Hizi ndizo sababu kuu mbili zinazo sababisha umasikini tanzania na afrika kwa ujumla

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
671
HIZI NDIZO SABABU KUU MBILI ZINAZO SABABISHA UMASIKINI TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA

1:UDHAIFU WA ELIMU YETU. Elimu yetu haijitosherezi wala haiendani na dunia tuliyo nayo leo tofauti na mataifa mengine kama uingereza, marekani, Canada n.k

Mfano mwanafunzi Alie Soma kombi ya hgk/hgl/hkl kwa level ya kidato Cha sita unaweza kunambia ni kitu gani ambacho mwanafunzi huyu anakua ametoka nacho shuleni ambacho kinaweza msaidia kuja kutatua changamoto za mtaani?

Just imagine mwanafunzi alie Soma history anatoka shulen akiwa anafaham mambo yaliyo tokea nyuma miaka 70 iliyo pita; mfano vita vya Kwanza ya dunia, anguko la uchumi wa dunia.
Sasa ashumu mtoto anatoka shuleni amekalili mambo ya miaka 70 nyuma, mtoto anatoka shuleni anajua mambo ya kuandika insha, kujitambulisha, kutafasiri maneno na namna ya kuwasiliana ( IELTS) kwenye language.

Ukija kwenye geography mtoto anakuja kasoma mambo ya ma barafu kama topic, ukiangalia barafu tunazo zisoma zinapafikana nchi za wenzetu canada,USA n.k Sasa hapa unategemea lini Africa tutajikomboa kwenye dhahama ya umasikini!?
Just imagine msomi mwenye level ya form 6 anakuja nyumban kichwani akiwa amebeba 85% ya mambo ambayo hayana impact kwenye suala la kujikwamua kiuchumi!! Shame

Viongozi tunao waona leo ni zao la elimu yetu kwa aslimia kubwa, labda ukitoa elimu za juu walizo kwenda kupata huko ughaibuni.

Ushauri wangu kwenye suala la elimu, Tanzania tunahaja ya kuireform elimu yetu tusiendelee na elimu ya kukalili kujibu mitihani, Tunahitaji elimu ya kuweza kutatua changamoto tulizo nazo,

Wanafunzi wasome kama ni mambo ya kilimo, ufugaji uvumbuzi ingali wakiwa vidudu, wasome namna ya kutumia vyanzo vyetu vya maji katika kukuza secta ya kilimo kuanzia vidudu mpaka vyuoni,

Wasome namna ya kutumia kilimo chetu kulingana na mazingira ya kila kanda, huwezi amini wavyetinam walikuja Tanzania kujifunza kilimo Cha alizeti, lakin leo sisi ndio tunaagiza mafuta ya kula kwa wanafunzi wetu na alizeti yetu haina ubora tena,. inaumiza Sana.

Kama ni ufungaji wajifunze ufugaji unao patikana kwenye taifa letu na namna ya kutumia,

Tuache kukalili ufugaji ambao unapatikana ulaya na marekani afu mwanafunzi anaenda kujibia mtihani huu ni ujinga kwa Africa nzima.

inasemekana kwasasa kuna hatari ya kupoteza kuku asilia kutokana nakukosa ubora yaan wanakua wadogo na si wazito hivyo hukosa sifa katika soko la biashara, lakin kumbe kuku wa kitanzania akifungwa vizuri anauwezo wa kufikisha mpaka kilo 4) ila mtoto anamaliza form 6 hajui hata namna ya kufunga kuku afu Wana siasa wanao kula mshahara wa zaid ya 11ml anakuja anakwambia watoto wajiajiri, hawa ni wajinga walio zalishwa na elimu yetu.

2: SIASA NA WANASIASA.(mfumo wa utawala na viongozi)

Tukatae tukubali kalibu 98% za hatima ya maisha yetu hasa ki uchumi huamuliwa na wanasiasa kwakua wao ndo hutunga sera zote za maendeleo ya taifa.

Kama nilivyo sema kwenye hoja ya elimu viongozi tulio nao Leo ni zao la elimu yetu hii tuliyo achiwa na mkoloni ambayo ni duni na haitoi hatima ya kujikomboa kama taifa.

Imekua kawaida Sana kuwa na wanasiasa ambao hawana vision kwa taifa lao wala mikakati maarumu ya kiukombozi kwa taifa letu.

Viongozi walio bahatika kupata elimu za juu, huja na maneno ya ki ulaghai, na kuwaaminisha watu kua uzalendo ni kuhakikisha unapambania chama kubaki madalakan, na kwa bahati mbaya wamefanikiwa pakubwa kutuaminisha hivyo kwa maslahi yao wenyewe.

Sisi kama taifa tunaongozwa na maono ya mtu mmoja, katiba yetu ya Tanzania imempa mamlaka makubwa Sana kiongozi wetu mkuu wa nchi yeye ndo muamzi wa kila kitu, mfumo wetu wa utawala na uongozi ni mmbovu kuanzia ngazi ya chama mpaka serikali, katika chama silaumu Sana maana mfumo unaminufaisha chama na wala sio taifa.

Yaan kwamba rais anakua mwenyekiti wa chama na Bado ni kiongozi wa taifa na ni amiri jeshi mkuu.

Katiba yetu inampa kiongozi wa nchi mamlaka makubwa na kuwekewa kinga, huu ni udhaifu kama taifa. Kwakua muwekezaji anauwezo wa musoma katiba yetu leo na sheria zetu za nchi akagundua udhaifu wetu kama nchi upo wapi na ni sehem gani pa kupitia.

Mfano mwekezaji akipitia katiba sheria zetu akagundua udhaifu wetu sisi ni kutoa mamlaka yote kwa rais na kumpa kinga, yeye atawaza namna ya ku deal na rais akimuweza rais ujue ameweza taifa.

Yatatokea yale ya kiongozi mmoja aliye kuja na sera za ubinafshaji, kwenye mgodi wa geita Tanzania ikawa inachukua 3%, kampuni GGM 70% zileeeee 27 utajua mwenyewe aliye kua anazichukua..

Just imagine yaan taifa linapata 3% kweli!!???? Shame
Hapa kama taifa ndipo kuna udhaifu.

Ushauri wangu kwenye inshu ya siasa

Sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu maamuzi yetu ni hatima ya taifa letu, tunawajibu wa kuyatafakari maisha yetu na haya ya wana siasa, tuna wajibu wa kutuliza akili na kukuunga mkono kila mwenye hoja ambayo unaona utalikomboa taifa, tukubari tuwe na katiba mpya
 
Haya Mambo muhimu Sana, huwa nafikiria Sana nakosa sababu ya sisi kurundika masomo yasiyo na faida.

Utakuta kijana kasoma PCM ila hajui hata kusuka mota au hata kuunda inverter tu.


Mtu kasomea uchumi na huo uchumi anakaririshwa theories nyingi ambazo haziendani na mazingira yetu.

Ni aibu na kukosa maarifa mpaka Sasa tunategemea mvua ya Mwenyezi Mungu na jembe lilitobolewa kuwekea mpini.


Elimu duni yetu ndiyo inapelekea ongezeko la ukosefu wa ajira. Unasoma sekondari masomo Hadi 11, ambayo mengi hayana umuhimu wowote.

Elimu hii mbovu Sana.

Naunga mkono hoja
 
Haya Mambo muhimu Sana, huwa nafikiria Sana nakosa sababu ya sisi kurundika masomo yasiyo na faida.

Utakuta kijana kasoma PCM ila hajui hata kusuka mota au hata kuunda inverter tu.


Mtu kasomea uchumi na huo uchumi anakaririshwa theories nyingi ambazo haziendani na mazingira yetu.

Ni aibu na kukosa maarifa mpaka Sasa tunategemea mvua ya Mwenyezi Mungu na jembe lilitobolewa kuwekea mpini.


Elimu duni yetu ndiyo inapelekea ongezeko la ukosefu wa ajira. Unasoma sekondari masomo Hadi 11, ambayo mengi hayana umuhimu wowote.

Elimu hii mbovu Sana.

Naunga mkono hoja
Inatia hasira Sana ukitafakari mambo kama haya aisee, ni aibu kua na bara tajiri wakati watu wake ni maskini
 
Back
Top Bottom