambao maombi yao yalikuwa na makosa hata yale madogo lakini haikusaidia kupunguza namba ya wingi wa watu.

Baada ya kutokea hivo, naona saili za serikali zimekuja na mikakati mikali sana kwenye Short listing tangu 2015 haya mambo hayawezi kujitokeza tena.

Hizo saili zitabaki historia hapa nchini, na kijana uliyeko chuoni, umehitimu au mtaani yajue haya pambania maisha yako ajira ikukutie buko.

Serikali hizi za Africa hazina Cha kupoteza hata Kama ukizeeka ukiwa huna ajira, pambana uwin maisha yako, Japo ni ngumu sana lakini inawezekana.
 
Vijana wengi wamekata tamaa kuomba nafasi za serikali mtu anasafiri kutoka kigoma anajipinda kufanya mtihani halafu anapewa marks 10.

Anarejea home kesho yake unapata taarifa kuna mtu kapiga oral interview wakati written hakufanya.

Ananyongonyea anajiuliza ile laki 3 aliyoitumia kusafiria kwenda kupata marks 10 angeiwekeza kwenye kuku ingemsaidia.

Yote maisha tu
 
Nilichojifunza watoto tuwaandae kwa maisha nje ya ajira...tusisubiri mfumo uwaandae
Tuchukue nafasi wenyewe kuandaa watoto kiakili
 
Vijana wajiandae namna ya kuishi nje ya mfumo rasmi wa ajira, japo si rahisi ila ndio njia pekee iliyopo.

The hard way, the only way.
 
Tunawaandaaje mkuu wakati mfumo wa elimu hauna uwezo wa kuwafanya angalau wakawa wabunifu? Fafanua kidogo namna ya kuandaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mfumo unabana na ndio hapo na sisi tuwe wabunifu zaidi
Mfano isiwe mtoto shule ndo kila kitu maishani mwake
Ajue vitu km michezo na kazi za nyumbani


Lakini pia kwa zile shughuli tunazofanya wazazi tushirikishe watoto kama wanavyofanya wahindi

Kama una duka auze kama una shamba aende kama una ofisi yako binafsi aje aanze kujua unafanya kazi gani na unampa kidogo kidogo majukumu akikua hutofundisha anajua the game mwanzo mwisho..hata akitaka chake ile spirit ya kujishughulisha tayari anayo..ataweza,.

Kuna dada mmoja huko Insta ni caterer anasomesha binti yake Feza ila anaenda na mtoto kwenye mgahawa wake na anapopanga vyakula vya wateja anaanza kumpa mtoto kazi kidogo kidogo
Mwishowe huyu mtoto atatoka na elimu ya nzuri ya darasani na ni mpishi mbobezi/mfanyabiashara either ataendeleza kazi ya mama au atafungua chake anachopenda
Tuwape watoto uzoefu
 
Back
Top Bottom