Hizi ndizo faida kuntu za kuwepo shetani na ibilisi duniani

Kwanza shetani ni an illusion tu, ila uwepo wa dhana hiyo ni fursa na faida kubwa.
Naomba ututhibitishie ukweli wa kauli yako hii.
Shetani hana watetezi, wala hajawahi kujigamba wala kujitetea sehemu... lakini Mungu katumia timu na nguvu nyingi mno kumchafua/kumshusha shetani na bado anadunda!
Hivi ujasiri wa kuandika juu ya mambo msiyo yajua huwa mnaupata wapi ?

Sababu ya Shetani kulaaniwa na kutolewa peponi ni Kiburi chake kwa kujiona yeye ni bora sana kuliko Mwanadamu.

Pili, Shetani baada ya kujigamba hakuomba Msamaha kama alivyofanya baba yetu Adamu. Bali aliomba moja tu toka kwa Mola wake muumba ya kupewa umri mrefu wa kuishi hapa duniani. Shetani ni miongoni mwa viumbe wa mwisho kabisa kufa.

Tatu, Mola wetu ni muweza wa kila kitu, anapotaka jambo liwe basi linakuwa tu, kwahiyo unaposema ametumia nguvu nyingi hali ya kuwa yeye akitaka jambo liwe linakuwa tu. Hapa unatakiwa utupe ushahidi wa hilo.

Nne, kuendelea kudunda kwa Shetani ni baada ya ombi lake kukubaliwa na Mola, na anadunda sababu Allah aliye juu ametaka adunde.
 
Binafsi siamini kama kuna kiumbe wa kuitwa shetani. Shetani ni imaginary character aliyetengenezwa na binadamu ili yeye (binadamu) apate uwezo wa kukwepa kuwajibika kwa makosa yake mwenyewe.
Ukiweza kuthibitisha ukweli wa hiki ulichokiansdika, mimi naacha kutumia hii ID.

Vipi uwe na Imani ambayo haijajengeka katika hakika zaidi ya dhana, kisha kwa imani yako hiyo unahitimisha juu ya jambo lenye uhalisia. Haya ni matumizi mabaya ya akili.
 
(ii) KUSINGEKUWEPO NA MITUME WALA MANABII
Ibilisi/shetani ndiye aliyesababisha manabii na mitume waletwe duniani ili kuja kupambana na ibilisi. Bila ya kuwepo kwa Ibilisi kulikuwa hakuna haja yoyote ya kuletwa kwa mitume na manabii dunia. Wangekuja kufanya nini?
Huu UONGI wa wazi kabisa. Sababu ya kuja kwa mitume na manabii ni baada ya watu kuanza kufanya shirki. Muda ambao Shetani alikuwepo tayari na laana ilikuwa imeshamfikia.

Lakini msilolijua ni kuwa Shetani alikuwa mja mwema na aliwekwa katika kundi moja na Malaika. Lakini kwa kiburi na ujinga wake akaasi.

MWISHO
Ibilisi ni dude lililomshinda Mungu na akaamua kuwasukumia binadamu.
Vipi muumba ashindwe na alicho kiumba ?

Pili, hitimisho lako linahitaji sana ushahidi kuliko uwepo wa mada yako yenyewe.
(vii) KUUMBWA KWA PEPO NA JEHANAMU
Ebu fikiria kama ibilisi asingekuwepo Mungu angeanzia wapi kuumba pepo na jehanamu? Ibilisi ndiye kamsukuma Mungu atengeneze vitu hivyo ili kama ukimfuata shetani mwisho wa siku uchomwe moto.
Nimecheka sana. Pepo na Moto vipo hata kabla ya Shetani kuwepo.

Shetani pale alipo muasi Allah aliye juu, alikuwa yupo peponi. Sasa unapo tuandikia uongo sijui kama unakijua unacho kiandika au la ?

Viumbe wa mwisho kuumbwa ni Majini na Binadamu, bali wa mwishi kabisa ni Binadamu. Maana yake kabla ya Shetani na sisi kuumbwa, pepo na Moto vilikuwepo kitambo sana.

Hizo nukta nyingine nilizo ziacha ni nyepesi sana, mpaka napata uvivu wa kukujibu.
 
Hivi ujasiri wa kuandika juu ya mambo msiyo yajua huwa mnaupata wapi ?

Sababu ya Shetani kulaaniwa na kutolewa peponi ni Kiburi chake kwa kujiona yeye ni bora sana kuliko Mwanadamu.

Nne, kuendelea kudunda kwa Shetani ni baada ya ombi lake kukubaliwa na Mola, na anadunda sababu Allah aliye juu ametaka adunde.

Kwa kujibu hoja yako hapo juu, kwanza shetani alikuwa level za malaika hivyo hakuwahi kujilinganisha ubora wake na mwanadamu.

Pia, hicho unachokisema kuwa alikubaliwa ombi lake aishi maisha marefu... ni uthibitisho mwingine kuwa shetani (kama yupo) ni beyond our discussion.

Yaani Mungu amsikilize na kumbariki halafu sisi tunaojiita watu wa Mungu tukeshe tukimpiga vita!!
 
Shetani au ibilisi kama kweli yupo duniani na sio dhana tu ya wajanja wa dunia ili wapige hela basi atakuwa amebeba faida kuntu kuliko hasara zake.

Moja ya faida kuntu za kuwepo shetani duniani ni kama ifuatavyo:-

(i) KUSHUSHWA NA KUANDIKWA VITABU VITAKATIFU
Mungu aliamua kushusha Quran na kuandikwa kwa biblia na vingine vingi ili Mungu ajipambanue kwenye hivyo vitabu na aoneshe kuwa yeye ndiye anafaa zaidi. Na ndani ya vitabu hivyo ibilisi ameoneshwa kuwa ni kiumbe mbaya sana na watu wamekatazwa wasimfuate. Bila ya uwepo wa ibilisi kulikuwa hakuna haya ya kuwepo kwa vitabu hivi vilivyosheheni majigambo ya Mungu.

(ii) KUSINGEKUWEPO NA MITUME WALA MANABII
Ibilisi/shetani ndiye aliyesababisha manabii na mitume waletwe duniani ili kuja kupambana na ibilisi. Bila ya kuwepo kwa Ibilisi kulikuwa hakuna haja yoyote ya kuletwa kwa mitume na manabii dunia. Wangekuja kufanya nini?

(iii) KUANZISHWA KWA DINI MBALIMBALI
Ibilisi ndiye aliyesababisha dini nyingi zianzishwe duniani kwa lengo la kupambana na majaribu ya ibilisi. Kama ibilisi asingekuwepo kulikuwa hakuna haja ya kuwepo kwa ukristo wala uislam na dini zingine.

(iv) BINADAMU ANGEKOSA WA KUMSINGIZIA MAKOSA YAKE
Binadamu anakosea makusudi na baadaye anamsingizia shetani kwamba eti shetani alinipitia. Hivi shetani asingekuwepo binadamu angemsingizia nani makosa yake?

(v) UWEPO WA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI
Kuna watu wanaitwa devil worshippers na wale wazee wa ndagu. Watu hawa wanaaminika kutusua kimaisha baada ya kumtumikia shetani na kufuata matakwa yake. Inaaminika kupitia shetani watu wengi sana wametusua kimaisha.

(vi) KUWEPO KWA TAASISI MBALIMBALI ZA KIDINI NA NYUMBA NYINGI ZA IBADA
Ibilisi ndiye aliyesababisha watu wajenge makanisa, misikiti na shule za dini,vyuo vya dini na madrassa ili wapambane kumpinga Ibilisi. Kama ibilisi asingekuwepo maana yake pia haya yote yalikuwa hayana maana yoyote kuwepo.

(vii) KUUMBWA KWA PEPO NA JEHANAMU
Ebu fikiria kama ibilisi asingekuwepo Mungu angeanzia wapi kuumba pepo na jehanamu? Ibilisi ndiye kamsukuma Mungu atengeneze vitu hivyo ili kama ukimfuata shetani mwisho wa siku uchomwe moto.

MWISHO

Ibilisi ni dude lililomshinda Mungu na akaamua kuwasukumia binadamu.
Labda nikuulize kidogo tu Alie kuumba ww ni Nani?
 
Ukitaka kutoboa chapchap "msujudu shetani " hutapenda kuiacha dunia. Dini zimetufunga akili tusijue siri ya maisha! Je kufunga macho na kuomba huoni ni "usanii "?

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Mfano ulio hai ni hawa jamaa wanaojiita manabii. Mtu anajiita nabii kumbe anamsujudu shetani na kufunga macho waumini wake huku akiwatumia na kuwaita wana kondoo wa Mungu bila wao kujijuwa kuwa ni mazezeta wanaotumiwa. We umeona wapi eti mtu anajinyima kula na kufanya la maana ili ampelekee hela nabii/baba mchungaji wake ili aishi vizuri.
 
Kwa kujibu hoja yako hapo juu, kwanza shetani alikuwa level za malaika hivyo hakuwahi kujilinganisha ubora wake na mwanadamu.
Naendelea kusisitiza ya kuwa haya mambo hamna elimu nayo.

Shetani hakuwa daraja moja na Malaika ila alipewa ofa kwa kuwa mutaabadi sana kuwazidi wengine katika majini. Malaika hawaasi ila majini na watu tuna asi. Vipi Shetani awe daraja moja na Malaika ? Hili halipo na halikuwahi kuwepo.

Najua huna ushahidi unao thibitisha ya kuwa Shetani hakujilinganisha na Mwanadamu. Sasa sijui ujasiri wa kuonyesha ujinga wako wa wazi unaupata wapi ?

Baada ya binadamu kuumbwa, Malaika na Shetani waliambiwa wamsujudie Adamu malaika walifanya hivyo isipokuwa Shetani alikaidi agizo hilo, kwa kigezo cha kuwa hawezi kumsujudia kiumbe ambaye ameumbwa kwa udobgo hali ya kuwa yeyw ameumbwa kwa Moto. Huku ni kujilinganisha tena kwa kufanya kiburi.
 
Pia, hicho unachokisema kuwa alikubaliwa ombi lake aishi maisha marefu... ni uthibitisho mwingine kuwa shetani (kama yupo) ni beyond our discussion
Beyond vipi wakati tunamjua na tunajua njia za kumuepuka.
Yaani Mungu amsikilize na kumbariki halafu sisi tunaojiita watu wa Mungu tukeshe tukimpiga vita!!
Kuruhusiwa ni jambo moja kubarikiwa ni jambo lingine.

Allah anawaruzuku mpaka wanao mkana na hili liko wazi, na kama angetaka pia aisngemruhusu.

Shetani amelaaniwa na ataishi motoni milele, na hajabarikiwa kwa lolote wala kwa chochote.
 
Naendelea kusisitiza ya kuwa haya mambo hamna elimu nayo.

Onesha hapa hiyo elimu unayodhani unayo, huenda mimi sina basi nitarajie kujifunza kwako.

Shetani hakuwa daraja moja na Malaika ila alipewa ofa kwa kuwa mutaabadi sana kuwazidi wengine katika majini. Malaika hawaasi ila majini na watu tuna asi. Vipi Shetani awe daraja moja na Malaika ? Hili halipo na halikuwahi kuwepo.

"Alipewa" ofa!
Kama unakiri alipewa ofa kuwazidi wengine mbona unajipinga na kutotambua ukuu wake?

Ninachojua mimi shetani alikuwa mmoja wa malaika wakubwa tu, kuhusu majini sijui tofauti yake na malaika.

Najua huna ushahidi unao thibitisha ya kuwa Shetani hakujilinganisha na Mwanadamu. Sasa sijui ujasiri wa kuonyesha ujinga wako wa wazi unaupata wapi?
Nahitaji ushahidi gani kuhusu hilo?
Shetani kama malaika au jini kama unavyomuita, hawezi kuwa daraja la mwanadamu kiasi cha kujilinganisha.

Baada ya binadamu kuumbwa, Malaika na Shetani waliambiwa wamsujudie Adamu malaika walifanya hivyo isipokuwa Shetani alikaidi agizo hilo, kwa kigezo cha kuwa hawezi kumsujudia kiumbe ambaye ameumbwa kwa udongo hali ya kuwa yeye ameumbwa kwa Moto. Huku ni kujilinganisha tena kwa kufanya kiburi.

Aisee hii ni kali, nahisi hii ID ya Zurie imedukuliwa.... kuna muda niliwahi kuamini kuwa una uelewa wa mambo haya kumbe nilijikosea pakubwa!

Eti Mungu awaambie malaika wamsujudie Adamu, hivi unaelewa maana ya kusujudia wewe!

Na kama utathibitisha hili pasipo mashaka, nitazidi kumheshimu shetani kwa vile aligoma kumsujudia Adamu... kitu ambacho ni Mungu pekee anayestahili kusujudiwa.

Come to your senses.
 
Naendelea kusisitiza ya kuwa haya mambo hamna elimu nayo.

Shetani hakuwa daraja moja na Malaika ila alipewa ofa kwa kuwa mutaabadi sana kuwazidi wengine katika majini. Malaika hawaasi ila majini na watu tuna asi. Vipi Shetani awe daraja moja na Malaika ? Hili halipo na halikuwahi kuwepo.

Najua huna ushahidi unao thibitisha ya kuwa Shetani hakujilinganisha na Mwanadamu. Sasa sijui ujasiri wa kuonyesha ujinga wako wa wazi unaupata wapi ?

Baada ya binadamu kuumbwa, Malaika na Shetani waliambiwa wamsujudie Adamu malaika walifanya hivyo isipokuwa Shetani alikaidi agizo hilo, kwa kigezo cha kuwa hawezi kumsujudia kiumbe ambaye ameumbwa kwa udobgo hali ya kuwa yeyw ameumbwa kwa Moto. Huku ni kujilinganisha tena kwa kufanya kiburi.
Kumbe biblia imeandika uongo?
 
Huu UONGI wa wazi kabisa. Sababu ya kuja kwa mitume na manabii ni baada ya watu kuanza kufanya shirki. Muda ambao Shetani alikuwepo tayari na laana ilikuwa imeshamfikia.

Lakini msilolijua ni kuwa Shetani alikuwa mja mwema na aliwekwa katika kundi moja na Malaika. Lakini kwa kiburi na ujinga wake akaasi.

Vipi muumba ashindwe na alicho kiumba ?

Pili, hitimisho lako linahitaji sana ushahidi kuliko uwepo wa mada yako yenyewe.

Nimecheka sana. Pepo na Moto vipo hata kabla ya Shetani kuwepo.

Shetani pale alipo muasi Allah aliye juu, alikuwa yupo peponi. Sasa unapo tuandikia uongo sijui kama unakijua unacho kiandika au la ?

Viumbe wa mwisho kuumbwa ni Majini na Binadamu, bali wa mwishi kabisa ni Binadamu. Maana yake kabla ya Shetani na sisi kuumbwa, pepo na Moto vilikuwepo kitambo sana.

Hizo nukta nyingine nilizo ziacha ni nyepesi sana, mpaka napata uvivu wa kukujibu.
Hahahaha mkuu umenichekesha Sana.

Hivi bila ya uwepo wa shetani duniani Mungu angeleta mitume na manabii waje wafanye nini duniani.

Nimekuambia ujio wa mitume na manabii duniani ni kuja kupinga kile kinachoitwa uasi wa shetani hivyo shetani ndiyo amepelekea mitume waletwe duniani ili kuwaokoa watu na harakati za shetani.

Mungu anaumbaje moto kabla ya shetani kuasi! Bila ya shetani kuasi na kudanganya watu kama jinsi inavyosema basi moto hauna kazi yoyote kwani kungekuwa hakuna maasi hivyo hakuna mtu ambaye angechomwa moto.

Ebu fikilia bila ya shetani kumuasi Mungu moto ungekuwepo wa nini?
 
Onesha hapa hiyo elimu unayodhani unayo, huenda mimi sina basi nitarajie kujifunza kwako.
Nimeanza kuionyesha tangu nilipo anza kuchangia huu uzi. Kwahiyo unachotakiwa kufanya ni kutuliza akili na kusoma hoja kisha uzielewe.
"Alipewa" ofa!
Kama unakiri alipewa ofa kuwazidi wengine mbona unajipinga na kutotambua ukuu wake?

Ninachojua mimi shetani alikuwa mmoja wa malaika wakubwa tu, kuhusu majini sijui tofauti yake na malaika.
Naendelea kuonyesha ujinga wako. Hakuna sehemu niliyo jipinga, sababu nimekuelezea nyakati mbili za Shetani, kabla alikuwa mja mwema lakini baadae akakaidi agizo la Mola wake na wema wake kupomoka, kisha akalaniwa. Sasa kilicho laaniwa hakiwezi kuwa na hadhi. Laiti ungesoma hoja yangu kwa umakini huu ujinga usingeuuliza tena.

Usiseme tu Shetani alikuwa mmoja wa Malaika, bali unatakiwa ututhibitishie huo Umalaika wa Shetani ulikuwa lini na marejeo yako ni wapi. Hatupo vijiweni hapa.
Nahitaji ushahidi gani kuhusu hilo?
Shetani kama malaika au jini kama unavyomuita, hawezi kuwa daraja la mwanadamu kiasi cha kujilinganisha.
Sasa unaposema hawezi kujilinganisha hali ya kuwa alijilinganisha na kujiona yeyw ni bora kuliko Mwanadamu kisha kwa kiburi chake akakaidi agizo la Mola wake, wewe nakuona ni mjinga usiyejua unachokijadili. Bali unapoteza muda kwenye hakuna, huwezi kupingana na uhalisia.
Aisee hii ni kali, nahisi hii ID ya Zurie imedukuliwa.... kuna muda niliwahi kuamini kuwa una uelewa wa mambo haya kumbe nilijikosea pakubwa!
Hili halinipunguzii wala haliniongezei kwa lolote. Tujikite kwenye mada na hoha zenye nguvu.

Sisi wenzako huwa tunajua kwanza kisha tunaamini.
Eti Mungu awaambie malaika wamsujudie Adamu, hivi unaelewa maana ya kusujudia wewe!
Naelewa sana maana ya kusujudia na hapa nimeliweka tamko mahala pake. Tamko hilo limekuja katika muktadha wa kuonyesha utiifu na si kuabudu bali kuheshimu, na hili lilithibitika baadae baada ya kuwauliza malaika na Shetani wataje majina ya vitu wakashindwa ila Adamu akavitaja.
Na kama utathibitisha hili pasipo mashaka, nitazidi kumheshimu shetani kwa vile aligoma kumsujudia Adamu... kitu ambacho ni Mungu pekee anayestahili kusujudiwa.
Kusujudu katika tukio hili ni kwa heshima na si kuabudu. Weka akilini hilo.
 
Ebu fikilia bila ya shetani kumuasi Mungu moto ungekuwepo wa nini?
Sasa unaukiza vipi swali la kitoto na nimeshalijibu huko juu, ya kuwa Moto upo hata Shetani hajulikani, Shetani alikuwa anaabudu huko awali na mwingi wa kufanya ibada, maana yake moto ulikuwepo kabla na pepo ilikuwepo.

Kijana acha kuparamia mambo yaliyo kuzidi ukajiona unahoji kumbe unatumia akiki vibaya kwa ujinga wako.
 
Naendelea kuonyesha ujinga wangu, hakuna sehemu niliyo jipinga.

Naelewa sana maana ya kusujudia na hapa nimeliweka tamko mahala pake. Tamko hilo limekuja katika muktadha wa kuonyesha utiifu na si kuabudu bali kuheshimu, na hili lilithibitika baadae baada ya kuwauliza malaika na Shetani wataje majina ya vitu wakashindwa ila Adamu akavitaja.

Kusujudu katika tukio hili ni kwa heshima na si kuabudu. Weka akilini hilo.

Naomba nihitimishe kwa kusema machache, kauli yako kuhusu tofauti ya kuabudu na kusujudu imetosha kuthibitisha pasi na shaka yoyote... ya kuwa wewe ni mjinga mjinga fulani hivi aliyechangamka.

Ila ni mjuaji na kuna kundi kubwa nyuma yako linakukubali na kukuamini kinyama, hivyo limekutia upofu na kuvimba bichwa.

Siwezi tena kuendelea kujishughulisha na wewe katika hili, you are no match kwa mambo yenye kuhitaji uelewa na ukomavu kama haya.

Umetaja ujinga mara nyingi kwenye kujenga hoja zako, ni mbinu yako ya kujilinda na kuficha ujinga wako... nachagua kukuacha nao.

Cheers
 
Hivi ndivyi nilivyo mimi. Nuru inapo ingia Giza hushika njia.

Nilijua tu huna uwezo wa kujibu hoja zangu, na hutoweza sababu kuna tofauti kati ya dhana na Elimu. Hapa nazungumzia ELIMU.

Kazi yangu nimemaliza.
 
Nimekuambia ujio wa mitume na manabii duniani ni kuja kupinga kile kinachoitwa uasi wa shetani hivyo shetani ndiyo amepelekea mitume waletwe duniani ili kuwaokoa watu na harakati za shetani.
Sasa hili siyo lengo ndiyo maana maneno yako yanabaki kuwa ya UONGO.

Sababu ya mitume na manabii kuletwa nimeshaiweka huko awali.
Mungu anaumbaje moto kabla ya shetani kuasi! Bila ya shetani kuasi na kudanganya watu kama jinsi inavyosema basi moto hauna kazi yoyote kwani kungekuwa hakuna maasi hivyo hakuna mtu ambaye angechomwa moto.
Shida yako kijana huna marejeo zaidi ya hisia na kuhangaika, haya yako wazi. Lengo la kuumbwa Majini na Watu, wote tumuabudu Mola aliye juu, ndiyo maana moto ukawepo na pepo vikawepo kabla ya kuumbwa viwili hivi.
 
Back
Top Bottom