GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Shetani au ibilisi kama kweli yupo duniani na sio dhana tu ya wajanja wa dunia ili wapige hela basi atakuwa amebeba faida kuntu kuliko hasara zake.
Moja ya faida kuntu za kuwepo shetani duniani ni kama ifuatavyo:-
(i) KUSHUSHWA NA KUANDIKWA VITABU VITAKATIFU
Mungu aliamua kushusha Quran na kuandikwa kwa biblia na vingine vingi ili Mungu ajipambanue kwenye hivyo vitabu na aoneshe kuwa yeye ndiye anafaa zaidi. Na ndani ya vitabu hivyo ibilisi ameoneshwa kuwa ni kiumbe mbaya sana na watu wamekatazwa wasimfuate. Bila ya uwepo wa ibilisi kulikuwa hakuna haya ya kuwepo kwa vitabu hivi vilivyosheheni majigambo ya Mungu.
(ii) KUSINGEKUWEPO NA MITUME WALA MANABII
Ibilisi/shetani ndiye aliyesababisha manabii na mitume waletwe duniani ili kuja kupambana na ibilisi. Bila ya kuwepo kwa Ibilisi kulikuwa hakuna haja yoyote ya kuletwa kwa mitume na manabii dunia. Wangekuja kufanya nini?
(iii) KUANZISHWA KWA DINI MBALIMBALI
Ibilisi ndiye aliyesababisha dini nyingi zianzishwe duniani kwa lengo la kupambana na majaribu ya ibilisi. Kama ibilisi asingekuwepo kulikuwa hakuna haja ya kuwepo kwa ukristo wala uislam na dini zingine.
(iv) BINADAMU ANGEKOSA WA KUMSINGIZIA MAKOSA YAKE
Binadamu anakosea makusudi na baadaye anamsingizia shetani kwamba eti shetani alinipitia. Hivi shetani asingekuwepo binadamu angemsingizia nani makosa yake?
(v) UWEPO WA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI
Kuna watu wanaitwa devil worshippers na wale wazee wa ndagu. Watu hawa wanaaminika kutusua kimaisha baada ya kumtumikia shetani na kufuata matakwa yake. Inaaminika kupitia shetani watu wengi sana wametusua kimaisha.
(vi) KUWEPO KWA TAASISI MBALIMBALI ZA KIDINI NA NYUMBA NYINGI ZA IBADA
Ibilisi ndiye aliyesababisha watu wajenge makanisa, misikiti na shule za dini,vyuo vya dini na madrassa ili wapambane kumpinga Ibilisi. Kama ibilisi asingekuwepo maana yake pia haya yote yalikuwa hayana maana yoyote kuwepo.
(vii) KUUMBWA KWA PEPO NA JEHANAMU
Ebu fikiria kama ibilisi asingekuwepo Mungu angeanzia wapi kuumba pepo na jehanamu? Ibilisi ndiye kamsukuma Mungu atengeneze vitu hivyo ili kama ukimfuata shetani mwisho wa siku uchomwe moto.
MWISHO
Ibilisi ni dude lililomshinda Mungu na akaamua kuwasukumia binadamu.