Hizi ndizo sababu zinazonifanya nakosa Imani na Serikali ya Kikwete na CCM. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndizo sababu zinazonifanya nakosa Imani na Serikali ya Kikwete na CCM.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtimbwafs, Mar 11, 2011.

 1. m

  mtimbwafs Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wakereketwa na Wananchi wenzangu, ni takribani miaka 5 imepita tangu tulipoahidiwa maisha Bora kwa kila Mtanzania ambayo hatuyaoni hadi sasa, na kibaya zaidi hata yule mwanazuoni aliyetunga slogani hii hana Imani tena na kauli mbiu hii japo imeongezwa neno moja tamu saaaaana na chama hiki kikongwe lisemalo "ZAIDI" yaani MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAPATIKA KWA ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI na KASI ZAIDI. Aaah achana na hizo propaganda hapo juu hebu nami niseme ambacho ninataka kusema ili wenzangu japo mtusaidie mawazo mimi na watoto wa wakulima wenzangu wa taifa hili.

  Haya yafuatayo ni mambo ambayo ni muhimu sana kwangu leo hii ili maisha yeweze kwenda japo si kwa neno ZAIDI ambalo limeongezwa na Wenzetu siku hizi;

  1. UMEME, UMEME, UMEME, UMEME.
  • Kama tujuavyo mimi na wachovu wenzangu wengi tu wa mtaani huwa tunajipatia kipato chetu kwa kuuza BARAFU, ICE CREAM, MAJI BARIDI, JUICE YA MIWA na Maziwa MGANDO huku uswazi kwetu na kwa kweli MUNGU si Athumani mambo madogo madogo yalikuwa hayasumbui ndugu zangu milo miwili ilipatikana na hata pale kwa wenzangu wa sagula sagula nilikuwa naonekana japo mara mbili au tatu hivi kwa mwaka hasa wakati wa sikukuu kama tujuavyo tena hawa watoto wetu wa kisasa akikosa nguo wakati wa sikukuu ananuna na hata kuugua kabisa. Sasa tangu hawa jamaa walipoingia nikasikia neno DOWANS, RICHMOND, IPTL na mambo mengine meengi kadha wa kadha na umeme ukaanza kuporomoka mgao ukawa ndio wimbo wa TAIFA siku hizi barafu hatuuzi tena na kipato changu kimeshuka kama si kuporomoka kabisa kupata hata JERO tu ya kupata hata kakikombe ka LOLIONDO kule kwa babu imekuwa shida na watoto wanataka kula!, ndiyo ni haki yao na narudia tena tuliambiwa na Baba wa Taifa kuwa kila mtu anahitaji mambo matatu ili aishi nayo si ya hiari ni ya lazima CHAKULA, MAVAZI, na MALAZI kwa hiyo watoto wanadai haki yao ya msingi na mimi siwezi hata kuwapa haki yao ya msingi!. JE KWA HILI NINA SABABU YA KUIPENDA CCM na serikali yake tena????.
  • Kodi ambazo siku hizi tunakatwa kwenye umeme wakati wa kwenda kununua LUKU ni kichefuchefu kabisa, mara utasikia hii ni kwa ajili ya EWURA, KODI YA KUPELEKA UMEME VIJIJINI, VAT n.k sasa najiuliza kama sisis tulio na umeme ndio wenye jukumu la kupeleka umeme vijijini TANESCO kazi yake ni nini hasa?. Na kama mimi ndiye ninaetakiwa nilipe hata mshahara na posho za Mkurugenzi na Watendaji wa EWURA kazi ya SERIKALI hii ni nini?. Na je hii VAT ninayoloipa kama haitoshi kufanya mambo yote hayo kazi YA VAT HASA NI NINI?. Aaah nasema tena sina IMANI TENA NA SERIKALI HII!!!!!!!!!!!!. kwa kuwa imekuwa inaninyonya kila siku bila hata kunipa fursa za kupata ili wanyonye tena. Tazama unaenda na shilingi 10,000/= unapata umeme wa 5400/= na 4600/= zote hizi ni kodi hivi huruma ya serikali hii kwangu iko wapi?????.
  2. KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA VS MISHAHARA.
  Mwalimu Nyerere alisema hivi " SUKARI SI MUHIMU KULIKO CHUMVI" na "MAFUTA YA TAA YAKIPANDA ANAEUMIA NI MWANANCHI WA KAWAIDA KABISA KULE KIJIJINI". Je kauli hizi hazina maana siku hizi tena?. Serikali inayojali na kuthamini Rushwa haina huruma kwa wananchi wake hata kidogo, haya ndiyo tunayoyaona leo hii hata kula mkate ni ANASA kwa mtanzania wa leo. KWA HALI HII SIONI SABABU YA KUIPENDA SERIKALI HII.

  3. MAUAJI YA NDUGU ZETU WASIO NA HATIA YANAYOTOKEA SASA PASIPO UWAJIBIKAJI WA WATENDAJI WAZEMBE!.
  • Thamani ya Mtanzania wa leo si ya maana sana kuliko Nyumba, Nguo, Magari n.k. Tumeshuhudia watu wakiuawa ARUSHA, MBAGALA, PEMBA na GONGO LA MBOTO lakini hakuna uwajibikaji wowote zaidi ya kuandaliana ulaji kwa wakubwa na wapambe wao kwa kigezo kuwa NAUNDA TUME mapendekezo ya hiyo tume hayatekelezwi watanzania wanakufa tena hakuna UWAJIBIKAJI kila mtu mjanja na hataki kuwajibika!!!. Wakitokea watetezi wa haki zetu mnasema WAHAINI, WANACHOCHEA Machafuko n.k na wimbo huo unaimbwa hata na wasio na sauti za kuimba kisa WATANZANIA WANASEMA UKWELI hii si haki na sikubaliani nalo hata kidogo.
  SINA IMANI NA KIKWETE NA SERIKALI YAKE sitaki niwachoshe mmeshasikia mengi sana wadau lakini huu ni mtazmo wangu tu!.
   
Loading...