Hizi ndiyo Mbinu za wizi wa kura hususani barani Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndiyo Mbinu za wizi wa kura hususani barani Afrika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dullo, Mar 22, 2012.

 1. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  • Kuhonga mawakala wa vyama vingine kwa gharama yeyote ili kuruhusu matokeo kubadilishwa. Hili linadhibitika ikiwa mawakala watasimamia maadili ya uwakilishi wa vyama vyao kwa uaminifu bila kutanguliza njaa.
  • Kuweka vituo hewa vya kupigia kura, hasa katika maeneo ambayo si rahisi mwananchi wa kawaida anaweza kuhoji i.e kwenye kambi za jeshi n.k. Pia kunaweza kuwekwa vituo hewa ambavyo vinakuwa na majina hewa mengi huku wapiga kura wengi wakishindwa
   kupiga kura.
  • Kuukimbia na masanduku ya kura..
  • Ushiriki wa vyombo vya kiserikali vyenye dhamana ya kusimamia haki, lakini badala yake vinaamua kuwa upande wa chama kinachotaka kushinda kwa wizi. Mfano Tume ya Uchaguzi n.k
  • Kununua shahada za kupigia kura ili waliouza shahada zao wasiweze kuwa na ruhusa ya kupiga kura.
  • Kutumia Polisi kutisha wapiga kura kwenye zoezi la kupiga kura na hata wakati wa kuhesabu kura.
  • Kusambaza Form chache sana kwenye vituo, zile fomu zinazoruhusu asie na kitambulisho ama kimeharibika details fulani aruhusiwe kupiga kura. Ni rahisi kuambiwa hizo form hazipo au hazijaletwa kituoni.
  • Kuondoa baadhi ya majina ya wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.
  • Kuharibu majina ya wapiga kura yaonekane yamekosewa ama hayafanani na picha ya mhusika
  • Kubandika majina siku chache sana kabla ya siku ya uchaguzi, muda ambao hauwaruhusu ambao majina yao hayapo au yamekosewa kuweza kufanya marekebisho
  • Kuchanganya majina ya wapiga kura na vituo. Mfano aliejiandikisha kituo A, jina lake unalikuta kituo B na pengine ikawa ni mbali sana na anapoishi
  • Kuingiza maboksi yaliyojaa kura zilizopigwa tayari za chama kinachotaka kuiba, aidha wakati wa kusafirisha ama wakati zimefungiwa ndani. hii ya wakati wa usafirishaji inawawia ugumu kwasababu mfumo wa kuhesabia kura kila kituo unaleta shida.
  • Wakati mwingine kura zikihesabiwa katika jengo ambalo lina ceiling kwa ndani wanaweza kuwaambia mawakala kwenda kupata chakula na milango inafungwa vizuri lakini kumbe kwa juu ya dari anakuwepo mtu alieandaliwa na mabox yake yenye kura ambazo zimepigwa, nyingi zikiegemea upande wa chama kinachotaka kuiba, mawakala wkiwa nje wanakula yule mtu darini anashuka na kuweka zakwake zilizoandaliwa.
  • Usalama wa nchi wakati mwingine unaweza kuhusika moja kwa moja katika wizi kwa kutumia nafasi yao ya kusimamia usalama, kwa kuvujisha siri za mwenendo wa uchaguzi!
  • Mbinu nyingine ambayo huwa wanaitumia ni kuj√≠fanya wema sana kwa wakala hasa yule wa chama ambacho kina nguvu, kwa kumpatia chakula ambacho akila tumbo linavurugika na anaanza kwenda chooni mara kwa mara na wao kutumia nafasi hiyo kuweka kura zisizo rasmi.
  • Kunayo taarifa za kuwako mbinu mpya ya kiteknolojia kwa zile fomu za majumuisho. Inaelezwa kuwa hii ndio mbinu kuu iliyo na nguvu kwasababu mara nyingi mawakala wakishasaini fomu moja na kubakia na kopi moja wanadhani wamemaliza. Ila wakati zinapelekwa kwenye majumuisho zinakuwa sio zile walizosaini mawakala. Kunakuwa na fomu nyingine kama ile ile lakini inajazwa pembeni!!
   
 2. d

  dada jane JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh hiyo kali lkn yote hiyo ili iweje. Ninachoamini kiongozi bora na mzuri ni yule alietokana na takwa la wale atakaowaongoza
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nimependa hiyo ya kutoka NDUKI na MASANDUKU YA KURA. Dr(?) Makongoro Mahanga ali-apply hiyo strategy.

  ILa umesahau nyingine, sehemu ambayo chama cha UPINZANI kina Nguvu wasimamizi wa uchaguzi deliberately kutopiga MHURI kwa nyuma kwenye karatasi ya kura baada ya mtu kupiga kura. Katika kuhesabu kura karatasi zote za kura ambazo hazikupigwa muhuri kwa nyuma na msimamizi wa kituo huwa zinahesabika zimeharabika.
   
 4. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wOW!! this is interesting!!
  yaani hayo yote ni kuvizia hizo kazi zisizohitaji kutumia akili Loh!!
  By the way kwa nini Sioi kakubali kurithi kiti cha baba yake?
  Je, huo ni ubani anaopewa na ccm baada ya mdingi wake kufanyiziwa au kusaidia kwenye zile dili za richmond na EPA?
   
 5. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  tatizo la wabongo uzushi ni desturi yao
   
 6. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,642
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  kuna hii nyingine ya kuingiza kura feki zinaletwa ndani ya hotpot la chakula wakati wakupata msosi
   
 7. R

  Rwechu Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu hebu fafanua mbinu hyo hapo chini.
  Kunayo taarifa za kuwako mbinu mpya ya kiteknolojia kwa zile fomu za majumuisho. Inaelezwa kuwa hii ndio mbinu kuu iliyo na nguvu kwasababu mara nyingi mawakala wakishasaini fomu moja na kubakia na kopi moja wanadhani wamemaliza. Ila wakati zinapelekwa kwenye majumuisho zinakuwa sio zile walizosaini mawakala. Kunakuwa na fomu nyingine kama ile ile lakini inajazwa pembeni!!
   
 8. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kaazi kweli kweli!!
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hfai kuwa wakala tena wewe kama hayo yote mmeyafanya wewe na chama chako ni hatari kwa sababu huwezi kuyajua hayo kama hujawhi kuwa wakala. kama hujawahi kuwa wakala basi wewe mtaalamu wa kupiga majungu.
   
 10. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Dada Jane, una umri gani? Je unaishi Tanzanai au Africa for that matter?

  Je unafikiri uchoamini wewe ndiyo kila mtu anaachoaimini? hasa watawala wetu? Open your eyes Jane, things are not black and white as you want us to believe.
   
Loading...