Uchaguzi 2020 Hizi ndizo hoja zitakazomuangusha Dkt. Magufuli na kumpaisha Tundu Lissu kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Mkuu bado una uchungu wa tonge kuondolewa mdomoni. JPM hana mpinzani, you know it and your friends know it. Mjiliwaze tu, bado wiki 2 na siku mbili mtalikimbia jukwaa hili. JPM moto wa kuotea mbali! Remember my words!
 
13 Oct 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania

CHADEMA Kampeni za Uchaguzi mkuu 2020
Msafara wa mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chadema, Mh. Salum Mwalimu wasimamisha shughuli Tunduma. Aomba kura kwa madiwani, mbunge na Tundu Lissu


Serikali ya CHADEMA imeendelea kuahidi
Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ili waTanzania wote wawe na uhakika wa kujiendeleza ktk maisha yao binafsi na ya katika maeneo yao kwani hili halihitaji matamko yote yatoke kwa mtu mmoja anayeendesha serikali Kuu iliyo mbali kule Dodoma au Dar es Salaam.
 
Magufuli ameilaumu serikali iliyopita ya Magufuli kwa kushindwa kuwapatia vijana ajira hivyo atahakikisha serikali yake inawapa vijana ajira za kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali ya Magufuli ndio kinara wa kuchota fedha za wastaafu kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii na afya. Mpaka sasa serikali iimekomba jumla ya Tsh Trilioni 1.6 , zikiwemo Tsh Bilioni 44.29 kutoka NHIF ambazo CCM ilichota kwa ajili ya kujengea chuo cha Kata (UDOM) na mpaka leo pesa hizo hazijarejeshwa kwa wenyeywe (wastaafu). Na hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya Magufuli na CCM yake kutunga sheria inayowapora wastaafu mafao yao yote na kuondoa fao la kujitoa kwani mifuko ilikuwa haiwezi kujiendesha tena. Ndipo wakaja na ujanja wa kuunganisha mifuko ili wapate kisingizio cha kufunika UFISADI wao. Mh Tundu Antipas ataondoa uporaji huu kwani anawathamini mno wafanyakazi wa nchi hii. Atahakikisha fedha zilizoporwa na Magufuli zinarudi kwa wastaafu.
 
Serikali ya Magufuli ndio kinara wa kuchota fedha za wastaafu kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii na afya. Mpaka sasa serikali iimekomba jumla ya Tsh Trilioni 1.6 , zikiwemo Tsh Bilioni 44.29 kutoka NHIF ambazo CCM ilichota kwa ajili ya kujengea chuo cha Kata (UDOM) na mpaka leo pesa hizo hazijarejeshwa kwa wenyeywe (wastaafu). Na hii ndio ilikuwa sababu kubwa ya Magufuli na CCM yake kutunga sheria inayowapora wastaafu mafao yao yote na kuondoa fao la kujitoa kwani mifuko ilikuwa haiwezi kujiendesha tena. Ndipo wakaja na ujanja wa kuunganisha mifuko ili wapate kisingizio cha kufunika UFISADI wao. Mh Tundu Antipas ataondoa uporaji huu kwani anawathamini mno wafanyakazi wa nchi hii. Atahakikisha fedha zilizoporwa na Magufuli zinarudi kwa wastaafu.
Pesa zipo lazima CCM waendelee kuchota na hatutaacha leo wala kesho. Lazima tuwashikishe adabu!
 
13 Oct 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania

CHADEMA Kampeni za Uchaguzi mkuu 2020
Msafara wa mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chadema, Mh. Salum Mwalimu wasimamisha shughuli Tunduma. Aomba kura kwa madiwani, mbunge na Tundu Lissu


Serikali ya CHADEMA imeendelea kuahidi
Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ili waTanzania wote wawe na uhakika wa kujiendeleza ktk maisha yao binafsi na ya katika maeneo yao kwani hili halihitaji matamko yote yatoke kwa mtu mmoja anayeendesha serikali Kuu iliyo mbali kule Dodoma au Dar es Salaam.

Mmeshindwa maendeleo ndani ya chama chenu mtaweza maendeleo ya Watanzania na uhuru wao?
1602620522713.png


Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, naingia kwenye mada moja kwa moja. Katika andiko hili nimebainisha kinagaubaga mambo ambayo yatamuangusha Magufuli na kumuinua Hon Dr Tundu Antipas Lissu kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 kama ifuatavyo:

1. Kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi
Mh Dr Lissu amebainisha wazi kwamba ndani ya siku 100 za kwanza za uongozi wake atawapandisha wafanyakazi madaraja, atawapa nyongeza ya mishahara, na kila mwaka atakuwa anawaongeza mshahara (statutory annual increament) kwa mujibu wa sheria.

Kama mnavyojua Rais Magufuli hajawahi kuwaongeza mishahara wafanyakazi kwa muda wa miaka 5 iliyopita na huwa hazingatii kuwapandisha madaraja kila baada ya miaka 3 kama sheria inavyosema. Katika utawala wake tumeshuhudia watumishi wa umma wakikaa miaka zaidi ya 8 bila kupandishwa madaraja, huku akijua fika kwamba jambo hili linawaumiza sana wafanyakazi pamoja na wategemezi wao. Wafanyakazi na wategemezi wao (idadi yao si haba) wana uchungu sana na Magufuli, hivyo wanaona kimbilio lao la uhakika ni Hon Dr Tundu Lissu.

2. Kufuta kikotoo dhulumishi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, serikali ya Magufuli, iliamua kufuta fao la kujitoa na kuja na kanuni (kikokotoo) ya ajabu katika kukokotoa mafao ya wafanyakazi. Sababu ya kufanya hivyo iko wazi kwa kila mtanzania mwenye akili timilifu. Serikali imeifilisi mifuko hii kwa kuifanya Shamba la Bibi. Serikali wamekomba fedha zote kwenye mifuko hii na kuifilisi kabisa. Hon Tundu Lissu ameahidi atakapoingia madarakani ataifutilia mbali sheria hii kandamizi inayowadhulumu wafanyakazi mafao yao. Inasikitisha athari za ufilisi huu uliosababishwa na serikali ya Magufuli umepelekea wastaafu watarajiwa kuishi kwa kihoro pasipokujua hatima ya jasho lao walilolipigania kwa zaidi ya miaka 40 ya kuitumikia serikali kwa uaminifu.

3. Kurejesha Uhuru wa kujieleza, mahakama, polisi, nk.
Hakuna mtu asiyefahamu kwamba serikali ya Magufuli imeminya na kukandamiza demokrasia, uhuru wa kujieleza pamoja na uhuru wa vyombo vya habari kwa muda wote wa miaka 5 aliyokaa madarakani. Pamoja na ukweli kuwa serikali ya CCM imekuwa ikiwatumia polisi kama tawi la CCM kwa muda mrefu, serikali ya Magufuli imekithiri katika matumizi ya polisi kuminya upinzani na kuwakandamiza raia wasiokuwa na hatia.

Rais Tundu Antipas Lissu atarejesha demokrasia, uhuru wa habari pamoja kuacha matumizi ya polisi kuisaidia Serikali yake. Jeshi la polisi litakuwa huru na litafanya kazi zake kwa weledi bila kuegemea upande wowote wa kisiasa. Tukumbuke sera ya CHADEMA ni ‘Uhuru na Maendeleo’. CCM kwa sasa hawana sera yoyote. Chini ya Uongozi wa Tundu Lissu wananchi watakuwa huru ktk nchi yao bila wasiwasi wa kutekwa na watu wasiojulikana.

4. Kubomoa flyovers na kujenga feeder roads
Hizi flyovers za serikali ya Magufuli zinazopigiwa chapuo kila kukicha zimeshindwa kabisa kutatua tatizo la foleni jijini Dar es Salaam. Kila mkazi wa Dar anayepita kwenye hizi flyovers ni shahidi. Tatizo la foleni bado lipo palepale.

Serikali ya Tundu Lissu itajikita zaidi kwenye ujenzi wa njia za pembezoni (feeder roads) ili kupunguza wingi wa magari kwenye barabara kuu. Wingi wa magari ukipungua kwenye main roads msongamano utakwisha na tatizo la foleni jijini Dar litabaki historia.

5. Kurejesha uhusiano wa kimataifa
Uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine ya nje ya Afrika umekufa kifo cha mende. Na jambo hili limefanywa kwa makusudi na serikali ya Magufuli kwa kuwatukana wazungu kila siku huku akiwabatiza majina ya ajabu ajabu kama vile mabeberu, mashoga, nk. Imefikia hatua hata watalii wanaotamani kutembelea vivutio vya utalii nchini Tanzania baadhi yao wameamua kwenda Kenya na nchi nyingine zinazowathamini.

Dunia ni moja. Hakuna haja ya kubaguana kwa misingi ya rangi na kubatizaba majina ya ajabu ajabu. Mh Tundu Lissu atarejesha uhusiano na mataifa ya nje na atashirikiana nao bega bega kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu. Huwezi kuwatukana watu mabeberu huku ukiwategemea kuchangia zaidi ya 40% ya bajeti ya serikali. Haiwezekani.

6. Kuondoa ubaguzi wa kijimbo
Ijapokuwa serikali ya Tundu Lissu itakuwa ya majimbo, hataruhusu watanzania kubaguliwa kwa misingi ya majimbo yao. Tumemsikia Magufuli akitamka hadharani wakati wa kampeni kuwa ikiwa wapiga kura watamchagua mpinzani, hawezi kamwe kuwapelekea maendeleo. Utadhani hayo maendeleo anayapeleka kwa fedha zake za mfukoni wakati anatumia kodi za watanzania wote.

Mh Tundu Lissu ataondoa ubaguzi wa aina hii. Ameahidi kutopendelea wananchi kwa misingi ya kisiasa kwa kuwa maendeleo hayana chama. Ukiwa na rais mbaguzi kama Magufuli, nchi hii haitakaa ipate maendeleo kamwe.


7. Kuongoza nchi kwa mujibu wa sheria badala ya matamko
Katika awamu hii tumeshuhudia nchi ikiongozwa kwa matamko na bila kuzingatia sheria za nchi kwa miaka 5 mfululizo. Tumeshuhudia ndege zikinunuliwa na uwanja wa ndege kujengwa Chato bila fedha zake kuidhinishwa na bunge, ambacho ndicho chombo kinachowawakilisha wananchi. Aidha, fedha za umma
Tsh Trillion 1.5 zimepotea katika mazingira ya kifisadi na mpaka sasa hazijatolewa melezo yoyote.

Mh Tundu Antipas ameapa kuongoza kwa kufuata misingi ya sheria endapo atachaguliwa kuwa Rais. Na hiki ndicho watanzania wengi wanachokitaka kwa kuwa wamechoshwa kuburuzwa na Jeshi la Mtu Mmoja miaka nenda miaka rudi. Mtu huwezi kuongoza nchi kama vile unaongoza familia yako. Haiwezekani.


Kwa hoja hizi, mpeni Tundu Lissu nchi asubuhi na mapema kabisa kabla jua halijachomoza. Tundu Lissu ataingia ndani ya Ikulu ya Chamwimo jijini Dodoma kabla ya misa ya kwanza.

Mungu mbariki Tundu Lissu, Mungu ibariki Tanzania. Amina.
Good thinking
 
Ndugu yangu hizi flyovers zimetumia fedha nyingi za walipa kodi wa nchi hii lakini zimeshindwa kuleta ahueni ya foleni. Ni bora zipigwe nyundo na kujenga feeder roads. Duniani kote flyovers hazijawhi kutatua tatizo la foleni ndugu yangu. Fanya utafiti utaona ninachokuambia Ukibomoa hiz
 
Uchambuzi wa kina kwanini ilani ya CHADEMA imeeleweka vyema na kukubalika, mapungufu ya ilani CCM Mpya ni yepi


Source : Swahili Villa
  1. Wananchi wakisabahiana huuliza hali zao za kiuchumi yaani Maendeleo binafsi (watu), furaha, haki zao, uchumi, afya n.k na siyo kuulizana umeona madaraja, ndege au flyover au daraja la baharini
  2. CHADEMA wameonesha kuwa wao ni watetezi au watakuwa wawakilishi wa kweli wa wananchi kwa kile walikuwa wanataka kukisema ndani ya miaka mitano iliyopita lakini walizuiliwa
  3. CHADEMA wamefanikiwa kuugeuza uchaguzi huu mbali ya kuwa ni uchaguzi Mkuu lakini ni wakati wa wananchi pia kuonesha hisia zao kama vile ni kura ya maoni dhidi ya CCM Mpya
  4. CHADEMA wana nidhamu ya kisiasa kutetea bila kuonekana wakipingana na wanachoamini
  5. CCM Mpya hawana nidhamu ya kampeni leo wanasema wanajali wanyonge kesho yake wanatishia wapiga kura kuwa wasipoipigia kura hawatawaletea maji
  6. CHADEMA kampeni zao zimefanikiwa kuunganisha kuongeza (+) na kuzidisha mara kadhaa (X) watu wawapigie kura
  7. CCM Mpya kampeni zao ni bila kujijua wanapunguza (-) na kuwagawa au kupunguza wapiga kura(/)
  8. CCM Mpya mgombea wao wa urais ameshindwa kuelezea na kushawishi baada ya anayoita mafanikio ya Maendeleo ya Vitu , miaka mitano mingine ataweka mazingira gani kufanikisha kiu ya waTanzania kurejeshewa uhuru, haki na Maendeleo binafsi (Watu)
  9. Mgombea wa CHADEMA amefanikiwa kuwashawishi kuwa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ndiyo kinachotakiwa na kuwa Maendeleo ya Vitu ni kitu cha kawaida kila serikali inatakiwa kufanya bila kuathiri au kubinya Uhuru, Haki na Maendeleo binafsi (watu)
  10. Kinamama wameonesha kumuamini mgombea wa CHADEMA wakati mgombea wa CCM Mpya anaonekana kuzidi kuwa kera na kuwanyanyapaa wanawake kwa muonekano wao, kutishia kuwapiga virungu mashangazi wanaodai pesa za korosho n.k
  11. WaTanzania hawavutiwi na hoja kuwa Tanzania imekuwa kama ulaya kwa madaraja ya baharini, flyovers, SGR inayojengwa wakati kipau mbele chao ni mahitaji yao wanayoona muhimu katika maeneo yao mfano maji, Walimu zaidi ktk shule, fedha kutokana na shughuli zao za kiuchumi, madawa / vifaa tiba / wafanyakazi zaidi sekta ya afya katika wilaya zao
  12. n.k
medium.com › one-of-my-political-...
One of my political mentors used to say that politics is a game of addition, not ...

3 Jan 2019 — One of my political mentors used to say that politics is a game of addition, not subtraction. It still amszes me how some activists treat their politics
Source : swahili villa


Anazidi kujichanganya mgombea wa urais 2020 kupitia tiketi ya CCM Mpya John Magufuli

 
13 Oct 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania

CHADEMA Kampeni za Uchaguzi mkuu 2020
Msafara wa mgombea mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chadema, Mh. Salum Mwalimu wasimamisha shughuli Tunduma. Aomba kura kwa madiwani, mbunge na Tundu Lissu


Serikali ya CHADEMA imeendelea kuahidi
Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu ili waTanzania wote wawe na uhakika wa kujiendeleza ktk maisha yao binafsi na ya katika maeneo yao kwani hili halihitaji matamko yote yatoke kwa mtu mmoja anayeendesha serikali Kuu iliyo mbali kule Dodoma au Dar es Salaam.

Magufuli na CCM yake kama wanaendelea kudharau na kupuuza hii movement ya CHADEMA wanajidanganya sana!!!
Mambo yote 28 Okt,2020.
 
Nitawashangaa sana watumishi wa umma watakaompa kura magufuli pamoja na kuwanyanyasa kwa miaka 5 kwa kutowaongeza mishahara na kuwapandisha vyeo, hivyo kuathiri maisha yao na familia zao kwa ujumla. Sijawahi kuona utawala wa kiimla na kandamizi na dhulumishi kwa watumishi wa umma kama huu wa awamu hii ya giza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom