Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
WAKATI ambapo uchumi wa Afrika unakua kwa kasi duniani ukitegemea zaidi uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, lakini hali ya uchumi kwa wananchi katika mataifa yanayozalisha nishati hizo barani humo umeacha ombwe kubwa, FikraPevu inaripoti.
Ingawa kuna nchi nyingi ambazo zinazalisha mafuta, lakini ni nchi 19 ambazo ni wazalishaji wa uhakika wa mafuta pamoja na gesi ambazo vinara wao ni nchi sita ambazo ni Nigeria, Libya, Algeria, Angola (mafuta), Sudan (mafuta) na Misri (gesi), rasilimali ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa mataifa hayo.
Takwimu zilizotolewa na taasisi ya US Energy Information Administration (EIA) tangu mwaka 2010, zinaonyesha kwamba nchi 16 kati ya 54 za Afrika zinasafirisha mafuta, ambazo ni Nigeria, Angola, Libya, Algeria, Sudan, Sudan Kusini, Guinea ya Ikweta, Congo (Brazzaville), Gabon, Chad, Misri, Tunisia, Cameroon, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mauritania.
ZAIDI...