Hizi ndizo faida kuntu za kuwepo shetani na ibilisi duniani

Kwanza shetani ni an illusion tu, ila uwepo wa dhana hiyo ni fursa na faida kubwa.

Shetani hana watetezi, wala hajawahi kujigamba wala kujitetea sehemu... lakini Mungu katumia timu na nguvu nyingi mno kumchafua/kumshusha shetani na bado anadunda!
sasa what if nayeye angekuwa na timu inayo mtetea !? Mungu angetafuta chimbo la kujigicha bila shaka
 
Wafia dini bwana! Badala ya kujibu kwa hoja mnaanza kutisha watu...

Binafsi siamini kama kuna kiumbe wa kuitwa shetani. Shetani ni imaginary character aliyetengenezwa na binadamu ili yeye (binadamu) apate uwezo wa kukwepa kuwajibika kwa makosa yake mwenyewe.

Mungu yupo
Shetani hayupo
Dhambi haipo
Nakazia
 
sasa what if nayeye angekuwa na timu inayo mtetea !? Mungu angetafuta chimbo la kujificha bila shaka

Shetani (kama yupo), hana mbwembwe... kila siku timu pinzani ni kumshambulia tu wala hajisumbui kuwajibu.
 
Kwa kujibu hoja yako hapo juu, kwanza shetani alikuwa level za malaika hivyo hakuwahi kujilinganisha ubora wake na mwanadamu.

Pia, hicho unachokisema kuwa alikubaliwa ombi lake aishi maisha marefu... ni uthibitisho mwingine kuwa shetani (kama yupo) ni beyond our discussion.

Yaani Mungu amsikilize na kumbariki halafu sisi tunaojiita watu wa Mungu tukeshe tukimpiga vita!!


Great thinker
 
Badala kupinga kwa facts mnaanza kumtisha.
Maana yake ufahamu wenu umefungwa msifikirie nje ya box lenu.

Hii ina maana wote mnaompinga mleta mada mnapinga sababu ya uoga.
 
Shetani au ibilisi kama kweli yupo duniani na sio dhana tu ya wajanja wa dunia ili wapige hela basi atakuwa amebeba faida kuntu kuliko hasara zake.

Moja ya faida kuntu za kuwepo shetani duniani ni kama ifuatavyo:-

(i) KUSHUSHWA NA KUANDIKWA VITABU VITAKATIFU
Mungu aliamua kushusha Quran na kuandikwa kwa biblia na vingine vingi ili Mungu ajipambanue kwenye hivyo vitabu na aoneshe kuwa yeye ndiye anafaa zaidi. Na ndani ya vitabu hivyo ibilisi ameoneshwa kuwa ni kiumbe mbaya sana na watu wamekatazwa wasimfuate. Bila ya uwepo wa ibilisi kulikuwa hakuna haya ya kuwepo kwa vitabu hivi vilivyosheheni majigambo ya Mungu.

(ii) KUSINGEKUWEPO NA MITUME WALA MANABII
Ibilisi/shetani ndiye aliyesababisha manabii na mitume waletwe duniani ili kuja kupambana na ibilisi. Bila ya kuwepo kwa Ibilisi kulikuwa hakuna haja yoyote ya kuletwa kwa mitume na manabii dunia. Wangekuja kufanya nini?

(iii) KUANZISHWA KWA DINI MBALIMBALI
Ibilisi ndiye aliyesababisha dini nyingi zianzishwe duniani kwa lengo la kupambana na majaribu ya ibilisi. Kama ibilisi asingekuwepo kulikuwa hakuna haja ya kuwepo kwa ukristo wala uislam na dini zingine.

(iv) BINADAMU ANGEKOSA WA KUMSINGIZIA MAKOSA YAKE
Binadamu anakosea makusudi na baadaye anamsingizia shetani kwamba eti shetani alinipitia. Hivi shetani asingekuwepo binadamu angemsingizia nani makosa yake?

(v) UWEPO WA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI
Kuna watu wanaitwa devil worshippers na wale wazee wa ndagu. Watu hawa wanaaminika kutusua kimaisha baada ya kumtumikia shetani na kufuata matakwa yake. Inaaminika kupitia shetani watu wengi sana wametusua kimaisha.

(vi) KUWEPO KWA TAASISI MBALIMBALI ZA KIDINI NA NYUMBA NYINGI ZA IBADA
Ibilisi ndiye aliyesababisha watu wajenge makanisa, misikiti na shule za dini,vyuo vya dini na madrassa ili wapambane kumpinga Ibilisi. Kama ibilisi asingekuwepo maana yake pia haya yote yalikuwa hayana maana yoyote kuwepo.

(vii) KUUMBWA KWA PEPO NA JEHANAMU
Ebu fikiria kama ibilisi asingekuwepo Mungu angeanzia wapi kuumba pepo na jehanamu? Ibilisi ndiye kamsukuma Mungu atengeneze vitu hivyo ili kama ukimfuata shetani mwisho wa siku uchomwe moto.

MWISHO
Ibilisi ni dude lililomshinda Mungu na akaamua kuwasukumia binadamu.
Ibilisi amekuwa sababu ya kutajirisha wengi wanaompenda na wasio mpenda
 
MWISHO
Ibilisi ni dude lililomshinda Mungu na akaamua kuwasukumia binadamu.


Maji tu yakikupalia au ukishikwa na kichomi cha moyo haya maneno yote utayakana.. na within a minute utajikuta umetubu dhambi zako zote haijalishi unamuamini au wamuamini...Tulifika Near death experience we know a bit about how death it's like. Chung sana, It's supper scary..Pumzi zako hizi unazovuta kwa uhuru zisikufanye ujione mwamba. It's matter of button, ikibonyezwa tukubadilisha jina kabisa. Be humble dogo..Be Kind
Lucifer ni kiumbe kilichoumbwa ili kuthibitisha ubaya wa "power of negativity" pale inapokinzana na "power of positivity'. Nguvu hizi mbili huthibitika tu pale panapotokea utashi wa kuamua juu yake.

Miti ile ya uzima, na ule wa ujuzi wa mema na mabaya ndani ya Bustani ya Edeni unathibitisha jambo hili. Wote Lucifer na Adam waliishi katika Bustani za Edeni ili waweze kupimwa uhuru wao wa kufanya maamuzi sahihi na kuthibitisha utii wao kwa Muumbaji wao, lakini wote wawili licha ya kuumbwa katika ukamilifu, lakini wote mtihani ukawashinda (Mwanzo 2:8-17; Ezekieli 28:13-17).

Naamini Bustani moja ya Edeni ilikuwa katika sayari ya Mars, na nyingine ikawa hapa katika sayari yetu ya Earth. Moja ikiwa ni makazi ya asili ya kiroho, na nyingine ikiwa makazi asili ya mwili ulioumbwa kwa mwili wa nyama, vyote vikifanyika hivyo kama "case study" yenye kuthibitisha ubaya wa dhambi.
 
God & Satan ni fiction characters ambao hawajawahi exist popote

Ni illusion tu na Hoax watu walikaa wakashiba wakaamua watengeze ma imagination Kwa bichwa zao Ili tu kujifariji wanapokutana na changamoto,
Zile zinazowapa faida wakaita
God
Zile zinazo waumiza wakaita
Satan

Mchezo ukaisha matokeo yakawa
0-0 game likafungwa!
 
Back
Top Bottom