Hizi ndizo sababu za CCM kuendelea kutawala Tanzania

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Salam wakuu,asubuhi iwe njema kwenu. Nami pia sijambo.

Baada tu ya Rais Magufuli kuingia darasani, vyama vya upinzani ni kama vimepoteza mwelekeo au pengine kuzimwa kabisa kistrategies. Rais Magufuli anaonekana kuwaweza hawa jamaa sana. Kelele zote kimya.

NCCR Mageuzi. James Mbatia (mama Tanzania) kapotea kabisa,haieleweki alipo, wanachama wake wanahamia CCM kila leo. Yeye amebaki kukaa kimya tu.Hana mpango mkakati wowote.

NLD. Baada tu ya Dk Emmanuel Makaidi kufariki dunia, chama hiki kimedondoka chini kabisa kwenye ulingo wa siasa.Hata mwenyekiti wake na viongozi wake sijui wako wapi.Kimya kabisa.

CUF. Kila siku migogoro isiyoisha,na wala hakuna mwelekeo wa kuzika tofauti zao.Maalim Seif Mbabe, Prof Lipumba komandoo.Sasa hawa nao hawajatulia kabisa.

CHADEMA. Wale makamanda wote tuliokuwa tunawategemea ; Sugu, Mdee, Mnyika, Ester Bulaya, Benson Kigaiya, John Mrema, Godlbless Lema, Joshua Nasari, Ezekiel Wenje, Msigwa, Mh Mbowe na wengineo wote wamekabwa koo, hawafurukuti kabisa.Hawana hoja , wapo kimya kabisa.Maana ake wanakubaliana na kinachoendelea.

ACT Wazalendo. Hawa bado wanakua kwanza. Masikio hayawezi kuzidi kichwa.

Hashimu Rungwe bado kabisa.

Ushauri: Hawa jamaa hawawezi kuungana wakawa na kitu strong kweli?Maana watapambana lakini hawatashinda.

Asante
 
Bila shaka wewe ni Lizabon au Barbarosa umekuja kwa ID nyingne upinzani upo vizuri kijana tena wapinzani wanamdondosha pombe mapema sana kama NEC ikiwa fair kwani huyo Pombe amefanya kipi cha kujivunia watanzania au huo ununuz wa ndege,
 
Unazidi tu kuuthibitishia ulimwengu jinsi taifa letu lilivoangukia mikononi mwa dikteta uchwara asiyejua utawala wa sheria wala kuheshimu katiba ya nchi iliyomwezesha kuingia madarakani. Nchi inaendeshwa kifashisti kama vile bado tupo karne za mawe ambapo akili haitumiki bali nguvu.

Kwamba unaweza kusifia hali hiyo isiyoonesha chembe cha ustaarabu ni kwamba taifa linaendeshwa kibashitebashie kama gari bovu mikononi mwa dereva mlevi. Fikiria zama hizi jiji kubwa kama Dar kuwa chini ya mhuni na mlevi wa madaraka ambaye sifa kuu aliyo nayo ni kughushi vyeti...je Hivi punde niendelee?
 
Umesema unaitwa Hivi punde !!?

CCM inatawala kwa sababu ya u dictator wa kutumia vyombo vya dola kunyanyasa wapinzani wake, Zanzibar CCM imeshindwa mchana kweupe lakini hawakufanya uungwana wa kukabidhi madaraka , je kwa hapo wapinzani unawalaumu vipi badala ya kuwapongeza kwa kuacha kufanya vurugu ili wakabidhiwe madaraka. CCM ikiacha tu kujiegemeza kwenye vyombo vya dola na kuwa kama vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii hata kwa sekunde
 
Bila shaka wewe ni Lizabon au Barbarosa umekuja kwa ID nyingne upinzani upo vizuri kijana tena wapinzani wanamdondosha pombe mapema sana kama NEC ikiwa fair kwani huyo Pombe amefanya kipi cha kujivunia watanzania au huo ununuz wa ndege,

Amefanya mengi sana moja wapo ni kukamata wapinzani na kuwaweka mahabusu,kumkingia kifua mwizi wa vyeti na jambazi la kutumia silaha aka Bashite
 
Mkuu uje hapa uchukue coke baridi maana CCM ni sawa na wachawi ubaya wanasema uzuri na uzuri wanasema uzuri
 
CHADEMA sasa ni pori(siyo kichata tena) la wahalifu(mafisadi, wabwia Unga, wakwepa kodi) kujificha
 
"You will not attain righteousness until you spend in charity of the things you love."

- Qur'an (Surah Al-Imran, Ayah 92)
 
Salam wakuu,asubuhi iwe njema kwenu. Nami pia sijambo.

Baada tu ya Rais Magufuli kuingia darasani, vyama vya upinzani ni kama vimepoteza mwelekeo au pengine kuzimwa kabisa kistrategies. Rais Magufuli anaonekana kuwaweza hawa jamaa sana. Kelele zote kimya.

NCCR Mageuzi. James Mbatia (mama Tanzania) kapotea kabisa,haieleweki alipo, wanachama wake wanahamia CCM kila leo. Yeye amebaki kukaa kimya tu.Hana mpango mkakati wowote.

NLD. Baada tu ya Dk Emmanuel Makaidi kufariki dunia, chama hiki kimedondoka chini kabisa kwenye ulingo wa siasa.Hata mwenyekiti wake na viongozi wake sijui wako wapi.Kimya kabisa.

CUF. Kila siku migogoro isiyoisha,na wala hakuna mwelekeo wa kuzika tofauti zao.Maalim Seif Mbabe, Prof Lipumba komandoo.Sasa hawa nao hawajatulia kabisa.

CHADEMA. Wale makamanda wote tuliokuwa tunawategemea ; Sugu, Mdee, Mnyika, Ester Bulaya, Benson Kigaiya, John Mrema, Godlbless Lema, Joshua Nasari, Ezekiel Wenje, Msigwa, Mh Mbowe na wengineo wote wamekabwa koo, hawafurukuti kabisa.Hawana hoja , wapo kimya kabisa.Maana ake wanakubaliana na kinachoendelea.

ACT Wazalendo. Hawa bado wanakua kwanza. Masikio hayawezi kuzidi kichwa.

Hashimu Rungwe bado kabisa.

Ushauri: Hawa jamaa hawawezi kuungana wakawa na kitu strong kweli?Maana watapambana lakini hawatashinda.

Asante
Kwa mtazamo wangu hypothetically, Upinzani hata kama wakiungana. Tundu Lisu+Mbowe+ Lowassa&Co.+Nani sijui. Magufuli BADO atawaangusha vibaya sana 2020.

Maana hawana AJENDA ya kubadilisha maisha ya Watanzania.Badala ya kufocus kwenye issues za maana na changamoto zinazowakabili Watanzania wao upinzani, WAMEBAKI kwenye PERSONALITIES Oh! Magufuli hivi Oh! Magufuli vile Oh! kavaa kakaribisha nani.
Just dwelling on TRIVIALITIES!!
Hawatawaweza CCM.
 
Bila shaka wewe ni Lizabon au Barbarosa umekuja kwa ID nyingne upinzani upo vizuri kijana tena wapinzani wanamdondosha pombe mapema sana kama NEC ikiwa fair kwani huyo Pombe amefanya kipi cha kujivunia watanzania au huo ununuz wa ndege,
Hata wakoloni walileta treni
 
Back
Top Bottom